Serengeti, Mara: Askari wa JWTZ kizimbani kwa kubaka na kumpa mimba Mwanafunzi

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), ambaye ni mshauri wa msaidizi wa mgambo wilayani hapa, Ramadhani Hamisi (46) amefikishwa Mahakama ya wilaya kujibu mashtaka mawili ya kubaka na kumpa mimba mwanafunzi.

Askari huyo mkazi wa Kebanchabancha, alikamatwa Januari 25 na kuwekwa mahabusu baada ya kutajwa na mtoto huyo kuhusika na kitendo hicho kilichomsababishia kukatisha masomo yake.

Juzi, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Ismael Ngaile, Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Renatus Zakeo alidai kuwa Hamisi alitenda makosa hayo Juni, 2018.

Alidai alimbaka mwanafunzi huyo wa kidato cha nne mwenye umri wa miaka 17 aliyekuwa akisoma Sekondari ya Ikorongo mashtaka ambayo mshtakiwa huyo aliyakana yote .

Askari huyo yupo nje kwa dhamana baada ya kukidhi masharti yaliyotolewa na Hakimu Ngaile ya kuwa na wadhamini wawili, mmoja akiwa mtumishi na kila mmoja asaini dhamana ya maneno ya Sh9 milioni na kesi hiyo itatajwa tena Februari 27.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ivi hapo wanatumia kipimo gani ili kujiridhisha km kweli iyo mimba ni yake, au huwa ushahidi tu Wa alietiwa mimba unatosha kumtia mtu hatiani, wajuvi wa sheria tufahamisheni, Kaka Petro E. Mselewa
Mkuu,kwanza nikiri kuwa kati ya kesi ngumu kuzidai,kujitetea au kuzithibitisha ni kesi ya ubakaji. Ushahidi wa kwanza na muhimu in ushahidi wa muathirika ambaye ni huyo mwanafunzi.Ushahidi mwingine ni wa kidaktari,kimazingira na kadhalika. Niliwahi kudokezwa mahali kuwa vipimo vya DNA vyaweza kupima hata mimba. Ni wajibu wa Mpelelezi na Mwendesha Mashtaka kuweka mambo sawa ili kuthibitisha kosa.
 
Aliyetia mimba ni Huyo Ramadhani Hamis. JWTZ halihusiki kwa namna yoyote, usitake kuvuta hisia za watu hapa kwa kuchafua Jeshi letu tukufu.
 
Sawa mwerevu.
Nielimishe basi, laa sivyo utakuwa mjinga kuliko mimi.
Sasa Kaka angu ww ulitaka muandishi aandikaje??? Kuna sehemu amehusisha na jeshi au amesema askari wa jwtz amebaka, kwaiyo Kwani umeambiwa ilo jeshi ni la malaika kuwa wote ni watakatifu ?
Kwan ujawai kusikia Kuna wanajeshi walimuua mjukuu wa Fundikira, na walifungwa, au Yule komando wa jeshi aliemuua rafiki yake temeke Mwaka 2013.....wapo wachache hawana nidhamu si kwamba ni jeshi
 
Hv wabakaji wanaofanya kazi taasisi zingine mbona huwa taasisi hzo hazitajagwi?kwa mfano Richard John mfanyakazi wa TC amembaka bi Grace Michael ?au Juma Rashid mfanyakazi wa NMB ametenda kosa so and so?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliyetia mimba ni Huyo ni Ramadhani Hamis. JWTZ halihusiki kwa namna yoyote, usitake kuvuta hisia za watu hapa kwa kuchafua Jeshi letu tukufu.
Hapo hajalidhalilisha jeshi letu tukufu, Bali amemtanvulisha mtuhumiwa kwetu kuwa yeye anafanya kazi gani na wapi. Hakuna kada yeyote ambayo watumishi wake wote ni malaika watakatifu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hv wabakaji wanaofanya kazi taasisi zingine mbona huwa taasisi hzo hazitajagwi?kwa mfano Richard John mfanyakazi wa TC amembaka bi Grace Michael ?au Juma Rashid mfanyakazi wa NMB ametenda kosa so and so?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wafanye wote hao ila sio mtumishi wa uma hasa jeshini, majishini watu wanatakiwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu, hivyo hata taarifa zake zinagonga vichwa vya habar ikiwa katika mshangao/taharuki kwakuwa haitegemewi kuwa hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliyetia mimba ni Huyo ni Ramadhani Hamis. JWTZ halihusiki kwa namna yoyote, usitake kuvuta hisia za watu hapa kwa kuchafua Jeshi letu tukufu.
Jeshi halijawahi kuwa tukufu. Labda kama hujui maana ya jeshi au msamiati wa tukufu unakupa shida.

Watu wanaofundishana kuua watakuaje watukufu?!??!
 
Huyu alitakiwa apelekwe Mtwara akabangue korosho kwa meno. Mharibifu sana huyu
 
Hapa Mkuu Mimi Niko gizani,je kama ushahidi utajikita kwa mtoto,vipi kama ni chuki za kifamili na mambo mengine,si MTU anaweza kwenda gerezani bila hatia?

Back
Top Bottom