Serikali awamu ya Sita ni butu? Makampuni ya simu yameipuuza

Retina

JF-Expert Member
Mar 6, 2015
1,038
1,154
Natafakari sana haya makampuni ya simu kuigomea serikali kupunguza bei ya vifurushi. Katika awamu ya tano tulijionea, serikali ilikuwa ikiamua jambo lake, watendaji waliwajibika kwa wakat na kwa speed mujarabu.

Tunajionea kwa macho na kwa vitendo awamu hii ya Sita ipo slow sana inaenda sawia na sauti ya upole na ya taratibu ya rais mama yetu Samia.

Takiriban miezi miwili sasa Wananchi tunapigwa punch za uso na makampuni ya simu kwenye bei ya vifurushi kuwa juu, hatimaye Wwnanchi wameanza kuizoea hali hii.

Huko mbele Kuna hatari tutakuja kujionea kila taasis za binafs zitoazo huduma kujipandishia bei watakavyo, mfano shule binafsi zitapandisha ada na kuongeza michango na kwani serikali ni butu, hii ni mfano Michache. Mapovu ruksa.
 
Serikali inajifunza kila CHANGAMOTO ITOKEAYO.

Serikali yetu haifanyi biashara bali INAWEKA mazingira bora ya uwekezaji na kuangalia maslahi ya RAIA WAKE.

Awamu hii ya 6 ni zao la Awamu iliyopita na INATAMBUA VYEMA CHANGAMOTO zilizoikumba AWAMU YA 5 katika masuala ya "kiuchumi".

Tuna imani na awamu ya 6 kuwa iko IMARA KUBALANCE VYEMA maslahi ya WAWEKEZAJI WAFANYABIASHARA NA YALE YA RAIA "walaji" wa huduma!

#KaziIendelee
#NchiKwanza
 
Mwamba ndo aliwapa nafasi makampuni ya simu kutukamua bei kubwa ya bando!.

Airtel walitii agizo la rais, labda kwa sababu serikali ina hisa mle!
Hawajutii chochote mkuu, wamefanya usanii hapa na pale - lakini either way wame-peg major/popular bundles predominantly kwenye 500Mb, wanacho ongeza ni muda wa maongezi wakati wateja wanacho gomba ni bundle za data sio voice.

TCRA wakumbuke kwamba wananchi karibu wote wanajifunza mengi kupitia kwenye mitandao na sio kwenye maongezi na simu - hilo wala Serikali yetu ilioni wana wachia makampuni ya simu yafanye yapendalo bila wasi wasi wowote - we fikiria kampuni hizi zilivyo za ajabu kidogo - mfano Airtel bundle ya UNI wameifanyia usanii na mamlaka husika wako kimya kabisa, mamlaka hii hii iliahidi wananchi pamoja na Rais kwamba wata hakikisha charges zitarudishwa kama zilivyo kuwa tangu mwanzo - sasa huu mwezi wa ngapi tangu TCRA itoe ahadi?
 
Mimi natumia vida, TTCl na halotel, Vifurushi vilipungua muda zamani Sana. Wewe uko mkoangani?
Nafikiri baadhi ya mitandandao wanafanya price discrimination, kwangu mimi offer ziko vizuri 1000tsh napata 1gb, dk 100, na sms 1000, laini zangu zote tigo na voda napata hii offer.
Ila kuna mtu kwa buku hapati kifurushi hicho.
 
Moja kati ya udhaifu mkubwa sana wa Watanzania ni upotezaji wa kumbukumbu hata kwa jambo ambalo halina hata miezi 6; kwani ile issue ya kuongeza bei za vifushi vya internet ilitamkwa lini na nani? Sio waziri muhusika tena enzi za mwendazake?

Tusiisingizie awamu ya sita, tusiyasingizie makampuni ya simu. Lawama au pongezi ziende kwa muhisika.
 
Serikali ndio iliagiza makampuni ya simu yapandishe bei za data, serikali hiyo hiyo inaagiza makampuni ya simu kushusha data.

Je, kama Kuna Sheria iliagiza hivyo hiyo Sheria imefutwa.

Toka Mama Samia ameingia hakuna Sheria hata moja aliyofuta halafu mnategemea mabadiliko chanya kwa muda mfupi.
 
Back
Top Bottom