Serikali acheni kutumia sheria kibaguzi na kulindana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali acheni kutumia sheria kibaguzi na kulindana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Father of All, Oct 18, 2012.

 1. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kifo cha kujitakia cha aliyekuwa kamanda wa polisi wa mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow kimeonyesha kuwa Tanzania inatumia sheria kibaguzi. Baada ya Barlow kuawa kutokana na kinchoonekana kuwa wivu wa kimapenzi, jeshi la polisi limehamanika kuliko wakati wowte. Mkuu wa upelelezi wa makosa jinai Manumba alisikika akiwaasa polisi kulipiza kisasi. Punde tu tunaambiwa watuhumiwa wameishanaswa. Ajabu wale majambazi wa EPA hadi leo hawajanaswa.
  Kumbe jeshi letu hufanya makusudi kushughulikia jinai,. Mbona wauaji wa Barlow wamepatikana hata kabla hajazikwa? Tuombe Mungu wafe vigogo wengi ili polisi wetu wazidi kuumbuka kwa kutumia sheria kwa upendeleo.
   
Loading...