Serikali bado inaendelea na ukamilishaji wa zoezi la uhakiki wa watumishi

mliverpool

JF-Expert Member
Jan 6, 2015
1,506
2,831
Hivi Karibuni Serikali ilitoa taarifa kwa umma kuwa Ajira zimesitishwa kwa muda ili kupisha zoezi linaloendelea la uhakiki wa watumishi Serikalini. Aidha Sekretarieti ya Ajira pia ilitoa taarifa ya kuahirishwa kwa usaili wa nafasi za kazi kwa tangazo lililotolewa tarehe 1 Juni, 2016 hadi hapo mtakapoarifiwa tena.

Pamoja na taarifa ambayo Sekretarieti ya Ajira iliiyoitoa, bado imekuwa ikipokea maswali kutoka kwa wadau mbalimbali hususan waombaji kazi wakiulizia ni lini mchakato wa ajira utarejea.

Kwa taarifa hii tunawataarifu kwa mara nyingine kuwa Serikali bado inaendelea na ukamilishaji wa zoezi la uhakiki wa watumishi na mara baada ya zoezi hilo kukamilika taarifa itatolewa na Mamlaka husika, hivyo mnaombwa kuendelea kuvuta subira.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, 9 Agosti, 2016.
 
Lini mwisho wa mchakato wa kuwabaini watumishi hewa?! In fact sioni mwisho maana kila leo watu hufa, huhama ama kuacha kazi! Wabadhilifu na wajanja wajanja wanazaliwa kila siku.

Serikali iliwapa jukumu wakuu wa Wilaya na Mikoa kubaini watumishi hewa na kwa deadline! No feedback. Bado tunakuja na kauli taarifa... Tuache ubabaishaji... Ajira zimesitishwa, madaraja hayapandishwi, Dodoma hamuendi mmebaki kututia vumbi tu humu..
 
Sasa hapa point iko wapi au umewajibu waliokuwa waki uliza? OK poa message sent and delivered. Kuna watu wamehamishwa yangu mwezi wa NNE hawajalipwa wsmepata shida tafikiri sio watumishi. Mbona hamjasema waliohamishwa vituo warudi wasubiri uhakiki ndio wahame? OK Sawa tunasubiri mmalize
 
Mwenye kale ka wimbo ka marehemu Komba nakaomba nimekamic, nataka nikacheze kimanjonjo.
 
Lakini wakumbuke kuwa kuna kundi kubwa sana la wafanyakazi halina mishahara na liko kazini linaumizwa sana na hili zoezi lisiloisha
 
Namkubali Magufuli ila katika hili suala la kusitisha ajira simuungi mkono hata kidogo
 
Hivi Karibuni Serikali ilitoa taarifa kwa umma kuwa Ajira zimesitishwa kwa muda ili kupisha zoezi linaloendelea la uhakiki wa watumishi Serikalini. Aidha Sekretarieti ya Ajira pia ilitoa taarifa ya kuahirishwa kwa usaili wa nafasi za kazi kwa tangazo lililotolewa tarehe 1 Juni, 2016 hadi hapo mtakapoarifiwa tena.

Pamoja na taarifa ambayo Sekretarieti ya Ajira iliiyoitoa, bado imekuwa ikipokea maswali kutoka kwa wadau mbalimbali hususan waombaji kazi wakiulizia ni lini mchakato wa ajira utarejea.

Kwa taarifa hii tunawataarifu kwa mara nyingine kuwa Serikali bado inaendelea na ukamilishaji wa zoezi la uhakiki wa watumishi na mara baada ya zoezi hilo kukamilika taarifa itatolewa na Mamlaka husika, hivyo mnaombwa kuendelea kuvuta subira.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, 9 Agosti, 2016.

Kwa hiyo hawa mabwana wanataka kuthibitsha kwamba ikulu imekurupuka kusema kwamba hili zoezi "litachukua kama miezi miwili au mmoja na nusu vile".Wanafaa kutumbuliwa kwa kwenda kinyume na kauli ya Rais..wanamuharibia
 
Kama ni hamna si bora waseme tu ukweli?? Kwani awamu hii tumejipanga kuupokea ukweli hata kama unauma ili kuleta mabadiliko ya kweli

Sasa wanavoanza maigizo na sisi tutawachukulia ki maigizo igizo

Taarifa kama hii sio ya kuweka kwenye webu wanapaswa watumie vyombo stahiki
 
"Ajira ni Bomu linalosubiri kulipuka" Lowassa ,

Magufuli kaamua kuja kulitegua kabisa,,mshaurini jamani ,hatoweza kuongoza kwa AMANI kama suala LA ajira na mikopo itaendelea kuwa ya kusuasua,,,,
 
Yaani serikali ina wafanyakazi ambao imewapa kazi kisha ikawaambia kaeni nyumbani.
Hawa hawajahakikiwa.
Hawa watalipwa mishahara bila kufanya kazi na malimbikizo yote wanayyodai.
Hawa hawajawezeshwa kuishi kwahiyo wana taabika huku wana kazi.

Hili la kusitisha ajira bila ukomo ( si miezi miwili sasa);
Linasubiri Mh Rais aseme maana siku hizi hata masuala madogo mawaziri wanaogopa kuongea.
Hawajaleta takwimu yoyote toka ile namba 12000+ ya wafanyakazi hewa. Huenda hakukuwa na ufanisi wakalazimika kuhamia kwenye vyeti fake.

Nchi inaenda wapi hii?
 
Sasa hapa point iko wapi au umewajibu waliokuwa waki uliza? OK poa message sent and delivered. Kuna watu wamehamishwa yangu mwezi wa NNE hawajalipwa wsmepata shida tafikiri sio watumishi. Mbona hamjasema waliohamishwa vituo warudi wasubiri uhakiki ndio wahame? OK Sawa tunasubiri mmalize
Mkuu Mimi siyo mfanyakazi wa utumishi wala siyo niliandaa hilo tangazo,kutokna na njaa yangu na kukosa LA kufanya mchana huu,nimeamua niingie kwenye hiyo mitandao yao nikakutana na huo ujumbe,nikaamua niwaletee wadau wenzangu,,usinihukumu mm kiongozi sote tunaendelea kuzisoma hizo namba..
 
Back
Top Bottom