Serikal yaongeza mishahara ghafla?

mkuu hebu uwe siriazi bana, hizi ni tetesi ama???.....mbona utanifanya niende kukopa tena lol!
 
jaman mwenye habar kamili anijuze,ni kwel serikal imeongeza mishahara ya watumishi ghafla?

ina maana zaid ya walivyoongeza mwez wa saba wameongeza tena??? imetumika sheria gani kuongeza ama lile ongezeko la mwez wa saba walituchakachua??
 
Hakunaga kitu kama hiki ikiwa mpaka leo sisi polisi hatujapokea mshahara wa mwezi Oktoba sasa watawezaje kuongeza mshahara ,Tunaomba serikali msitugombanishe na wenye nyumba wetu.

mkuu kama ni kweli aisee nawapeni pole sana.
sasa kama serikali imeshindwa kuwalipa ni wazi kwamba haina hela kwa uwezo wangu mdogo wa kufikiri, na ikiwa kwamba CCM waliweza kufanya mkutano wa mamilioni kule Dodoma bila kujali kwamba kuna watumish ambao hawajalipwa mishahara basi CCM imekosea sana. Nafikiri kama iliweza kutafuta hela kwa wafadhili na popote pale ili kufanikisha ule mkutano basi wangeweza kutumia nguvu hizo hizo kutafuta hela za kulipa watumish wake kwakua CCM ndo serikali yenyewe...............
 
jaman mwenye habar kamili anijuze,ni kwel serikal imeongeza mishahara ya watumishi ghafla?

Yapandisha mishahara ya vigogo ghafla
*Waziri Kombani adai imefuata taratibu
*Wengine waongezewa Sh milioni moja
SERIKALI imefanya marekebisho ya mishahara kwa watumishi wake kwa mwaka wa fedha 2012/2013, MTANZANIA imebaini. Sambamba na hilo, mishahara ya viongozi wa Serikali kwa mwaka huo wa fedha, nayo imefanyiwa marekebisho.

Marekebisho hayo ni kwa mujibu wa waraka wenye kumbukumbu namba S/AC 205/ 399/ 01/ 44, kutoka Ofisi ya Rais Ikulu (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), uliotolewa Julai 25, mwaka huu.

Waraka huo, umesambazwa kwa wakuu wote wa idara za Serikali, wakurugenzi wa majiji, manispaa, miji na wakurugenzi wa halmashauri zote za wilaya nchini.

Waraka huo, uliosainiwa na Kaimu Katibu Mkuu (Utumishi), Hab Mkwizu, umehusisha pia marekebisho ya ngazi za mishahara kwa viongozi hao wa Serikali.

Kwa mujibu wa waraka huo, ngazi za mishahara zilizokuwa zinaanzia TGS I hadi TGS Q, zimebadilishwa na sasa zitasomeka LSS (E) 1 hadi LSS (E) 9.

Watumishi na viongozi wa Serikali walionufaika na marekebisho hayo, ni pamoja na makatibu wakuu wa wizara, manaibu wao pamoja na wakurugenzi wa idara zote za Serikali. Marekebisho hayo yameanza kutekelezwa Julai, 2012.

Hata hivyo, marekebisho hayo yamelalamikiwa na baadhi ya watumishi wa Serikali, wakidai kuwa hayana uwiyano unaoeleweka kati ya mishahara ya wamtumishi wa Serikali.

Marekebisho hayo yanaoneshwa katika kiambatanisho namba 1 cha waraka huo, ambapo watumishi na viongozi hao wameongezewa mshahara usiopungua 400,000.

Mfano mshahara wa mtumishi wa ngazi TGS P, umepanda kutoka Sh 3, 216, 000 hadi Sh 4, 500, 000 katika ngazi mpya ya LSS (E) 9, ongezeko ambalo ni zaidi ya Sh milioni moja.

Mmoja wa wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambaye hakutaka jina lake litajwe, alikosoa marekebisho hayo na kusema kuwa, hayana uwiyano mzuri kati ya mshahara wa mtumishi na mtumishi mwingine.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi), Celina Kombani, amekiri kuwapo kwa marekebisho hayo ya mishahara kwa watumishi na viongozi wa Serikali.

Akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya simu, Kombani alisema, marekebisho hayo ni ya kawaida na kwamba yanawagusa watumishi wote wa Serikali bila kubagua.

“Serikali ikifanya marekebisho ya mishahara, inafanya hivyo kwa watumishi wake wote. Hatuchagui nani aongezewe nani asiongezewe ni wote,” alisema.

Alisema vigezo vilivyotumika katika marekebisho hayo, ni pamoja na aina ya kazi, uzoefu na muda aliotumia mtumishi kukaa kazini.

“Unauliza kwanini watumishi wengine wamepewa nyongeza kubwa na wengine kidogo, ndugu yangu sifa zinatofautiana, mtumishi anayeanza kazi leo, hawezi kulipwa mshahara na mtumishi aliyepo kazini kwa miaka 20,” alisema.

Alipoulizwa ni sababu zipi zilizoifanya Serikali kurekebisha ngazi ya mshahara kutoka TGS na sasa kutumia ngazi mpya ya LSS, Waziri Kombani alisema. “Hayo ni masuala ya kitaalamu zaidi.”

Kombani alikiri kima cha chini cha mshahara ni kidogo na kueleza kuwa, Serikali ipo katika majadiliano.

“Kima cha chini kilipanda kutoka Sh 130, 000 hadi Sh 170, 000. Tunajua kima hiki hakitoshi lakini tupo katika majadiliano,” alisema.
 
Hakunaga kitu kama hiki ikiwa mpaka leo sisi polisi hatujapokea mshahara wa mwezi Oktoba sasa watawezaje kuongeza mshahara ,Tunaomba serikali msitugombanishe na wenye nyumba wetu.

mkome kabisa nyie polissm
 
wanatekeleza ilani ya chadema..bado elimu bure na gharama za vifaa vya ujenzi vikishushwa watakuwa wametekeleza kwa 2/4..
 
mkuu kama ni kweli aisee nawapeni pole sana.
sasa kama serikali imeshindwa kuwalipa ni wazi kwamba haina hela kwa uwezo wangu mdogo wa kufikiri, na ikiwa kwamba CCM waliweza kufanya mkutano wa mamilioni kule Dodoma bila kujali kwamba kuna watumish ambao hawajalipwa mishahara basi CCM imekosea sana. Nafikiri kama iliweza kutafuta hela kwa wafadhili na popote pale ili kufanikisha ule mkutano basi wangeweza kutumia nguvu hizo hizo kutafuta hela za kulipa watumish wake kwakua CCM ndo serikali yenyewe...............

unampa pole ya kazi gani, kurushia watu vitu vyenye ncha kali ama?
 
Hakunaga kitu kama hiki ikiwa mpaka leo sisi polisi hatujapokea mshahara wa mwezi Oktoba sasa watawezaje kuongeza mshahara ,Tunaomba serikali msitugombanishe na wenye nyumba wetu.

Hivi jamani, mtu anawezaje kuishi hajapewa mshahara wa miezi miwili au hata mmoja? Mbona mii kila mwezi lakini ukitoka hivyo ninavyoufakamia! Mungu yuwajua.
 
leo ktk mapitio ya magazeti kuna habari kwamba serikali imepandisha mishahara ni kweli? nisaidieni kujua ni kiwango gani
 
Back
Top Bottom