Serikali acheni tuuze kahawa nje, maana ninyi mnanunua kwa bei ya chini kuliko Uganda na Burundi

chotera

JF-Expert Member
May 19, 2016
6,300
15,018
Wakuu.
nawasalimu sana sana.
Baada ya salamu naomba nieleze kua serikali haichangii chochote kwenye uzalishaji wa kahawa na hakuna msaada wenu.
Bado mnanunua kwa bei za chini yaani nipate hasara eti kisa nina uzalendo hiyo haijawahi kutokea hata siku moja.
Kahawa ina bei nzuri Rwanda , Uganda, Burundi Na kenya msitulazimishe tuwauzie ninyi kwa hasara mlivoua bei za mahindi na mbaazi muishie hapo hapo tuachieni kahawa tusomeshe watoto kwenye shule bora baada ya faida tutayopata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu.
nawasalimu sana sana.
Baada ya salamu naomba nieleze kua serikali haichangii chochote kwenye uzalishaji wa kahawa na hakuna msaada wenu.
Bado mnanunua kwa bei za chini yaani nipate hasara eti kisa nina uzalendo hiyo haijawahi kutokea hata siku moja.
Kahawa ina bei nzuri Rwanda , Uganda, Burundi Na kenya msitulazimishe tuwauzie ninyi kwa hasara mlivoua bei za mahindi na mbaazi muishie hapo hapo tuachieni kahawa tusomeshe watoto kwenye shule bora baada ya faida tutayopata.

Sent using Jamii Forums mobile app
msimamo kama huu ndio unaotakiwa.. KOMAAA KAZA BUTI KAKA!!
 
SAFI SNA.WAMEUA BEI YA MAHINDI NA MBAAZI.MAHNDI SAHV HAPA NILIPO NI 18 ALFU.wakulima tumekata mitaji.
 
Mkulima ana hali ngumu sana. Serikali iko kimya kusaidia wakulima, hakuna ruzuku, hakuna pembejeo kwa bei nafuu, serikali inahimiza hapa kazi tu, uchumi wa viwanda, vijana tujiajiri wenyewe,....watu wanajitutumua kwa nguvu zao binfsi. ILA linapokuja suala la soko la mazao no one cares, matamko tu ya kumdidimiza mkulima.
 
Serikali inakandamiza saaana wakulima,, nimelima kahawa hekari Tano..nmepata mavuno mengi sana mwaka huu.. Lakini nmeishia kuuza kwa ushirika tena kwa hasara kubwa mno. Bei wanayo nunulia Kwa kahawa ya maganda ni sh 300 kwa kilo. Yan nmeambulia MIL 2 kwa Hyo bei yao. Wanadai watalipa tena awamu ya pili.


Nimalizie Kwa kusema, adui wa mkulima nchini ni serikal ya CCM
 
hatutofika kwa mtindo huu huku ni kurudishana nyuma bila sababu hadi warundi watushinde bei , uganda hatujawahi kuwazidi bei miaka yote kwenye kahawa hapana serikali tuangalieni hapo kuna tatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katikati ya miaka ya tisini kama sijakosea, kulitokea sintofahamu baina ya wakulima wa kahawa, chama cha ushirika( KNCU) na serikali.

KNCU ni chama cha ushirika cha kahawa mkoa wa Kilimanjaro.
Kilichotokea, bei ya kahawa ilisemekana imeanguka katika soko la dunia na kupelekea kutokuwa na kukosa uwiano wa faida na gharama za pembejeo, mbegu, madawa anayotumia mkulima.

Enzi zile alikuwepo Augustine Lyatonga Mrema, nakumbuka aliwaambia wakulima wa kahawa kama wanaona zao la biashara haliwalipi waachane nalo.
Kilichotokea kina athari mpaka leo hii, wakulima wa kahawa waliamua kung'oa kahawa na wakapanda migomba na kuachana na zao ambalo haliwalipi.

Njia hiyo waliyotumia inaweza ikawa siyo sahihi ila kilichotokea miaka kumi baadae, serikali ilibidi ihamasishe tena kwa kuwabembeleza wakulima wa kahawa kuitikia wito kwa kuanza tena kuwahamasisha wakulima wapande kahawa kwa kuwahakikishia upatikanaji wa pembejeo kwa gharama nafuu sana na uwepo wa masoko ya uhakika.

Badala ya wakulima kuendelea kulalamika wachukue hatua ambazo wataona zitawasaidia na zitakuwa na manufaa na faida kwao


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Raisi Magufuli sikia kilio cha wakulima, Kwa nini mnatutesa hivo? Niliwekeza mtaji wangu usio pungua million 10 nikitegemea hali kuwa nzuri kama enzi hizo za kikwete. Matokeo yake serikali imepiga marufuku soko huria, ushirika unanunua kahawa Kwa bei ya chini.nmekatishwa Sana tamaa
 
Hapa ndipo Serikali yetu tukufu inakosea. Kwani kahawa wanataka iuzwe wapi si nje ya nchi? kwani Uganda au Rwanda si nje ya nchi? au kumuuzia mzungu ndo nje ya nchi kuliko kumuuzia Muafrika mwenzio mwenye uwezo wa kununua kwa bei kubwa kuliko hata huyo mzungu mnyonyaji?Kwani hizo fedha tutakazouza Uganda tutazitumia wapi si hapa Tanzania kwa kununua bidhaa mbalimbali na kuongeza mapato ya kodi?Mimi nadhani Serikali yetu ina mpango maalum wa kuwafanya watu maskini ili iwatawale kwa urahisi ., kwani mtu tajiri ajikombi kupata chochote.
 
Hii nchi kila unacho Fanya unakatishwa tamaa.. Wakulima, wafanya biashara,watumishi .wote ni kiliooooo
 
Jana nlikuwa nachangia uzi mmoja humu,Kuna mleta uzi mmoja alikuja na kuanzisha uzi humu akitaka serikali iweke askari wa kuzuia MAGENDO yasipitishwe mpakani!

Sasa badala ya kutafuta solution yeye anafikiria tumiaa miguvu akili hakuna!

Swali kwanini wenzetu jirani Wana bei nzuri hko wananunua?na hku nchini wanalalia kwenye ununuaji!

Hakuna mtu anayeweza uza bidhaa kwa bei ya chini wakati kuna sehemu amepata bei nzuri!hata kama uzalendo syo hivyo....

Lazima serikali na vyama hivyo vya ushirika vijitafakari!

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom