Uchaguzi 2020 Serikali Amkeni: Taarifa lukuki za kutekwa wagombea wa chama kimoja tu cha siasa zisizo na uthibitisho ni hatari kwa usalama wa taifa

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
11,284
17,713
Kuna taarifa mpya ya kutekwa mgombea wa CHADEMA kwa ngazi ya UDIWANI na UBUNGE kila baada ya dakika chache ndani ya siku 5 za mwisho kuelekea siku ya leo tarehe 25/08/2020 ya kupitishwa majina ya wagombea na NEC.

Nyingi ya hizi taarifa hazina uthibitisho kiasi kwamba zinaleta hofu kuna watu wamepanga kuichafua nchi kwa makusudi na kutaka kupata uhalali wa kuja kufanya vurugu na kuomba jumuiya za kimataifa kuingilia mambo ya ndani ya Tanzania.

Sasa ifike wakati Tanzania iwe mbele kuliko maslahi binafsi. Kuna uwezekano mkubwa huu ni ushauri hatari uliopendekezwa na watu wa ndani au wa nje ya nchi ambao wana maslahi binafsi. Ninacho kiona ni hatari ya vita kama nchi zingine zilizo ingia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe au kuvamiwa na majeshi ya kigeni kwa mlango wa kukomesha vurugu, kulinda amani na kusimamia demokrasia.

Vita hivi havitachagua familia za wana CCM au wana CHADEMA, ACT, NCCR-Mageuzi, ADC, CHAUMA au CUF pekee.
Mnaofanya mambo haya na kushawishi vijana wasiojielewa kutumika katika mipango hovu, haya mambo yatatudhuru wote na biashara zetu wote.
Msitumike na nchi jirani au watu wa mabara mengine kama hamjitambui.

Napata shida kuishauri serikali hasa Idara ya Usalama wa Taifa, JWTZ, na jeshi la polisi kuanza kuchukua hatua ngumu zaidi kwa waeneza taarifa hizi. Lakini sina budi niwashauri ikiwalazimu fanyeni hivyo, kama media zikishindwa kuwadai uthibitisho zaidi basi ziwekeeni speed governor maana hakuna namna, hapo baadaye watanzania wema watawashukuru kwa kuwaokoa na mkono wa mtoa roho. Wanasema 'the end justifies the means'.

Jukwaa letu pendwa JF nawashauri mjisafishe mikono yenu na damu zinazokaribia kumwagika sababu ya habari hizi za propaganda, jifuteni mikono yenu machozi ya watoto yatima watakao telekezwa na familia zao wakati wa vurugu, picha maarufu ya mtoto wa Sudan aliyekaribia kuliwa na tai baada ya kukosa uangalizi wakati wa vita inatembea kwenye akili yangu na kunitia simanzi sana nikiwaza jambo kama lile linaweza kuwatokea maelfu ya watoto wa kitanzania.

Ile picha ni mbaya kiasi kwamba mpigaji alikufa kwa msongo wa mawazo na kujutia kuchukua picha kama ile ingawa ilimpa utajiri, fikiria wewe unaye leta taarifa za uzushi zikija kusababisha mambo kama yale unafikiri utaishi kwa amani ndani ya nafsi yako hata kama unayemtaka ataingia Ikulu na kukupa ulaji wa keki ya taifa?

Mambo yalianza kama hivi hivi propaganda kwenye media kule kwa wenzetu nchi za jirani maziwa makuu. Yale mafuvu yanatisha zaidi kama ukiona ulikuwa sehemu ya jambo ovu kama lile kutokea.

Yale magofu ya Libya na biashara ya utumwa inasikitisha zaidi kama wewe ni sehemu ya waliochangia kutokea jambo lile.

Mchana mwema.
 
Wangapi wanasoma mitandao? Haiwasaidii. Dawa ya wanaharakati ipo jikoni soon watalia.
 
Ni swali tu nimeuliza baada ya kusoma tweet hii ya mmoja wa wagombea ndugu Boniface Jacob.
Screenshot_20200825-121054.png
 
Kuna wimbi limezuka yakwamba wagombea wa chadema wanatekwa na kunyang'anywa form za kugombea nafasi za ubunge na udiwani wanapoelekea kuzikabidhi kwa tume ya uchaguzi.

Kwanini ni chadema pekee na si vyama vingine?,jibu ni kwamba chadema inatafuta attention kwa nguvu, ndani ya nchi na nje katika jumuiya ya kimataifa kujionyesha wanaushawishi wakati si kweli hata kidogo.

Hili la kujiteka lipo ndani ya Chadema wenyewe.

Chadema hakina fedha za uchaguzi kuweka wagombea na wasimamizi au mawakala nchi nzima ,hili liko wazi, wanachofanya ni kutaka kuvuruga uchaguzi huu tu.

Hawakufanya vetting ya kutosha kwa wateule wa nafasi za udiwani ,ubunge na hata urais,wamekurupuka na hilo liko wazi kabisa.

Utachukuaje wagombea bila mchakato makini?, haya ndio matokeo yake . Wagombea wao Wanatelekeza nafasi zao kwa ukata ,chama hakina fedha ya uchaguzi , wakijua hawatashinda.

Wakitumia njia ya kujitoa wataonekana wasaliti kwa wafuasi wao

Njia wanayoitumia kwa sasa ni kuingia mitini kwa kisingizio cha kujiteka na huu ni upumbavu wa hali ya juu sana.

Naviomba vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na TCRS kubaini mwenendo huu ambao unaharibu taswira ya nchi yetu kwa makusudi kabisa.

Hili likiendelea kuachwa madhara yake ni makubwa huko mbeleni.
 
Ni chini ya wiki moja tangu IGP Kamanda Sirro atoe angalizo na kukemea vitendo vya kihuni na vurugu wakati huu kuelekea uchaguzi mkuu.

Kakemea wagombea na misafara yao kufanyiwa fujo
Kakemea uharibifu wa mali kama kuchoma ofisi moto nk
Kakemea mengi na kuwaonya makamanda wa mikoa chukua hatua stahiki pale wanapoona viashiria vya fujo na uhuni mwingine

Tamko kemevu la IGP ni kama limetoa ruhusa rasmi ya kuteka, kujeruhi na kutesa wagombea wa upinzani(CHADEMA)..Na baadhi ya maeneo wagombea wakifunguliwa kesi na kuwekwa mahabusu kwa makosa yasiyojulikana rasmi.

Matukio ni kama sasa yanashika kasi..kwa uchache kabisa kuna matukio zaidi ya kumi tayari yaliyokwisha ripotiwa.

IGP yuko kimya ..hajitokezi kulaani wala kukemea
Je IGP naye katishwa? Je kuna sauti nyingine nyuma ya pazia yenye nguvu zaidi inayokwenda kinyume na tamko la IGP?
 
Inafikia mahali unajiuliza hizi drama mbona hazishtui WaTz??

Mood ni funika kombe mwanaharamu apite.
Tumepigika kimaisha tunataka sera.
CHAUMA walishasema #ubwabwa_juju
#twende_na_Rungwe


Everyday is Saturday........................... :cool:
 
Nawashangaa sana ninyi chama mnachojinasibu kila siku kua ni chama kikubwa kumbe hopeless kabisa.

Wagombea wengi wanavamia na wananyang'anywa fomu zao, wengine wameshikiliwa na polisi wakati huu na wengine wanasakwa. Polisi wanajua kua huu ni muda wa kurejesha fomu lakini wao wanaendelea kuwashikilia makusudi ili ratiba ya kurudisha forms upite.

Chama chenu kuna viongozi wako kimya hawatoi tamko lolote, mna viongozi makatibu wakuu, wenyeviti wapo, manaibu wa katibu mkuu wapo ninyi mmekaa kimya tu kwanini?
Ninyi uchaguzi ukiisha vinjeni chama chenu wananchi watafute chama kipya. Mnaonekana wasanii ninyi
 
Hao wanaofanya hayo wanakiuka sheria za nchi!Ikifika mahali hakutakuwa na kurudi nyuma,mtu akiona haki haipatikani katika utaratibu wa kawaida kinachofuata ni violence!Tutafika tu huko na watawala watakumbuka walipojikwaa!
Haki huzaa amani,uonevu huzaa maafa!
 
Ni vyema mamlaka zingetoa tamko juu ya huu uhuni. Jeshi la Polisi angalau lionekane linachukia mambo haya japo kwa matamko ya kukemea kama wanavyokemea kauli zinazoitwa za kichochezi

Tume ya Uchaguzi nayo itoe faida kwa waathirika wa matendo haya kwa kukubali kupokea fomu zao au hata kuwapa fomu zingine wote walioumizwa kwa kutekwa au kuporwa fomu hata kama muda umepita. Hii ingesaidia kuwanyima sababu ya kufanya hivyo(motive) watekaji na vibaka wapora fomu
 
Back
Top Bottom