Serikali acheni "Kutengeneza Kick" kwa gharama zetu; Bando za Data mlitudanganya, tuondoleeni kabisa hii Sheria ya Tozo

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,734
6,292
Nilipomsikia Mh Mwigulu kuwa wameagizwa na Mama kuangalia upya Tozo za miamala kuwa zinatia shaka ghafla nimekumbuka suala la Bando za data kupunguzwa kipindi kile na Mh Ndugulile. Zilipopunguzwa ziliibuka sarakasi nyingi na maneno yakawa ni mengi. Hatimaye Mama Samia akaagiza zirudishwe na watanzania wakampongeza na kufurahi sana. Kiuhalisia tatizo halikuondolewa. Na sisi watumiaji wakubwa wa mabando haya tunaona kuwa hazikurudishwaa bali ziliongezwa KIDOGO SANA. Kilichotokea ni tumefunika kombe, kuzizoea na mwanaharamu apite tunaendelea kuzitumia. Nilijiuliza tu ina maana MAMA hakujua chochote mpaka zinapopandishwa?

Suala hili la pili ambalo leo hii Mwigulu, Shigongo na wengine wanasema wameshaongea na Rais. Nimekumbuka juzi kuwa UVCCM nao walimuomba Rais aziangalie hizi tozo za miamala. Inaonekana kabisa kuna jambo linakuja so wanaanza kujibaraguza. Shigongo ni juzi tu alikuwa anapiga hesabu zake za kinafiki na kutuambia tulipe kodi. Kiuhalisia Mama Samia tangu Mh Zungu alipopendekeza hizi kodi kelele za wananchi zilikuwa nyingi na I am sure alizisikia. Mpaka siku zinapelekwa bungeni kujadiliwa na kupitishwa alitusikia tukipinga lakini alizipuuza kama zilezile za Bando za simu. Kama hilo halitoshi bado zikapitishwa na YEYE AKAPELEKEWA NA KUSAINI, Yaani aliziidhinisha. Asituambie kuwa hakuzisoma au wataalamu wake hawakumsomea, Lah alizisoma na hakuona athari ya makato hayo sababu hazijui hali zetu labda. Leo hii makelele yamekuwa mengi toka kwetu ambao hata wabunge wametukataa na kuamua kuwa wasemaji wa serikali ndiyo anaona noma na kuibuka kutoa kauli.
Inafikirisha sana.

Nini kinatokea ?. Tukumbuke suala la Bando halikuisha kwani halikuondolewa. Leo hii tumemsikia Mwigulu akisema "KWA KUWA SHERIA IMESHAPITISHWA NA BUNGE" , maana yake hawezi kuitoa ila watakachokifanya watarekebisha kanuni ambazo zitapunguza tu hiyo Tozo. Hii ni Cheap Politics ya KumCredit Mama lakini tatizo lipo palepale. Kiuhalisia Serikali inajua kuwa ina lengo lake la tozo so wameweka kubwa ili tukipigiwa kelele Mama aseme kitu zipungue kidogo kisha itakayobaki tuendelee kupasuka nayo. Mama Samia na Mwigulu walipaswa kuirudisha bungeni Sheria hiyo kwa hati ya dharura ili iende ikafutwe kama kweli wamesikia kilio chetu na suala la "Double Taxing".

Tengeneza tatizo kubwa Sana - Litatue kidogo upate political Mileage = Tatizo Kubwa

Tujiulize sasa, Kama zikipunguzwa, Zile Zahanati na Madarasa waliyotaka kujenga yatapungua Mangapi? Watatuambia au Watatumia ile Trilioni 5 ya kumwagwa mtaani?

E6pV2coXIAEDADq.jpg
 
Hakuna mwananchi atakuwa mzalendo kama kila siku anasikia upotevu wa fedha (kodi) huko serikalini. Hakuna mwaka tutapita bila kusikia upotevu wa pesa ambazo ni kodi za wananchi.

Kisha mwananchi huyohuyo unamkamua vilivyo ili kupata pesa ambazo zitaenda kujenga sijui barabara na vitu vingine. Imani katika hili mimi kama mwananchi sina kabisa.

Taifa linaenda kitumbukia kwenye shimo refu la umaskini kwa ubunifu wa kodi za ajabu zenye kupewa majina ya kuvutia kumbe ni kodi kandamizi kwa wananchi.

Kama mna nia ya kuchukua kila kilichopo kwa wananchi basi ahuweni mchukue kwa mitutu kuliko kuja na hizi kodi zenye majina ya kinafiki.
 
Back
Top Bottom