Serikali amrisheni watu wapunguze kuzaliana!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Watu wanazaliana hovyo na ndiyo maana kuna shida ya kila kitu, sasa ona hata mnahangaika kupiga marufuku watu wasisafiri wakati hapa nyumbani hakuna kitu cha kuwaweka, hivyo ili kuokoa haya matatizo huko mbele ni lazima tuache kuzaliana bila ya mpango, kama hauna uwezo Watoto 2 mwisho, halafu unapigwa sindano, kama hauwezi kujizuia, ...

Waafrika wakiparamia Meli kwenda Ulaya kutafuta Maisha!
600x338

Majeneza ya Waafrika waliokufa wakijaribu kuingia Ulaya kutafuta maisha huko Lampedusa!
mediterranean-migrants.jpg
 
SIjui pengine ila ...
Tanzania kuna fursa nyingi sana .. tatizo watanzania hawatumii vyema akili walizopewa na Mungu ..
Pia serikali za nchi za Afrika .. viongozi wake ndio vinara wa kudidimiza maendeleo ya Afrika.
 
Kuilamu Serikali ya Afrika ni kukimbia na kukwepa tatizo, kwani Serikali siyo chombo bali inaongozwa Watu ambao ni mimi na wewe, hivyo ni sisi na siyo Serikali!
 
Kuilamu Serikali ya Afrika ni kukimbia na kukwepa tatizo, kwani Serikali siyo chombo bali inaongozwa Watu ambao ni mimi na wewe, hivyo ni sisi na siyo Serikali!
Sijasema serikali .. soma vizuri .. nimesema viongozi ambao ni miongoni mwetu ..
Mfano miaka nenda rudi serikali imekuwa ikiruhusu mchanga unasafirishwa toka migodini kwenda nje ... mimi kama mimi mwanachi wa kawaida nahusikaje .. ? hapo lazima niwalaumu wenye dhamana.
 
Serikali ipi Mkuu?
Akizindua daraja la Kigamboni, Rais aliagiza watu wafyatue watoto kwa raha zao!
 
Hicho kitu nakiwaziaga sana....watu wanazaa sana alafu hawana uwezo, omba omba wanazidi kuongezeka mitaani....yaani kero kwakweli
Ingekua bora mkaua familia zenu nakujimaliza wenyewe itakua mfano bora zaid ktk kupambana na ongezeko la watu au mnasemaje? pamoja na mleta uzi
 
Kwa hili nakubaliana na wewe. Miaka kama minne hivi iliyopita nilileta mada humu kuhusu umuhimu wa family planning na wazazi kuwa responsible na "matendo" yao. Watu wanaingiliana hovyo mwanaume akijua kabisa "hana mpango".

Itungwe sheria kali kuwawajibisha wazazi. Mtu anapozaa ajue anawajibika pia kulea hususan wanaume. Jamii ielimishwe umuhimu wa family planning. Zile enzi za kila mtoto na riziki yake zimepita; au kwamba ni sunna kuwa nao wengi zimepitwa na wakati. Kama unataka kushindana na familia ya kifalme ya Saudia ambayo mafuta yote ni yao jaribu.
 
watu walishaambiwa na mtukufu wafyetue tu sasa kwa vichwa vyetu vilivyo unatarajia nini?
 
Kuhusu kuzaa watoto wawili au mmoja anzia na ww bt mm hapana, izo sheria zenu za kizungu hazinifai, Muumba wa Dunia kusema tuje kuijaza dunia na si kujaza magari na madege
 
Huwezi kuuaga unaskini kwa kumchukia tajiri

Huwezi kupona uhanithi kwa kuwachukia marijali
 
Watu wanazaliana hovyo na ndiyo maana kuna shida ya kila kitu, sasa ona hata mnahangaika kupiga marufuku watu wasisafiri wakati hapa nyumbani hakuna kitu cha kuwaweka, hivyo ili kuokoa haya matatizo huko mbele ni lazima tuache kuzaliana bila ya mpango, kama hauna uwezo Watoto 2 mwisho, halafu unapigwa sindano, kama hauwezi kujizuia, ...

Waafrika wakiparamia Meli kwenda Ulaya kutafuta Maisha!
600x338

Majeneza ya Waafrika waliokufa wakijaribu kuingia Ulaya kutafuta maisha huko Lampedusa!
mediterranean-migrants.jpg

Una akili na mawazo ya kishetani,imagine wewe ungekuwa hujazaliwa ingekuwa je??

Kuna vitu mnaviongea kama vile mmerogwa. Mnatia hasira na mnaudhi.
 
Wewe jamaa leo umekuwaje tena? Unapingana na alichosema mkuu? Au account yako wamei hack?
 
Mimi nafikiri tatizo lipo juu ya idadi ya watu na malighafi zilizopo. Elimu ya Uzazi wa mpango ni muhimu.
 
Back
Top Bottom