Serengeti: Watu 40 wanashikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na ghasia za mgogoro wa ardhi ulioua watu 2

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Takriban watu 40 wamekamatwa na maafisa wa polisi nchini Tanzania kufuatia mauaji ya watu wawili waliouawa kutokana na mgogoro wa ardhi.

Mgogoro huo unashirikisha takriban hekari 4,000 za ardhi za kilimo karibu na mbuga ya kitaifa ya wanayama pori ya Serengeti.

Wawili hao waliuawa kwa kukatwakatwa mapanga siku ya Ijumaa wakati walipokuwa katika na kijiji chao cha Remng'oroni .

Washambuliaji hao ambao maafisa wa polisi wanasema walibeba mishale baadaye walitorokea katika nyumba zao katika kijiji jirani.
 
Back
Top Bottom