Uchaguzi 2020 Serikali Amkeni: Taarifa lukuki za kutekwa wagombea wa chama kimoja tu cha siasa zisizo na uthibitisho ni hatari kwa usalama wa taifa

Hao wanaofanya hayo wanakiuka sheria za nchi!Ikifika mahali hakutakuwa na kurudi nyuma,mtu akiona haki haipatikani katika utaratibu wa kawaida kinachofuata ni violence!Tutafika tu huko na watawala watakumbuka walipojikwaa!
Haki huzaa amani,uonevu huzaa maafa!
Dah!! Watu mna mikwara humu JF
 
Ni swali tu nimeuliza baada ya kusoma tweet hii ya mmoja wa wagombea ndugu Boniface Jacob.
View attachment 1547469
Jeshi la polisi lilitakiwa limuite huyu Bon awasaidie polisi ushahidi wa hao wahalifu.
Kama hajaitwa mpaka sasa kuna shida kidogo katika kujivua na lawama hizi upande wa serikali na CCM.
 
Kama ilivyo tabia yoyote ile, lazima ianzie au ianzishwe mahala fulani na watu fulani au viumbe fulani, ilelewe kwa malengo fulani ichongewe mifereji na mirija ya kuendelea kwenda mbele na kuimarika.
Wakati fulani mwishoni mwa mwaka 2015 hadi 2017 kuliibuka tabia ya utekaji na mauaji nchini. Jamii iliingia kwenye tahayari kubwa sana. Serikali haikuonekana kustuka japo ilikua ikitoa kauli za hapa na pale just to mark their presence.
Baada ya hapo kukawa na ukimya fulani ambao randomly ulitawaliwa na unyanyasaji na matumizi mabaya ya madaraka kutoka kwa baadhi ya wakuu wa wilaya na mikoa. Hali iliendelea na baadaye ikafuatiwa na kuhamahama kwa kwa madiwani na pia baadhi ya wabunge, na matukio kadhaa ya utekaji wa wanasiasa.
Tukashuhudia bungeni jinsi wapinzani wanavyotendwa ili kudhibitiwa.

Wakati huu ulipofika uchukuaji wa form tumeshuhudia vikwazo vya waoinzani kupewa form, na kwa waliopewa form tumeshuhudia namna zoezi la urudishwaji wa form hizo ulivyoibua matukio ya kyvamiwa, kutekwa na kukamatwa kwa wapinzani n.k

Matukio yanaoendelea hivi sasa yanaleta tafsiri ya kushindwa kwa serikali kusimamia vyombo vyake au kama inavisimamia basi itakua inavisimamia kwa faida ya serikali na wananchi na nchi.
Tumemsikia Kamanda Sirro alipohojiwa na ITV, alipoulizwa kuhusiana na upelelezi juu ya shsmbulio la Tundu Lissu, jinsi alivyojibu iliinyeshwa mhanga Lissu ni kama wameshaamua kumgeuzia kesi pale aliposema "safari hii hatiki ni lazima wampate".

Kwa mtiririko huo wa matukio inaleta picha kwamba serikali na imetengeneza magenge ambayo ndiyo designer na watekelezaji wa matukio yote haya katika awamu hii.

Sura inayojengwa na matukio ya haya si nzuri kabisa. Inaudhi, inadharirisha, inajenga chuki, inakatisha tamaa pia inajenga kiburi na moyo wa utayari kwa lolote.
Serikali iliyopo madarakani ni halali kwa vigezo vyote, lakini kushindwa kuchukua hatua stahiki kulinda ustaarabu wetu ni kushindwa kuongoza nchi, na kuyaacha makundi haya yafanye watakayo ni hatari zaidi kwa nchi.

Tunaweza tukajiuliza sana yanayoendelea, watu wanatekwa, wakipatikana moja kwa moja wanajivua nafasi waliyochaguliwa na wananchi kwa madai kwamba wanaunga mkono juhudi.
Wakati wa uchukuaji form umefika, lakini vikwazo vinaanzia kwa wakurugenzi, ukivivuka hivyo mtaani unasubiriwa kutekwa, ukisalimika kutekwa Polisi wanakuja kukukamata, ikishindikana kuiamatwa kitakachofuata ni kiwatangaza kutokidhi vigezo vya kugombea.
Huu ni mkakati unaoonekana kuwa una rasimishwa, lakini ni wa kijinga na kipunguani sana.
Serikali inabidi ijitathmini sana katika swala hili.

Nawasilisha
 
Mgombea wa Chadema Kongwa kavamiwa na watu wakamnyanganya begi ambalo lilikuwa na copy ya fomu. Hivyo original form ilikuwa salama. Kesho yake mgombea wa CDM akaipeleka kwa msimamizi ikapokelewa.

Ona kichekesho:
Job akaweka pingamizi kuwa FOMU ILIIBIWA SASA HII ULIYORUDISHA UMEIPATA WAPI?

Maana yake nini:
Job anajua fika kuwa fomu imechukuliwa ... hivyo aliwatuma yeye kufanya aborted kitendo hicho cha uvamizi!
 
Mgombea wa hadema Kongwa kavamiwa na watu wakamnyanganya begi ambalo lilikuwa na copy ya fomu. Hivyo original form ilikuwa salama. Kesho yake mgombea wa CDM akaipeleka kwa msimamizi ikapokelewa.

Ona kichekesho:
Job akaweka pingamizi kuwa FOMU ILIIBIWA SASA HII ULIYORUDISHA UMEIPATA WAPI?

Maana yake nini:
Job anajua fika kuwa fomu imechukuliwa ... hivyo aliwatuma yeye kufanya aborted kitendo hicho cha uvamizi!
Hapo anamuwinda amtandike bakora ya kichwa ili asilete kiwingu. Ccm ya jiwe ya kishamba sana
 
SI JOB KAWEKA PINGAMIZI KUWA FOMU IMEIBIWA HII KAIPATA WAPI? MKURUGENZI KAKUBALI , KAMUENGUA S........ TYPE!
Haa! Kumbe ndio hivyo? Hivi hayo mapingamizi yanafanywaje? Yaani upumbavu wa maamuzi ya DED unaweza kupita bila kuhojiwa?
 
Kwa maelezo hayo Ndugai ndio aliziteka hizo fomu copy, hivi hawezi kuchukuliwa hatua za kisheria kwa ushahidi wa maandishi yake?
 
Mgombea wa Chadema Kongwa kavamiwa na watu wakamnyanganya begi ambalo lilikuwa na copy ya fomu. Hivyo original form ilikuwa salama. Kesho yake mgombea wa CDM akaipeleka kwa msimamizi ikapokelewa.

Ona kichekesho:
Job akaweka pingamizi kuwa FOMU ILIIBIWA SASA HII ULIYORUDISHA UMEIPATA WAPI?

Maana yake nini:
Job anajua fika kuwa fomu imechukuliwa ... hivyo aliwatuma yeye kufanya aborted kitendo hicho cha uvamizi!
Ha haaa
Hii kali mkuu.
Kama kweli kuna mengi sana ya kujiuliza hapo.
 
Kuna wimbi limezuka yakwamba wagombea wa chadema wanatekwa na kunyang'anywa form za kugombea nafasi za ubunge na udiwani wanapoelekea kuzikabidhi kwa tume ya uchaguzi.

Kwanini ni chadema pekee na si vyama vingine?,jibu ni kwamba chadema inatafuta attention kwa nguvu, ndani ya nchi na nje katika jumuiya ya kimataifa kujionyesha wanaushawishi wakati si kweli hata kidogo.

Hili la kujiteka lipo ndani ya Chadema wenyewe.

Chadema hakina fedha za uchaguzi kuweka wagombea na wasimamizi au mawakala nchi nzima ,hili liko wazi, wanachofanya ni kutaka kuvuruga uchaguzi huu tu.

Hawakufanya vetting ya kutosha kwa wateule wa nafasi za udiwani ,ubunge na hata urais,wamekurupuka na hilo liko wazi kabisa.

Utachukuaje wagombea bila mchakato makini?, haya ndio matokeo yake . Wagombea wao Wanatelekeza nafasi zao kwa ukata ,chama hakina fedha ya uchaguzi , wakijua hawatashinda.

Wakitumia njia ya kujitoa wataonekana wasaliti kwa wafuasi wao

Njia wanayoitumia kwa sasa ni kuingia mitini kwa kisingizio cha kujiteka na huu ni upumbavu wa hali ya juu sana.

Naviomba vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na TCRS kubaini mwenendo huu ambao unaharibu taswira ya nchi yetu kwa makusudi kabisa.

Hili likiendelea kuachwa madhara yake ni makubwa huko mbeleni.
Inamana hao wagombea wa ACT waliotekwa wao sio wapinzani sio?
 
Bahati mbaya sana mada yangu imeungwa huku ...IGP ni mtoa miongozo na maamuzi hivyo kauli yake ni muhimu
Basically mada yako ilimlenga zaidi IGP, naona kama wameipunguza uzito kuunga hapa ambapo nazungumzia utekaji wa wagombea na uporaji fomu uliokuwa unadaiwa kutokea lakini hatupati uthibitisho zaidi wa vyombo husika.
Au mtu anaonekana anarudisha fomu ofisi za NEC wakati ilisemekana fomu zake ziliiibiwa. Tumeona hili kule Bumbuli na Dodoma Kama sikosei Kongwa.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom