Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,533
Do we need more hotels in Serengeti to increase Watalii or we need to be creative to maximize the facilities in place to provide quality services that Watalii will feel comfortable to pay for?
Nukuu kutoka gazeti la Mwananchi. Someni maoni ya Mkurugenzi.
Nukuu kutoka gazeti la Mwananchi. Someni maoni ya Mkurugenzi.
Hoteli za kitalii kujengwa Serengeti
Na Anthony Mayunga, Serengeti
SERIKALI imesisitiza nia yake ya kujenga hoteli nyingi za kitalii hifadhi ya Taifa ya Serengeti ili kuongeza mara dufu idadi ya watalii wanaotembelea hifadhi hiyo katika kipindi cha miaka 10 ijayo.
Idadi ya watalii itaongezeka mara mbili kutoka 700,000 kwa kipindi hicho kutokana na mikakati hiyo.
Azma hiyo ya serikali,ilitangazwa na Waziri wa Maliasili na utalii Shamsa Mwangunga katika mkutano wa kimataifa kuhusu uwiano wa utalii na uhifadhi wa baoinuai na mazingira ,uliofanyika katika hifadhi hiyo.
Akifungua mkutano huo, uliowashirikisha wataalam wa mazingira , wanasayansi na wawekezaji katika sekta ya utalii nchini,alisema nia ya serikali ni kuona rasilimali zilizopo kwenye hifadhi hiyo zinawanufaisha Watanzania na vizazi vijavyo.
Waziri huyo, alisema kwa kufanya hivyo, serikali itakuwa imepanua wigo wa utalii na kuliwezesha taifa kupata mapato mengi kutokana na hoteli nyingi kukodishwa na wageni na watalii wengi watakaoingia nchini kutoka ndani na nje ya nchi.
" Serikali itafuatilia ili kuhakikisha ujenzi huo hauathiri mfumo wa ikolojia, na kutosababisha wanyama kuhama makazi yao kutokana na uharibifu wa mazingira," alisema .
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Gerard Bigurube ,alisema utalii unaotakiwa katika mwelekeo mpya ni ule wenye thamani kubwa wala si ule wa wageni wengi.
Naye Mtaalam wa Kimataifa wa Mazingira, Profesa Anthony
Sinclear kutoka Chuo Kikuu cha British Columbia cha nchini Canada , alisema Serengeti ni hifadhi yenye umuhimu wa kipekee duniani na inaweza kuinua haraka uchumi wa taifa ikiwa uwiano kati ya Utalii na uhifadhi wa mazingira utazingatiwa
Awali Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Serengeti, Martin Loiboki alifafanua kuwa, ili kukabiliana na wimbi la ujangiri ambao unaathiri utalii kwa kuua wanyama, hifadhi hiyo imeajiri askari 50 wa ulinzi, ikiwa ni hatua ya kwanza ya kuimarisha utalii.
Mkutano huo uliandaliwa na Tanapa kwa ushirikiano na taasisi ya uhifadhi wa wanyamapori ya Frankfurt Zoological Society ya Ujermani. Lengo ni kutafakari na kupata mwelekeo mpya wa utalii na uhifadhi wa mazingira katika hifadhi hiyo iliyoanzishwa mwaka 1959 chini ya muasisi wa Uhifadhi nchini na Raiswa kwanza wa Tanzania, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.