Serengeti: Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu azindua Jeshi jipya nchini

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,939
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan leo katika eneo la zamani la jeshi yaani Fort- Ikoma wilayani Serengeti amezindua jeshi jipya litakalojulikana kama Jeshi la wanyamapori na Misitu nchini.

Akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae kwa mamlaka aliyopewa na katiba kuanzisha vikosi vya majeshi kama ataona inafaa.

Makamu wa Rais amewaonya majangili na magaidi kuacha kujihusisha na vitendo vya uporaji wa rasilimali za Taifa hasa ujangili na utekaji wa watalii maana sasa rasmi jeshi lipo kazini.

Katika hafla ya uzinduzi huo ilihudhuriwa na Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Jenerali Venance Salvatory Mabeyo, Katibu Mkuu Maliasili na Utalii, Waziri wa Maliasili na utalii Dr. Hamis Andrea Kigwangalla pamoja na naibu wake Mh Kanyasu, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mh Adam Malima, Wakuu wote wa wilaya na wakurugenzi wao mkoa Mara, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Dr Allan Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya wanyamapori Dr Wakibara na Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro Dr Freddy Manongi.

Makamu wa Rais amewataka wapiganaji wa vikosi hivyo kulinda maliasili kwa uzalendo mkubwa pia kushirikiana na wananchi katika jukumu hilo.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan leo katika eneo la zamani la jeshi yaani Fort- Ikoma wilayani Serengeti amezindua jeshi jipya litakalojulikana kama Jeshi usu la wanayamapori na Misitu nchini.

Akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae kwa mamlaka aliyopewa na katiba kuanzisha vikosi vya majeshi kama ataona inafaa.

Makamu wa Rais amewaonya majangili na magaidi kuacha kujihusisha na vitendo vya uporaji wa rasilimali za Taifa hasa ujangili na utekaji wa watalii maana sasa rasmi jeshi lipo kazini.

Katika hafla ya uzinduzi huo ilihudhuriwa na Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Jenerali Venance Salvatory Mabeyo, Katibu Mkuu Maliasili na Utalii, Waziri wa Maliasili na utalii Dr. Hamis Andrea Kigwangalla pamoja na naibu wake Mh Kanyasu, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mh Adam Malima, Wakuu wote wa wilaya na wakurugenzi wao mkoa Mara.

Makamu wa Rais amewataka wapiganaji wa vikosi hivyo kulinda maliasili kwa uzalendo mkubwa pia kushirikiana na wananchi katika jukumu hilo.
Kwahiyo kile kikosi cha wanyama pori kimevunjwa?
 
Kilikuwepo kikosi cha wanyamapori, kuanzishwa jeshi la USU kumeongeza nini kwa faida ya tusiojua tofauti?
 
Kukosa kazi za kufanya unajikuta unazindua kitu kile kile ila unabadiri jina na kutegemea matokeo tofauti
 
IMG-20181109-WA0010.jpg
IMG-20181109-WA0010.jpg
IMG-20181117-WA0017.jpg
 
Mimi nilifikiri ameenda kuzindua jeshi la wokovu ili chama chake kiwataje waliompopoa tundu lissu
 
Uzinduzi wa ilo jeshi usu uendane na maboresho makubwa yautendaji kazi ndani ya hiyo wizara.
 
Back
Top Bottom