Serikali awamu ya tano heshimuni haki za raia na zaidi ya yote muogopeni Mungu

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,823
35,829
Kutendeana haki ni jambo la kiungwana tu ambalo ni wajibu wa kila mtu katika jamii iliyostaarabika. Hii ni bila kujali nafasi wala wadhifa wa mtu katika jamii husika.

Yapo mengi tunayoyashudia katika awamu hii ambayo ni tofauti mno ukilinganisha na awamu zote zilizopita hasa katika masuala ya kufuatwa sheria na kuheshimu haki za binadamu. Pasipo na kupepesa maneno kuthaminiwa kwa haki za msingi za binadamu katika awamu hii imekuwa kizungu mkuti kweli kweli.

Polisi wamegeuka miungu watu wakithubutu bila aibu kujiita wao ni mamba. Nani asiyemjua mamba wala tabia zake? Ni wapi mamba aliwahi pewa jukumu lolote kuhakiki wala kusimamia lolote?

Awamu hii udhalimu wa polisi umekuwa mkubwa mno. Usumbufu wa polisi vituoni, barabarani nk vimeshamiri vilivyo na hali kwa ujumla ni mbaya mno!

Mombasa trader Hamisi Madilo's arrest in Tanzania 'mistaken identity'

Inawachukua polisi Tanzania hadi siku 11 raia wa nchi nyingine hatimaye kujua haki zake zinakiukwa? Mistaken identity? Hii imefikia huku baada ya nguvu kubwa tokea Kenya kuhusiana na raia wao huyu. Poor we, poor us. Ama kweli alikuwa mkononi mwa mamba wala watu.

Serikali msijisahau dhana halisi ya serikali ni kufanya matakwa ya raia ambao ndiyo wanaowaweka madarakani. Kama si kutekeleza matakwa ya raia nyiye awamu hii ridhaa yenu mnaipata wapi?

Nani anaye kutumeni nyiye kukandamiza na kunyanyasa watu?

Ni wazi kuwa ni baina ya mambo haya mnayokomaliwa na mataifa ya Ulaya na Marekani hadi kufikia kwenye kunyimwa misaada. Ama kweli sikio la kufa halisikii dawa, wenyewe kwa wenyewe hata hamjihoji?

Mnanufaika na nini kwa udhalimu wenu wa aina hii? Mnanufaika na nini na huu usanii wenu wa kuwashikilia watu rumande kwa kucheza cheza na mnachoita ufundi wa maneno? Mnadhani hatuwaoni? Mnadhani mwenyezi Mungu hawaoni?

Ni maneno yenye mantiki sana aliyosema bwana yule kuwa waliovunjiwa nyumba watunze nyaraka. Hata kama ni baada ya miaka 200 itajakuja serikali ya watu ya watu wenye utu itakayo kuja kulipa fidia.

Malipo ni hapa hapa duniani.
 
Back
Top Bottom