Seriakali ya CCM inafanya maamuzi kana kwamba wao ndio kizazi cha mwisho TZ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Seriakali ya CCM inafanya maamuzi kana kwamba wao ndio kizazi cha mwisho TZ

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Livanga, Jul 6, 2011.

 1. Livanga

  Livanga JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2011
  Joined: Apr 15, 2010
  Messages: 458
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Ni jambo la kushangaza sana kuona wasomi na akili zao zote wanakubaliana na mambo yasiyokuwa na msingi yoyote kisa tu wako kishabiki zaidi ya kizalendo. CCM ni chama tu ambacho hakiwezi kudumu milele bali kizazi kinakuwa na kitaendelea kukua hata kama nyinyi mliopo bungeni sasa ivi mtakufa, kwanini hamkumbuki kama mna watoto na wajukuu, kwanini hamfanyi maamuzi yenye busara na kwa faida yenu na vizazi vijavyo, je mnafikiria kabla ya kutenda na je mnajua kwamba mnawaweka watoto na wajukuu zenu katika hali ngumu sana kimaisha siku zijazo. Utakapokuwa babu au Bibi unategemea utasifiwa na nini wewe? je utasifiwa kuliangusha taifa kwenye matatizo makubwa kama umeme, maji na umasikini uliopindukia, nitakuwa sijakosea kabisa kama nitawaita vichwa vya wendawazimu na mwingine nikamuita kubwa jinga.

  kama mkiona nakosea basi naomba mjibu maswali yangu na ya wadau wengine wengi watakaoendelea kuuliza kwani mimi naamini siwezi kuyamaliza yote
  1. Mlitegema nini lutokana na maamuzi yenu ya siyokuwa na busara na umimi uliokidhiri.
  2. Kwanini mnatunga sheria ambazio nyie wenyewe hamuwezi kuzitekeza (mfano mpango wa maendeleo wa miaka mitano)
  3. kama nyinyi sio makubwa jinga na kwanini mnafundishana kila kukicha na bado hamuelewi ( semina elekezi)
  4. Nini maana ya nguvu zaidi hari zaidi na kasi zaidi, si ndio haya yanayotokea ssa ivi shilingi kushuka kwa kasi ya ajabu
  5. Hivi kweli mnadhubutu vipi kusema posho hazitoshi na zisifutwe ilihali mwalimu analipwa mshahara wa 192,000/= na mnapata hadi posho kumi
  6. bila mwalimu wewe mbunge wa CCM ungekuwa hapo bungeni kweli wewe je ungekuwa unajua kusoma na kuandika
  Naomba niungane na Sabodo kwa kumpongeza Zitto kwa kutufungua macho na kuongea ukweli kwani nina amini hakua kipindi wananchi wanafuatilia serikali yao kama kipindi hiki
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Asanteeee.......aje mchangiaji mwingine....
   
Loading...