Serikal kuu vesus serikali za mitaa

GwaB

JF-Expert Member
Mar 19, 2014
1,564
2,000
Kati ya mambo yanayochelewesha maendeleo ya watu au taasisi binafsi zinazonuia kutoa huduma vijijini kwa wananchi pale ambapo kuna mahitaji ni kukosekana kwa miundombinu kiunganishi kati ya serikali kuu na serikali za mitaa. Kwenye ngazi ya kata kuna viongozi wanaoitwa wenyeviti wa vitongoji au kijiji ambao nagundua kuwa wao kazi yao ni kuonyesha njia na kuhamasisha.Katika ngazi hiyo hiyo ya kata kuna watendaji ambao wanatekeleza sera zilizowekwa na serikali iliyoko madarakani,hapa kuna watendaji wa kitongoji au kijiji ambao hadi leo najitahidi kujua kama wanateuliwa au wanaajiriwa kwa nafasi hizo.Watendaji katika ngazi ya kata ikiwa ni pamoja na jopo zima la watumishi wa halimashauri wana aina yao ya uongozi au utendaji ambao mimi binafsi nimeshindwa kuuelewa maana mara nyingi hawataki kuhimizwa kufanya kazi ambayo wanawajibika nayo, labda kwa kuwa hawasimamiwi na mtu au kwa kuwa wana mamlaka kamili na hawapaswi kusimamiwa na mtu mwingine isipokuwa wakurugenzi wa halimashauri.Kwa kuwa JF kuna hazina kubwa ya michango ya mawazo ningeomba wale wanaofahamu vizuri muundo na utendaji wa vyombo hivi viwili wanipe darasa ili nami niweze kuelimika kwenye hili. Nimeanza mada hii kwa kutoa angalizo la ucheleweshaji wa maendeleo ya watu kwa kuwa ndivyo ninavyodhani,ninapotafakari jinsi mambo yanavyoendeshwa ngazi za chini za utawala.Huo ni mtazamo wangu ambao yawezekana siyo sahihi na niko tayari kukosolewa.Natanguliza shukurani,
 
shige2

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
7,904

Mkuu nitachangia mada yako hii kama Mtanzania na si kama mtaalamu maana kuna wataalamu wengi humu waliobobea katika nyaza za LOCAL GOVERNMENT/ AUTHORITY/SERIKALI ZA MITAA.

Umesema kuhusu KUCHELEWESHWA kwa maendeleo ya watu. Mimi katika mtazamo wangu ni kuwa. Bila KUZIWEZESHA/ Kuzi Empower serikali za MITAA KIKAMILIFU hakutakuwa na MAENDELEO yeyote.

Maana Serikali za mitaa Local (gvt -Authority ndizo zilizo KARIBU na wananchi zaidi KULIKO serikali KUU.
Maana wanajua
NINI mahitaji ya WATU wao,
NINI ni KIPAU mbele katika Maendeleo ya watu wao.
SERIKALI KUU yaweza kuchelewa lakini serkali za mitaa ZIKIWA EMPOWERED kabisa na watendaji waache DILI DILI basi hizi local authority/ Mitaa ZINAWEZA KUBADILISHA kabisa SURA ya Tanzania.
Maana ikiwa kila MAAMUZI yatangojewa kutoka serikali basi kusema Maendeleo yaweza kuwa ndoto.
Lakini nafikiri kuna devolved functions siku hizi.
Ni jinsi gani ama kiasi gani zilivyowezeshwa hilo ndo swali kila mmoja wetu aweza kuchangia.
 
VeroEretico

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
389
500
Kati ya mambo yanayochelewesha maendeleo ya watu au taasisi binafsi zinazonuia kutoa huduma vijijini kwa wananchi pale ambapo kuna mahitaji ni kukosekana kwa miundombinu kiunganishi kati ya serikali kuu na serikali za mitaa. Kwenye ngazi ya kata kuna viongozi wanaoitwa wenyeviti wa vitongoji au kijiji ambao nagundua kuwa wao kazi yao ni kuonyesha njia na kuhamasisha.Katika ngazi hiyo hiyo ya kata kuna watendaji ambao wanatekeleza sera zilizowekwa na serikali iliyoko madarakani,hapa kuna watendaji wa kitongoji au kijiji ambao hadi leo najitahidi kujua kama wanateuliwa au wanaajiriwa kwa nafasi hizo.Watendaji katika ngazi ya kata ikiwa ni pamoja na jopo zima la watumishi wa halimashauri wana aina yao ya uongozi au utendaji ambao mimi binafsi nimeshindwa kuuelewa maana mara nyingi hawataki kuhimizwa kufanya kazi ambayo wanawajibika nayo, labda kwa kuwa hawasimamiwi na mtu au kwa kuwa wana mamlaka kamili na hawapaswi kusimamiwa na mtu mwingine isipokuwa wakurugenzi wa halimashauri.Kwa kuwa JF kuna hazina kubwa ya michango ya mawazo ningeomba wale wanaofahamu vizuri muundo na utendaji wa vyombo hivi viwili wanipe darasa ili nami niweze kuelimika kwenye hili. Nimeanza mada hii kwa kutoa angalizo la ucheleweshaji wa maendeleo ya watu kwa kuwa ndivyo ninavyodhani,ninapotafakari jinsi mambo yanavyoendeshwa ngazi za chini za utawala.Huo ni mtazamo wangu ambao yawezekana siyo sahihi na niko tayari kukosolewa.Natanguliza shukurani,
Mkuu kwanza kabisa kuhusu hao watendaji wa vijiji/ kata ni wajiriwa wa serikali na nafsi zao hutangazwa na hufanyiwa usaili na kuajiliwa utumishi wa umma zamani ilikuwa kuanzia elimu ya form four lakini siku hizi lazima wazie elimu ya cheti, stashahada, shahada ktk fani za utawala , sociology , na kadhalika ila kwenye ngazi ya cheti na diploma wana chuo chao cha Serikali za mitaa Homboro- Dodoma , watendaji wa kijiji/ kata wapo chini ya mkurugenzi ( TAMISEMI) .
Kuhusu muundo huu wa Tamisemi ngazi za chini
1. Kijiji. a) mtendaji wa kijiji ni katibu/ mtendaji/msemaji wa mambo yote yanayohusu serikali ktk ngazi ya kijiji, ni katibu wa mwenyekiti wa kijiji
Mwenyekiti wa kijiji pamoja wa wenyeviti wote vitongoji ndio wana unda serikali ya kijiji hivyo mambo yote yanayohusu maendeleo ya kjiji kweye vikao vyao ndiyo yanaratibiwa na mtendaji wa kijiji na huyatolea mhutasari na kuupeleka kwa mtendaji wa kata au moja kwa moja kwa Mkurugenzi mtendaji (W) pia ngazi hii ina institution ( taasisi) kama shule za msingi/ Secondary, zahanati, idara za kilimo/ mifugo , afya e.t.c hizo zote huandaa bajeti ya kijiji na kuipeleka kwenye kikao cha WDC pamoja na kutekeleza maagizo kutoka juu na kusolve matatizo kijijini.
2. Kata huundwa na Diwani, mtendaji wa kata pamoja na watumishi wote wa aerikali ngazi ya kata kama maafisa kilimo/ mifugo, mratibu elimu kata, afisa mendeleo jamii, afisa afya.
Diwani ni mwenyekiti wa W. D .C na wajumbe wake ni wenyeviti wa vijiji vyote vinavyo unda kata , mtendaji kata ndio katibu wa kikao hicho pamoja wataalamu wote katani ndio hushauli kikao hicho pamoja na kujadili bajeti ya kata nzima na kuituma kwenye full concel ( kikao cha madiwani wilayani)
Hivyo serikali za mitaa ndizo zinazotekereza maagizo yote yanayotolewa na serikali kuu na zinatoa huduma kwa wananchi kwa niaba ya serikali kuu
 
Eudorite

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
1,138
2,000
Hapo juu utakuwa umejibiwa vyema. Tofauti yabserikali kuu na serikali za mitaa ni anuai lakini kwa kifupi serikali za mitaa ndizo hushughulika moja kwa moja na maendeleo ya huduma za jamii na ulinzi wa wananchi kila siku. Pia serikali hizi ni wawakilishi wa serikali kuu.

Ngazi ya juu ni ngazi ya Halmashauri ambayo Mwenyekiti wa Kanseli au Meya ni kama Spika na Mkurugenzi wa Halmashauri ni kama waziri mkuu ambapo baraza la madiwaji ni kama bunge la Jammhuri. Hivyo madiwani ni kama wabunge na wakuu wa idara na vitengo kama mganga mkuu wa wilaya. Afisa elimu wa wilaya nk. ninkama mawaziri.

Baraza la madiwani hutunga sheria husimamia na kupitisha bajeti ya halmashauri husika.

Chini ya baraza la madiwani kuna baraza la kata na chini yake kuna halmashauri ya kijiji.

Vikao hivi vitatu ni vya kiutendaji na kiutawala ndani ya halmashauri na huamua aina ya maendeleo wanayoyataka.

Ikumbukwe kwa tanzania serikali za mitaa zinaunganishwa na kitu kinaitwa Tawala za mikoa ambazo ni mikono ya serikali kuu, hizi tawala za mikoa zikiondoka nchi inakuwa na majimbo.

Tawala za mikoa zinahusisha taasisi za Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Ofisi ya Mkuu wa Wilaya. Mkurugenzi wa halmadhauri. Ofisi ya Katibu Tarafa. Mtendaji wa kata mtendaji wa kijiji au mtaa na mtendaji wa kitongoji.
 
Emmathias

JF-Expert Member
Jan 22, 2018
311
250
Asante sana kwa elimu nzuri, swali langu Je, mtendaji anaruhusiwa kuingia kwenye baraza la madiwani?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom