Serengeti: Mfano wa Majimbo yatima ...loh!Naona sasa Elimu ya uraia nayo ni tatizo kwa Wabunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serengeti: Mfano wa Majimbo yatima ...loh!Naona sasa Elimu ya uraia nayo ni tatizo kwa Wabunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ben Saanane, Jun 30, 2011.

 1. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #1
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Stephen Kebwe,mbunge wa jimbo la Serengeti anaonyesha kabisa kwamba suala la elimu ya uraia kwake ni tatizo.

  Anajenga hoja kwamba kuna wanasiasa wanaotaka kujifunza siasa kupitia uhamasishaji wa migomo vyuo vikuu,analaumu na kulaani wanafunzi kufanya maandamano at the same time anakiri kwamba matatizo ya wanafunzi yaliyoko vyuoni ni kwa sababu wanakosa haki yao kwa hiyo inakuwa rahisi kuwa triggered kufanya maandamano na migomo kwa kuwa wanaahidiwa kwamba watasaidiwa!

  Anashindwa kuelewa kwamba Maandamano ni njia mojawapo ya kudai haki.Maandamano ni njia ya kuhamasisha jambo muhimu na lenye manufaa.Mwalimu Nyerere alifanya na kuhamasisha maandamano ya kuunga mkono azimio la arusha kutoka Musoma,Seti Benjamaini mojawapo wa mashujaa wa Azimio la arusha na Taifa kwa ujumla alifariki akiwa njiani kwa kutembea umbali mrefu katika jitihada za kuunga mkono azimio la Arusha.

  Anaongelea hoja ya Upinzani kupunguza posho za Semina ya ukimwi na Malaria,anapinga kwa kupotosha kwamba upinzani unataka vijana wetu wafe.Sijui kama amefanya tafiti na kujua kiasi halisi kinachotumika vs Kiasi kinachoombwa na sijui kama amefanya Evaluation na Research katika hilo

  Kwa hoja zake hizi anajipa Moyo na kuwahimiza watu wa serengeti wawe na msimamo na kukataa hoja za upinzani.Tafadhali wana wanaserengeti mlioko humu jiandaeni kwa kutoa Elimu ya Uraia jimboni mwenu,hili jimbo ni kama halina mbunge kabisa.Wanaserengeti ni miongoni mwa majimbo yasiyo na uwakilishi unaostahili

  List ya majimbo yatima inaendelea.............hili Bunge la bajeti litatoa Reflection ya the wrong and the right choice of People!
   
 2. m

  mwanza_kwetu JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 684
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  I agree with you
   
 3. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #3
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Ni lazima wananchi wajue kile anachofanya mbunge wao bungeni
   
 4. Andrew Kellei

  Andrew Kellei JF Gold Member

  #4
  Jun 30, 2011
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Bwana Misosi alivyoimba NITOKE VIPI hakukosea.
  Huyo kachagua njia yake atoke hivyo.Anafikiri kwa alichoongea atajijengea umaarufu na ataonekana walau naye anatoaga michango bungeni.
  Ingekua ni amri yangu michango kama hii nisingeiruhusu maana badala ya kujenga inabomoa.
   
 5. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ben, hilo tunalijua tangu huyu mkulu alipochakachua matokeo ya uchaguzi mkuu mwaka jana na kushinda, tulishajua tumelamba garasa. Hata hivyo ahsante kwa muhtasari wa pumba alizotema mbunge wangu huko mjengoni, kwa kweli inasikitisha sana.

  Kwetu hilo si jambo geni, kwakuwa huyo bwana hajui hata kuongea, wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana alikuwa anafanyiwa kampeni na wapambe, yeye mwenyewe hawezi kuongea pointi hata kidogo. Alifika mahali akataka kujitoa kwenye kinyang'anyiro baada ya kukumbwa na zomea zomea ya wananchi.

  Huyo mbunge wakati huo akiwa mganga mkuu wa mkoa wa mara ndipo mgodi wa barrick north mara walipotiririsha maji yenye sumu kuingia mto tigithe na kusababisha magonjwa na vifo kwa wakazi wa nyamongo pamoja na wananchi wengine wanaotumia maji ya mto huo. Baada ya taarifa zile kuanikwa hadharani na vyombo vya habari yeye alikuwa ni mtu wa mwanzo kukanusha taarifa za watu na mifugo kufa kutokana na sumu zilizotiririshwa na barrick, na kuanzia hapo ndipo watu wa mara na hususan serengeti walianza kumuona hafai kwa kushindwa kusimamia maslahi ya wananchi wanyonge.

  Kwa taarifa yako hana hata jeuri ya kuitisha mkutano wa hadhara mugumu mjini, na tangu "amechaguliwa" amekuwa akijichimbia nyumbani kwao ngoreme, akija mugumu mjini anaingia kimya kimya utadhani sio mbunge. Wananchi wa serengeti wana matatizo mengi sana kuanzia kwenye elimu, miundombinu, afya, ardhi na zaidi ya yote ukosefu wa utawala wa sheria(utawala bora) hayo ndio mambo ambayo angalau angeweza kuyasemea ili aonekane anawajibika kwa wapiga kura wake lakini hana lolote analofanya, kweli huu mwaka wa hasara kwa wanaserengeti.

  Ila jambo la muhimu ni kwamba tumeanza kujiandaa vizuri ili 2015 tupate mwakilishi anayekubalika na wananchi na anayewakilisha matakwa ya wananchi, hawa mamisukule ya wanamagamba hawana msaada wowote zaidi ya kutetea posho. Wapo vijana wengi tu wenye uwezo, maarifa na elimu za kuwawezesha kuwa wawakilishi bora wa wanaserengeti. Na kwa kupitia forum hii ninawasihi wanaserengeti wenzangu tujipange vizuri tangu sasa ili tusijeaibika tena 2015. Najua mzee serengeti, chomete na wengine wengi mtajiunga pamoja na wanaserengeti wenzenu kuhakikisha hatulambi garasa tena.
   
 6. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #6
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Mwita,

  2015 zaidi ya aslimia 75 ya wabunge watarudi nyumbani,bunge linaweza kuwa na sura mpya kabisa.jiandaeni vyema mpate mpiganaji
   
 7. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,628
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 160
  What do you expect from a rural medical aid turned law maker
   
 8. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #8
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Kuna mwingine sasa anaongelea siku ya Uhuru sasa tuchinje nyumbu,tembo,tuwagawie wanafunzi wafurahi.Anasema tangu tupate uhuru tumefanya mengi mno,wanaoongea vibaya ni kwa sababu mdomo haulipiwi kodi.Duh!
   
 9. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #9
  Jun 30, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,628
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 160
  Ukifuatilia bunge hili la 10 utashangaa jinsi idadi kubwa ya wabunge wasivyojua hata wajibu wao wacha swala lakuwa na hoja zenye mashiko...It tell you its terrible.
  .
   
Loading...