Serikali angalieni suala la Tanesco, maji , miamala na vifurushi vya simu

Hata Kenyan Power Limited (KPL) nao walikuwa wasumbufu kama TENESCO. Wakenya wengi walijiongeza kutumia masolar panels, KPL walipoona wateja wengi wanahamia kwenye masolar ndo wakaanza kuboresha huduma zao mpaka Leo. Ila shida ya watanzania wengi sijui wanakwama wapi kutumia njia mbadala mbona TENESCO wangenyooka wenyewe.
serikali ikiona hivyo mwaka unaofuata hivyo vifaa vinaongezewa kodi, ukipiga hesabu unaona ni bora kusubiri tanesco
 
Mimi naona wanafanya hivo kutengeneza mazingira ya rushwa. Ukiingia kwenye tovuti yao nako vituko tu, yaani wanaweka nambari ya mawasiliano isiofanya kazi. Serekali inapoteza kodi nyingi kwenye huduma ya umeme hata sioni sababu ya kuzuia ushindani na makampuni mengine
Hapa nafikiri serikali ingebadilisha Mfumo wa uongozi ,kwa sababu shirika limeshaanza kuonesha Dalili mbaya na wasipokuwa Makini litarudi nyumba tena litakuwa Bovu sana
 
Tafadhali tujulishe una changamoto gani haswa na TANESCO, eneo gani? Namna ya simu tuifanyie kazi mara moja.
Tanesco Apps ilikuwa ya awamu ya 5 ?
Mbona alivyoondoka tu mkaipiga chini? Na sasa sisi wateja hatuwezi hata ku access ?
 
Back
Top Bottom