Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,476
- 4,752
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), imeagizwa kulipa faini ya asilimia tano ya mapato yake yote ya mwaka jana kwa Tume ya Ushindani (FCC), baada ya kubainika kuihujumu Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kibiashara.
Hukumu hiyo dhidi ya TBL, ilisomwa makao makuu ya Tume hiyo, Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa FCC, Nikubuka Shimwela, kutokana na kesi mbili zilizofunguliwa na kampuni hizo mbili TBL na SBL, kila moja ikimshitaki mwenzake kwa ‘kumchezea rafu' sokoni.
TBL ilitakiwa kulipa asilimia tano ya mapato ambayo tayari yamekaguliwa na Mkaguzi wa Nje ili kuondoa uwezekano wa kudanganya mapato halisi iliyopata mwaka jana.
Shimwela alisema baada ya kusikiliza mashitaka ya pande zote mbili, Tume hiyo ilibaini kuwa TBL iliihujumu SBL kutokana na kuendesha kampeni ya kuondoa alama zake sokoni na kuagiza wamiliki na mameneja wa baa mbalimbali nchini, kutouza bidhaa za SBL na badala yake kuuza za TBL pekee.
Alisema kupitia kampeni hiyo, TBL iliwaamuru wamiliki wa baa na mameneja, kuondoa mabango na vipeperushi vinavyoitambulisha SBL sokoni na vifaa vinavyotumika kibiashara kama majokofu, viti na meza na kuweka mabango na meza zake pekee, hatua ambayo ni kosa kwa mujibu wa sheria ya ushindani wa kibiashara ya mwaka 2003.
Katika hukumu hiyo iliyosomwa kwa zaidi ya saa moja, Mwenyekiti wa FCC alisema pia Tume hiyo ilibaini kuwa TBL iliingia mikataba na wamiliki na mameneja wa baa, ili kuwashinikiza kuuza bia za TBL na kutouza za SBL, hatua ambayo pia ni kosa katika ushindani wa kibiashara.
Alisema pamoja na kuita mashahidi kutoka mikoa mbalimbali waliothibitisha TBL kuhusika na kampeni hiyo, TBL yenyewe katika utetezi wake uliowasilishwa katika Tume hiyo na shahidi wake wa kwanza, David Mgwasa, ilikiri kuhusika na vitendo hivyo kwa madai kuwa ilikuwa inaondoa 'takataka' katika baa ilizozifanyia ukarabati kwa kupaka rangi na kuweka alama zake.
Alisema katika uamuzi wake, Tume hiyo pamoja na kuitaka TBL kulipa faini hiyo au kukata rufaa katika kipindi cha siku 21 tangu siku ya hukumu, lakini imetengua makubaliano yote yaliyokuwa yamefanywa baina yake na wamiliki au mameneja wa baa, ya kutaka kuuza bidhaa za TBL pekee na kutengua pia maafikiano ya kuweka alama za TBL pekee.
Alisema hatua ya kuondoa mabango au alama zinazoonesha uwepo wa bidhaa za SBL ni kosa kisheria, kwani inahujumu jitihada zinazofanywa na SBL katika kuwafahamisha wateja wake maeneo yanayouza bidhaa zake, hatua ambayo haikubaliki katika soko la ushindani.
Wakati SBL ilifungua mashitaka mawili katika Tume hiyo la kuondolewa kwa mabango na alama zake kwenye baa na la TBL kufanya kampeni za kushawishi wenye baa na mameneja kutouza bidhaa za SBL, TBL ilifungua kesi ikiilalamikia SBL kuwa ilikuwa inatumia masanduku na chupa za TBL kujaza bidhaa zake na kuzisambaza badala ya kuingiza kwenye soko chupa na masanduku yake.
Katika uamuzi wake, Tume hiyo ilisema hoja hiyo ya TBL ilishindwa kuwatia hatiani SBL, kwa vile chupa na masanduku vilivyokuwa vikitumiwa na kampuni zote mbili, vilikuwa vikifanana kwa kiasi kikubwa na hivyo kushindwa kubaini ni mali ya nani baina yao, kwa vile hakukuwa na alama zinazotambulisha kampuni mojawapo.
Source: Gazeti la Habari Leo
Hatimaye haki imetendeka hapa.............TBL wameonesha udhaifu hasa katika ushindani mbele ya SBL