Serikali bila kufungua viosk vya kukatia tiketi hili la electronic ticket hamtoweza, wajanja wa mabasi ndio tegemeo lao kukwepa kodi

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,824
2,000
Wana JF,

Baada ya Serikali kutoa tamko la kukata ticket kieletroniki sasa wafanyabiashara wa Mabus kwa kushirikiana na brokers au madalalie wa ticket. Kibaya zaidi hupewi ticket baada ya kutoa fedha.

Leo nimejifunza kitu gari no. T 195DAV KVC Safari karibu abaria wote hawana ticket. Jambo ambalo ni hatari, akitokea la kutokea hatujui hatima yetu.

Leo gari la Harambee limeharibika njiani baada ya kumaliza mto wami abiria tukafaulishwa. Baadaye tuko njiani tukadaiwa upya, tumebishana hadi mwisho sisi tukawa na hatia ya kutopewa ticket ikala kwetu.

Nimejaribu kushitaki kwa traffic mombo bila mafanikio traffic akaniambia niende nishitaki mwisho wa gari kwani safari bado ndefu. Mtindo Huu tutaumia wengi, bora traffic wawe wanaingia ndani kukagua ticket vinginevyo serikali itapoteza mapato na akitokea ajari kunakupoteza insurance.

Kampuni za kuanzia njia ya Boko - Bunju hawakati electronic.
 
Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
32,034
2,000
Tatizo lipo Kwa watu wa njiani baada ya business kutoka kituoni yaani wote hawana ticket yakitokea ajari hata kujua majina Yao shida hata msaada wa karibu hakuna...
Mimi sijasafiri tokea haya mambo ya ticket za electronic yaanza,naomba nikuulize swali:Mtu akishakata ticket ya electronic na akafika kwenye basi anapaswa kupewa ticket ya hard copy(ticket ya karatasi)?
 
mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,824
2,000
Mimi sijasafiri tokea haya mambo ya ticket za electronic yaanza,naomba nikuulize swali:Mtu akishakata ticket ya electronic na akafika kwenye basi anapaswa kupewa ticket ya hard copy(ticket ya karatasi)?
Mimi nimekatia kwenye vibandani umiza vilivyowekwa barabarani kama wakala. Hivyo nilitafuta site ya kukatia ticket ikazingua ndipo nilienda kukutana Na maafa, wakala wanatoa ticit zilizokatazwa
 
BABAREY

New Member
Dec 6, 2020
2
20
Nilishalipa nauli kwa mfumo huo miaka miwili ilopita, unapata sms kwa simu yako na pia wanakupa na risiti ya malipo ambapo zote zinakutambua hadi kiti chako cha abiria
 
Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
16,434
2,000
Leo nimejifunza kitu gari no. T195DAV KVC Safari karibu abaria wote hawana ticket. Jambo ambalo ni hatari, akitokea la kutokea hatujui hatima yetu.

Leo gari la Harambee limeharibika njiani baada ya kumaliza mto wami abiria tukafaulishwa. Baadaye tuko njiani tukadaiwa upya, tumebishana hadi mwisho sisi tukawa na hatia ya kutopewa ticket ikala kwetu.
Kwahiyo umepanda mabasi matatu kwa safari moja
 
Stefano Mtangoo

Verified Member
Oct 25, 2012
4,846
2,000
Kwenye hili la Ticketing, nadhani serikali inapaswa ifikirie upya. Kwanza LATRA wangebakia kuwa regulators na kuwaacha wafanyabiashara wa makampuni ya IT yafanye biashara. LATRA waweke standards ambazo vendors watahakikisha wanazifuata ili kupewa leseni.

Kuna changamoto kadhaa hapo
1. Wenye mabasi kutengeneza mifumo yao wenyewe. Hili wasiruhusu kwa sababu ya conflict of interest.

2. Vendors wanaweza kudanganya. Kuzuia udanganyifu, LATRA wata setup system ya monitoring ambayo kila vendor atajiunga kama sehemu ya masharti ya leseni yake

3. Askari atakuwa na app kwenye simu iliyounganishwa na monitoring server kwa ajili ya ukaguzi na kusaidia kuzuia fraud ya vendor.

Faida za open market kuliko serikali au kampuni chache kuhodhi kazi ya kufanya tiketi ni

1. Kuongeza ajira. Kampuni zitazaliwa na zingine kukua na hivyo kuongeza wigo wa serikali kukusanya kodi. Latra pia watapata fedha kwenye utoaji wa leseni.

2. Kwa sababu ya mashindano kati ya vendors, bei ya huduma kwa wenye mabasi itashuka, na wamiliki wa mabasi watapata huduma bora toka kwa vendors. Kwa hiyo soko litakuwa na gharama fair na huduma bora. Vendor ambaye atatoa huduma mbovu au bei ghali, atakosa wateja na atajiondoa kwenye soko mwenyewe.

3. Baada ya muda soko la Bongo litakuwa saturated na haya makampuni yatalazimika kutafuta soko la nje. Hapa tena serikali itavuna kodi ya ziada kwa sababu mwisho wa siku fedha ya huko itarudi huku nyumbani kwenye kampuni mama.

Kwa hiyo ushauri wangu kwa serikali kupitia Wizara na LATRA ni kuwa waliache soko liwe huru bila limitation, wao waweke vigezo na masharti ili wataalamu wa Software Development wa Tanzania wachuane kutengeneza mifumo bora, watengeneze ajira na kulipa kodi.

Serikali kupitia viongozi wetu imekuwa inatutia moyo vijana tujiajiri. Ni wakati mzuri wa kuonyesha kwa vitendo kwa kuruhusu nafasi za kujiajiri kwa wote wanaoweza.

Disclosure: Mwandishi ni mtaalamu wa mifumo ya kielektroniki na ana uzoefu wa kuongoza, kujenga na kusimamia mifumo hiyo kitaifa na kimataifa.
 
Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
12,140
2,000
Electronic ticket kwa mabasi ya Tanzania tunahitaji smart minds kuwekezwa hapo. Kwa serikali hii na kiki hatuta fika..

Kuna mtu anafungulia mbuzi, akisha wafungulia basi anarudi kulala, hana habari watakula djamba la mtu , wataibiwa, anasubirikesho asubuhi awafungulie tena.

Tulisha washauri kwamba ni bora watumie mashine zile za TRA na kwa mabasi ya mikoani iqe ni moja ya masharti ya kukabidhizwa leseni ya route.

Pia Latra waunganishwe na TRA kwa maan kwamba kabla LTRA hajatia leseni ahakikishe kodi imelipwa.

Pia magari yalipiwe kodi kwa gari moja moja, na sio kuchanganywa na makadirio ya biashara nyingine, serikali inakosa kodi nyingi tuu.

Wana JF,

Baada ya Serikali kutoa tamko la kukata ticket kieletroniki sasa wafanyabiashara wa Mabus kwa kushirikiana na brokers au madalalie wa ticket. Kibaya zaidi hupewi ticket baada ya kutoa fedha.

Leo nimejifunza kitu gari no. T 195DAV KVC Safari karibu abaria wote hawana ticket. Jambo ambalo ni hatari, akitokea la kutokea hatujui hatima yetu.

Leo gari la Harambee limeharibika njiani baada ya kumaliza mto wami abiria tukafaulishwa. Baadaye tuko njiani tukadaiwa upya, tumebishana hadi mwisho sisi tukawa na hatia ya kutopewa ticket ikala kwetu.

Nimejaribu kushitaki kwa traffic mombo bila mafanikio traffic akaniambia niende nishitaki mwisho wa gari kwani safari bado ndefu. Mtindo Huu tutaumia wengi, bora traffic wawe wanaingia ndani kukagua ticket vinginevyo serikali itapoteza mapato na akitokea ajari kunakupoteza insurance.

Kampuni za kuanzia njia ya Boko - Bunju hawakati electronic.
 
mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,824
2,000
Kwenye hili la Ticketing, nadhani serikali inapaswa ifikirie upya. Kwanza LATRA wangebakia kuwa regulators na kuwaacha wafanyabiashara wa makampuni ya IT yafanye biashara. LATRA waweke standards ambazo vendors watahakikisha wanazifuata ili kupewa leseni.

Kuna changamoto kadhaa hapo
1. Wenye mabasi kutengeneza mifumo yao wenyewe. Hili wasiruhusu kwa sababu ya conflict of interest.

2. Vendors wanaweza kudanganya. Kuzuia udanganyifu, LATRA wata setup system ya monitoring ambayo kila vendor atajiunga kama sehemu ya masharti ya leseni yake

3. Askari atakuwa na app kwenye simu iliyounganishwa na monitoring server kwa ajili ya ukaguzi na kusaidia kuzuia fraud ya vendor.

Faida za open market kuliko serikali au kampuni chache kuhodhi kazi ya kufanya tiketi ni

1. Kuongeza ajira. Kampuni zitazaliwa na zingine kukua na hivyo kuongeza wigo wa serikali kukusanya kodi. Latra pia watapata fedha kwenye utoaji wa leseni.

2. Kwa sababu ya mashindano kati ya vendors, bei ya huduma kwa wenye mabasi itashuka, na wamiliki wa mabasi watapata huduma bora toka kwa vendors. Kwa hiyo soko litakuwa na gharama fair na huduma bora. Vendor ambaye atatoa huduma mbovu au bei ghali, atakosa wateja na atajiondoa kwenye soko mwenyewe.

3. Baada ya muda soko la Bongo litakuwa saturated na haya makampuni yatalazimika kutafuta soko la nje. Hapa tena serikali itavuna kodi ya ziada kwa sababu mwisho wa siku fedha ya huko itarudi huku nyumbani kwenye kampuni mama.

Kwa hiyo ushauri wangu kwa serikali kupitia Wizara na LATRA ni kuwa waliache soko liwe huru bila limitation, wao waweke vigezo na masharti ili wataalamu wa Software Development wa Tanzania wachuane kutengeneza mifumo bora, watengeneze ajira na kulipa kodi.

Serikali kupitia viongozi wetu imekuwa inatutia moyo vijana tujiajiri. Ni wakati mzuri wa kuonyesha kwa vitendo kwa kuruhusu nafasi za kujiajiri kwa wote wanaoweza.

Disclosure: Mwandishi ni mtaalamu wa mifumo ya kielektroniki na ana uzoefu wa kuongoza, kujenga na kusimamia mifumo hiyo kitaifa na kimataifa.
Njia yako Ni sahihi mno lakini Hawa Ni NADRA Sana kuchukua mooni ya watu
 
ninja666

Member
Mar 14, 2017
70
125
hadi sasa kuna mkanganyiko wa hii huduma ya E ticket maana mmiliki lazima ununue p.o.s yaan point of sale halafu uiweke float ndio uanze kukata tiket sasa mkanganyiko upo wapi ni hivi unaweza weka float halafu signal ipo chin yaan mtandao upo chin la pili unaweza weka float isionekane na ukifatilia pia haionekani sasa wenye mabus wanshindwa waanzie wapi la tatu garama imeongezeka maana kama una mabus ya route nne tofauti kila bus lazima liwe na p.o.s na kila moja inauzwa zaid ya laki4 had 5 na float isiyopungua laki 8 hadi milion ikumbukwe hii ni biashara nani huduma pia lamwisho ambalo ndio baya zaid ni mmiliki hawezi uza ticket under charge yaana kwa mfano dar mwanza nauli ni elfu 55 mtu akiwa na elfu 50 mashine haikubali sasa ndio wewe ndugu abiria una safiri una majanga yako upo na familia unasidiwaje ,ni changamoto kwa kweli
 
wakolosai

Member
Aug 22, 2017
98
250

Huu utetezi umekaa kipigaji pigaji
 
Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
2,477
2,000
Kwani kampuni za simu haziwezi pewa uwakala, m pesa, tigo pesa nk viosk vyao vitumike kukata hizo tiketi za ki electrinucs kwa sababu tayari wanauzoefu wa e bussiness.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom