Serikali, Baada ya kuwafukuza UDOM vijana wetu, haya ndiyo wanayokumbana nayo Vyuoni

MLALUKO JR

JF-Expert Member
May 3, 2015
962
305
Habarini wanaJF.

Mimi leo imekuwa siku yangu nzito na ngumu imeyonifanya niwaze na kuwaza bila kupata majibu .

Wote tunakumbuka tukio la vijana waliokuwa wanasoma special program ya sayansi ktk chuo cha Udom,Dodoma kufukuzwa ktk hali isiyo ya kibiinadamu na kuwaacha na taharuki na sintofahamu.!

Mbaya zaidi ni ilipofikia kuitwa majina mabaya na viongozi wakubwa wa serikali kama vile "vilaza" na "Vihiyo" kuonesha zarau,kejeri na Istazai kwa vijana wale.

Tunashukuru Mungu lilitoka tamko la baadhi yao kurudi Udom na wengine kupangiwa vyuo mbalimbali nchini.Hili sina tatizo nalo!!!!!!!

Leo nimepigiwa simu na mdogo wangu anayesoma chuo mbeya(naye alitokea Udom) akiniambia kuwa serikali iliamrisha vijana hao kufanya kazi ya kusahihisha mitihani ya darasa la nne kwa kipindi cha mwezi mzima na kuahidiwa kulipwa 50000/= huku wakilishwa chakula cha kawaida.Wakati kazi ingegharimu pesa nyingi kma wangewatumia walimu waajiriwa takribani 700000/= kwa mwezi.

Kikubwa na cha kushangaza vijana wale wameambiwa kufikia kesho trh 24 dec wawe wamemaliza kazi na isipokamilika wataifanya trh 25 dec siku ya X-mass.Nakuambiwa kuwa soon wanapomaliza kukabidhi waondoke chuoni kwa wiki moja bila kufikiria umbali Wa mahali watokapo wanachuo hao mfano:Kigoma n.k na hakuna atayeruhusiwa kubakia chuoni hata mmoja.

Kwa uchungu alikika akisema "Kaka usione watu wanakuwa magaidi,watu kuwa magaidi ni kitu kidogo hasa mtu anapodhurumiwa au kunyanyaswa".
Nafikiri serikali inajua inachokifanya si sahihi na unyanyasaji pia,watoto na wadogo zetu wanalia!


Je,Serikali hamuwaoni!?????

Nawaombeni radhi kwa maneno,japo si Mimi ni hasira zimenifanya niandike Mengi!!

[Hash]Tunaisoma[Hash]
 
kwahiyo unaamua lipi mkuu. naona malalamiko mengi sana. hebu weka picha ya simu yako unayotumia tuone kama kweli hali ni mbaya.. wanaume wa dar bwana
 
Hizi tends kuna watu wanazililia sana mtaani. Mkitoka chuo mtazikumbuka hizi, nyie endeleeni kulialia yaani mnapata fursa mnaanza kulia. Hata wakifika JKT watalia na kuwapigia simu mama zao kwamba wanateswa!......muda tu ndio jibu la kweli
 
Hatunywi sumu, hatujinyongi,
Ccm mbele kwa mbele*2

Tumeipenda wenyewe
Chaguo letu milele
Na wavimbe wapasuke

Nami mdogo wangu form six EGM badala ya kwenda dip, amechaguliwa cert. Imebidi aende tu, atasolve baadae hakuna namna
 
Huu uzi nimeusoma mara 3 kabla ya kutoa comment. Nimesoma mara ya kwanza nikawa kama vile sijaelewa kitu. Nimesoma mara ya pili nikawa kama vile sihamini ninachokisoma. Nimeusoma mara ya tatu nikaishiwa kupata hasira na viganja kuanza kutetemeka. Kwa sababu nimejaa na jaziba ngoja kwanza nitulia nitarudi kutoa dukuduku langu baadaye.
 
Hicho chuo cha Mbeya hakina jina?
Je endapo serikali itaamua kufuatilia ukweli wa jambo husika iende chuo kipi maana Mbeya ni kubwa
Tukuyu teaching college hata Mpwapwa nao walifungashiwa vilago Jana!
 
Back
Top Bottom