Serengeti

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Do we need more hotels in Serengeti to increase Watalii or we need to be creative to maximize the facilities in place to provide quality services that Watalii will feel comfortable to pay for?

Nukuu kutoka gazeti la Mwananchi. Someni maoni ya Mkurugenzi.


Hoteli za kitalii kujengwa Serengeti
Na Anthony Mayunga, Serengeti

SERIKALI imesisitiza nia yake ya kujenga hoteli nyingi za kitalii hifadhi ya Taifa ya Serengeti ili kuongeza mara dufu idadi ya watalii wanaotembelea hifadhi hiyo katika kipindi cha miaka 10 ijayo.

Idadi ya watalii itaongezeka mara mbili kutoka 700,000 kwa kipindi hicho kutokana na mikakati hiyo.


Azma hiyo ya serikali,ilitangazwa na Waziri wa Maliasili na utalii Shamsa Mwangunga katika mkutano wa kimataifa kuhusu uwiano wa utalii na uhifadhi wa baoinuai na mazingira ,uliofanyika katika hifadhi hiyo.


Akifungua mkutano huo, uliowashirikisha wataalam wa mazingira , wanasayansi na wawekezaji katika sekta ya utalii nchini,alisema nia ya serikali ni kuona rasilimali zilizopo kwenye hifadhi hiyo zinawanufaisha Watanzania na vizazi vijavyo.

Waziri huyo, alisema kwa kufanya hivyo, serikali itakuwa imepanua wigo wa utalii na kuliwezesha taifa kupata mapato mengi kutokana na hoteli nyingi kukodishwa na wageni na watalii wengi watakaoingia nchini kutoka ndani na nje ya nchi.

" Serikali itafuatilia ili kuhakikisha ujenzi huo hauathiri mfumo wa ikolojia, na kutosababisha wanyama kuhama makazi yao kutokana na uharibifu wa mazingira," alisema .

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Gerard Bigurube ,alisema utalii unaotakiwa katika mwelekeo mpya ni ule wenye thamani kubwa wala si ule wa wageni wengi.

Naye Mtaalam wa Kimataifa wa Mazingira, Profesa Anthony
Sinclear kutoka Chuo Kikuu cha British Columbia cha nchini Canada , alisema Serengeti ni hifadhi yenye umuhimu wa kipekee duniani na inaweza kuinua haraka uchumi wa taifa ikiwa uwiano kati ya Utalii na uhifadhi wa mazingira utazingatiwa

Awali Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Serengeti, Martin Loiboki alifafanua kuwa, ili kukabiliana na wimbi la ujangiri ambao unaathiri utalii kwa kuua wanyama, hifadhi hiyo imeajiri askari 50 wa ulinzi, ikiwa ni hatua ya kwanza ya kuimarisha utalii.

Mkutano huo uliandaliwa na Tanapa kwa ushirikiano na taasisi ya uhifadhi wa wanyamapori ya Frankfurt Zoological Society ya Ujermani. Lengo ni kutafakari na kupata mwelekeo mpya wa utalii na uhifadhi wa mazingira katika hifadhi hiyo iliyoanzishwa mwaka 1959 chini ya muasisi wa Uhifadhi nchini na Raiswa kwanza wa Tanzania, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
 
Do we need more hotels in Serengeti to increase Watalii or we need to be creative to maximize the facilities in place to provide quality services that Watalii will feel comfortable to pay for?

Nukuu kutoka gazeti la Mwananchi. Someni maoni ya Mkurugenzi.


Rev.Kishoka
Haya ni mambo ya Lowasa ya ku copy na ku paste.Wakasema Kenya wana kiwanja mbugani .Mie nikaenda kenya kiwanja cha ndege nakuta wanaongelea Wilso air strip nikachoka kabisa .Kuna deals akina JK na wakuu wenzake walisha setup.Baada ya kuona ugumu wa kule ndiyo wamempa Wanyancha hongo ya Unaibu waziri akae kimya na wao wajenge hotels zao.Je ni hotels za Serikali ama za wawekezaji ? Wakisema ni wawekezaji ujue the deal is complete na JK na Lowasa wamo .Hakuna ubishi na wakipinga tutaleta nondo hapa na hata jina la Hotel tunalijua labda wabadili baada ya kuona bandiko hili .

Nchi imeliwa wabunge na maziri wengi wana CCM karibia kila mmoja ana kipande chake huko Mbugani .Kama huamini jaribu kufuatilia kuanzia leo .
 
Kimsingi sasa hivi yeyote atakaye ingia madarakani anaangalia wapi afanye manuva ili apate chake. Siasa za kusema tuongeze watalii si za kweli maana sawa wanaweza lakini taifa lisinufaike kabisa kama ilivyo ktk madini. Kama serikali inajenga hizo hotel ok lakini ninaona ni mabepari tu wanataka ku hold hicho kivutio cha dunia. We need to be careful Tanzania especially to the natural resourses. By the way why to build a hotel inside the national parks? Why not the government create a small town out of national park and buld a nice road to the national park?
 
Hivi serikali haiwezi kufanya jambo lolote kwa sasa bila 10% mbele au kuwepo manufaa binafsi?

Kwa kweli mwelekeo wa Tz umebadilika.. may be kama alivyofanya Mwal. raslimali zetu zikae kwanza hadi misingi ya kimaadidi na uwezo wa kielimu viongezeke!

Mfano wa Kenya..Kenya has one of the highest Inequalites in the World..kweli wawekezaji ni wengi-- but who is benefitting from such resources? Ona maana sasa watu wanachinjana!

JF tuendelee kufuchua deal mbovu ktk kujenga mahoteli Serengeti na kuyaanika majina ya viongozi/mafisadi hapa!
 
Jamani,

Hawa planners wetu sijui wakoje. Tuongeze hoteli ili kuongeza watalii na mapato? je ubora wa huduma?

  • Je serikali inapata hasara gani kutokana na hoteli zilizopo?
  • Je serikali imepata mapato kiasi gani kutokana na hote,li ilizopo?
  • Je tukiongeza hoteli na kuweka viwanja vya ndege, je makisio yetu ni uchumi kuongezeka kwa kiasi gani na mapato hayo kwa kiasi gani na yatatumika vipi?
  • Je wameshawahi kuomba maoni ya watalii kujua ni kitu gani kinahitajika ili kuboresha huduma za utalii? kama maji, vyoo, majiko, vyakula, magari, vyandarua, vitanda, mahema au wasaidizi?
  • je ecosystem ambayo ipo sasa hivi, wanafikiri itaaribika namna gani ikiwa binaadamu tutaendelea kuingilia hifadhi hizi?
  • Je katika mipango yua kuimarisha utalii huu, wamezingatia kuwepo kwa namna ya kuhakikisha Wanyama hawa wanaongezeka kwa vizazi kwa kuhakikisha kuwa vyanzo vya chakula na maji ni wazi kwa wanyama hawa bila kuingiliwa na binaadamu au takataka?
  • Je wanafanya sensa kuangalia idadi ya wanyama waliopo na jinsi ya kuratibu mfumuko wa wanyama au kupungua wanyama hawa? Je fedha za utafiti huu zinatokana na mapato ya utalii au ni misaada kutoka National Geographic?
  • Tukiweka hoteli hizi mpya, ina maana tuongeze makazi kwa wafanyakazi na hivyo tutegemee wananchi wa kawaida waanze kusogea kwenye hifadhi hizi, je kuna mipango gani kuhakikisha kuwa hili halitokei?
Ukiangalia kwa undani, sisi Watanzania hukimbilia sana kuanzisha vitu vipya eti kujiongezea mapato, huku tukiwa tumeshindwa kabisa kuvihudumia vianzo vya uzalishaji mali vilivyopo. Sijui ni ufupi wa utaalamu au ni jazba ya kuanzisha "elephant project" kwa kuwa pesa zitaletwa na wahisani na wawekezaji?

Lets save Serengeti, Ngorongoro and be creative to improve number of tourists and revenues by improving and modernizuing facilities that are in place and not wasting resources to expand services by adding new infrastructure while our services and promotion to attract more tourists sucks!
 
Yale yale ya kumchinja bata anayetaga mayai ya dhahabu! Hao wanaojiita wapinzani wako wapi kwenye hili? Na lile la Ziwa Natron? Mungu ainusuru nchi yetu!
 
Back
Top Bottom