Serikali, Bunge na Mahakama Tanzania - Utatu uliolaaniwa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali, Bunge na Mahakama Tanzania - Utatu uliolaaniwa.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kapotolo, Feb 19, 2011.

 1. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #1
  Feb 19, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,717
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Tunayo mihimili rasmi mitatu ya dola ambayo kazi yake kubwa ni kusimamia shughuli za umma na kuwaletea maendeleo wananchi. Tuna serikali, Mahakama na Bunge. Kwa nchi yetu mihimili hii imekuwa ni kero kubwa kwa watanzania badala ya kusimamia maendeleo, imekuwa chanzo na kudidimiza maendeleo na haki.

  1)Serikali.
  Ingetakiwa kuwa mfano lakini ni kinyume chake, Serikali :-
  a)Imeshindwa Kusimamia uwajibikaji na kubariki wizi kwa kutumia mikataba feki bila kuwachukulia hatua wezi hao japo inawafahamu na wengine kuwapa vyeo serikalini na kwenye chama.
  b) imeshindwa kudhibiti mfumuko wa bei na kushuka kwa thamani ya shilingi
  c)imeshindwa kusimamia demokrasia, uchaguzi mkuu matokeo kutangazwa kukiwa na kura zilizopotea (Shinyanga) na zisizohesabiwa, Uchaguzi wa Meya arusha kufanywa na wajumbe chini ya 2/3, haki ya kuandamana imeondoka n.k.
  d) imeshindwa Kujua vipaombele muhimu vya taifa, wabungwe mil 90 kwa ajili ya mashangingi, akina mama Bajaji ambulance, tusubiri akina mama watakavyokufa kwa 'abruptio placenta' kwa mitikisiko ya bajaji
  e)imeshindwa kutupatia umeme wa uhakika na viongozi kujinufaisha kwa ukosefu wa umeme.
  f) Imeshindwa kusimamia elimu, wako tayari waingize 100 wakifaulu 11 shauri yao
  g) kwenye ajira, zimeongoezeka mil 1 za kuokota makopo.
  h)Mizaha kwenye mambo mazito:
  - wanaopata ukimwi na mimba ni kiherehere chao
  - Dowans siwajui na hawanihitaji - Mwenyekiti wa baraza la mawaziri
  - tukio la mbagala ni tofauti na gongo la mboto kwa hiyo sijiuzulu.
  - Swala la mgao wa umeme litakuwa historia, sikia mikakati utalia
  - n.k.

  2) Mahakama- huku nako ndio haki inabadilishwa kwa dola, utasikia hukumu zenye utata, mtu anaua anashitakiwa kwa uzembe na faini laki 700,000/ (sijui ndio thamani ya damu lita 10,000 za watu wawili zilomwagika), imeshindwa kutoa haki kwa wazee wa EAC na kuwapiga kalenda zizisokwisha, nk.

  3) Bunge - Hasa hili la kumi ndio hovyo kabisa, ni mipasho kwa kwenda mbele, bunge limekosa mvuto, halina tija kwa taifa, wabunge badala ya kujadili mambo ya msingi ni kujadili upuuzi na kuulizia mil 90 zao zitaingia lini kwenye account zao.

  Kumbukeni: Watanzania hawatakuwa wajinga milele, naamini siku moja wataamka na kudai haki zao. Sauti ya umma ni sauti ya Mungu endeleeni kuipuuza.
   
 2. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #2
  Feb 19, 2011
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,357
  Likes Received: 467
  Trophy Points: 180
  Si kitambo sana ya MUBARAK yanakuja hapa.
   
 3. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,717
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Yanachelewa, natamani ingekuwa leo.
   
 4. T

  Taso JF-Expert Member

  #4
  Feb 19, 2011
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,531
  Likes Received: 250
  Trophy Points: 160
  Mahakama na Serikali angalau ni career oriented professionals fulani hivi. Bunge ni watu watu wameokotwa okotwa kwenye matawi ya vyama hawana professional track record yeyote. Matokea yake serikali kwa kutumia Waziri Mkuu wanakuja Bungeni kuwaburuza buruza kama ngamia.

  Angalia jinsi Waziri Mkuu anavyochukua center stage bungeni, kuanzia kufungua, kuongea kila siku, kufunga bunge. Last say jana ilitolewa na Pinda, akasema "wote tumeona kabisa kwamba Bunge limeenda vizuri na Spika unaweza kabisa kuliongoza Bunge." Akamaliza na Bunge likafungwa. Hakuna aliyedai fursa kupinga hilo, kusema "Pinda speak for your freaking self." Wamelala pono.
   
 5. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #5
  Feb 19, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,717
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  I completely agree.
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  Feb 19, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,752
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  NDO MAANA MIMI NASEMA PUMBAVU ZAO! b
   
 7. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #7
  Feb 19, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,717
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  "….huku kwetu kuna kuwajibika pindi inapotakiwa uwajibike siyo kujiuzulu…na hadi sasa bado haijabainika nini chanzo cha milipuko hiyo hivyo tuachane na maneno yanayozagaa na hisia ambazo hazijengi nchi tusubiri ripoti ya uchunguzi ndiyo itatupa jibu," alisema Brigedia Jenerali Meela

  Hivi kuwajibika jeshini ni nini? Ni kuchapwa viboko au kupigishwa kwata?
   
Loading...