BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 422
- 1,049
Baadhi ya wananchi wamewatuhumu wanaodhaniwa kuwa ni askari wa wanyamapori katika Hifadhi ya Serengeti kwa kuteka wananchi huku ikidaiwa kuna baadhi ya watu wanapotea kusikojulikana katika mazingira ya kutatanisha.
Gumzo kubwa kwa sasa ni kupotea kwa Nyamuhanga Mnanka (40) mkazi wa Mtaa wa Lubana, Kata ya Balili ambaye alipotea tangu Januari 5, 2022.
Bhoke Mnanka ni kaka wa Nyamuhanga, anasema: “Siku ya tukio walikuja magari mawili ya askari hao wakiwa katika mgari ya hifadhi wakamkamata na kuondoka naye, alikuwa shambani, wakazungumza naye kirafiki ghafla wakamkamata na kumtupa kwenye gari wakaondoka naye, hawakurudi tena, hizo gari hazikuingia ndani ya hifadhi zilipotea kusikojulikana.”
Naye, kaka mkubwa wa Nyamuhanga, Marwa Mnanka anasema: “Mpaka sasa hawajui alipo, wahifadhi majibu yao nao wanasema wameuliza kambi zote, hawajamkamata, ndiyo maana watu hawana imani na askari wenye hifadhi.”
Jambo jingine linalodaiwa kutokea ni vipigo kwa raia.
Mkazi wa eneo hilo, Emmanuel Mayila Abdallah (60) amedai kuwa amewahi kuwa mwathirika kwa hao wanaodhaniwa ni askari wa wanyamapori, anasema:
“Kuna vijana waliwahi kunivamia nikiwa ndani ya eneo la kiraia, nikawaambia sipo sehemu ya hifadhi lakini walinivamia na kunipiga sana, wakaniwekea silaha kitovuni, niliokolewa baada ya mke wangu kutokea, alinikuta kwenye hali mbaya sana.”
Mwenyekiti wa Mtaa wa Lubana, Kata ya Balili, mzee Marase Kilangi anasema matukio kama hayo ni kawaida kutokea mtaani hapo.
“Kuna watu kama sita wamepotea na hatujui wako wapi. Tumepambana kuwatafuta lakini hatujawapata, tumeshirikiana na Askari Polisi lakini hatujafanikiwa,” anasema.
Kamishna wa Hifadhi Kanda ya Magharibi, Martine Bhoke alipoulizwa kuhusu hilo alisema: “Ndio kwanza tunasikia hizo taarifa, tutafuatilia, kama wananchi wana malalamiko wafikishe katika vyombo stahiki.”
Chanzo: Watetezi TV