Serikali acheni kuwafunga Waethiopia/Wasomali, wana-hustle tu kama sisi

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786
Ni sawa wamevunja Sheria zetu kuingia kwenye nchini bila ya kibali lakini tusiwafunge na kuwatoza mafaini makubwa aidha tuwaache wapite au tuwarudishe.

95% ya Wasomali/Waethiopia wanaoingia nchini bila ya kibali wanapita tu wanakwenda AK kutafuta maisha, wana-hustle tu kama Wabongo wengi waliotapakaa Duniani kote, wanahustle. Hivyo tuwaachieni, hawachukui kazi wala kuhatarisha maisha ya Mtanzania yoyote. Hawa ni ndugu zetu.

Waasia wamejaa viwandani na mahoteli makubwa wanafanya kazi bila ya vibali hao ndiyo wa kukamata na kudhalilisha.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.

1605859436982.png

1605859459659.png
 
Kuna mikataba ya kimataifa ya kuzuia human trafficking, Tanzania imeiriehia, kwa hiyo nchi inachokifanya ni kutimiza Yale yaliyomo kwenye makubaliano hayo

Tunaweza kufumba macho, kwani mangapi tumesaini na hatuyafwati? Binafsi naumia sana kuona Mwafrika mwenzangu ambaye anahustle akinyanyasika namna hii, tuwaachie waende au tuwarudishe walikotoka, lkn siyo kuwafunga na kuwapiga mafaini makubwa.
 
Nasikia kuwasafirisha hao watu kuna hela nzuri ,mwenye kujua wapi naweza pata connection mtaa mgumu
 
Tunaweza kufumba macho, kwani mangapi tumesaini na hatuyafwati? Binafsi naumia sana kuona Mwafrika mwenzangu ambaye anahustle akinyanyasika namna hii, tuwaachie waende au tuwarudishe walikotoka, lkn siyo kuwafunga na kuwapiga mafaini makubwa.

Tz kuwaruhusu wapite waende AK Ni sawa na kubariki na Hilo Ni kosa kisheria... Pia na faini wanazopigwa zipo kisheria...

Labda kwakuwa nnchini kwao wanavita ya ndani ya nchi ingekuwa busara waombe kuwa wakimbizi wanao kimbia vita... Tz wakiwaruhusu kuwa wakimbizi hapo ndio kitakuwa kituo Cha muda ya safari zao kihalali...
 
Hao wanapita nchi nyingine kabla ya kufika Tanzania wanapita Kenya/Uganda mbona hausikiii wakikakmatwa na kudhalilishwa huko kama tunavyowafanyia, isitoshe wakishapita Tanzania hakuna ambaye anawakamata na kuwadhalilisha Waafrika wenzetu ni sisi tu, ...
 
Tz kuwaruhusu wapite waende AK Ni sawa na kubariki na Hilo Ni kosa kisheria... Pia na faini wanazopigwa zipo kisheria...

Labda kwakuwa nnchini kwao wanavita ya ndani ya nchi ingekuwa busara waombe kuwa wakimbizi wanao kimbia vita... Tz wakiwaruhusu kuwa wakimbizi hapo ndio kitakuwa kituo Cha muda ya safari zao kihalali...
Wewe ni mtoto wa mama kila kilala,hujui hata ugumu wa maisha ulivyo,waulize waxazi wako wanavyopata shida kukuhudumia,hao waethiopia ni wapitajiji tu,wanaenda kutatuta nafuu ya maisha kule mbele,na si wakimbizi.
 
We mesengere
Kwahiyo ww mtoto wa umbwA?
Usinitathimini kwa kunikejeri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom