Serengeti: Katibu CHADEMA apigwa mshale akitoka kwenye kampeni

Mapengo 17

R I P
Mar 28, 2014
1,232
609
attachment.php

Katibu Mwenezi wa CHADEMA Kata ya Rigicha Wilaya ya Serengeti Bahati Mayala


Serengeti. Katibu mwenezi wa Chadema, Kata ya Rigicha wilayani hapa, Bahati Mayala (37) amelazwa katika Hospitali Teule ya Nyerere baada ya kujeruhiwa kwa mshale wakati akitoka kwenye kampeni.

Tukio hilo lililotokea Desemba 5, aa 1:30 jioni katika Kijiji cha Kitembele limethibitishwa na polisi na uongozi wa hospitali hiyo.

Mganga mkuu wa hospitali hiyo, Calvin Mwasha alikiri kupokewa kwa majeruhi akiwa na mshale mgongoni saa 6:00 usiku juzi na kufanyiwa upasuaji kutoa silaha hiyo ya jadi.

Mwasha alisema mshale huo ulikuwa umeingia inchi sita katika eneo la mapafu.

Akizungumza na gazeti hili hospitalini hapo, Mayala alisema alipigwa baada ya kumalizika kwa mkutano wa kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

"Nikiwa njiani katika Kitongoji cha Ngayani ghafla nikasikia kitu kinakita mgongoni...nikaona watu wawili wanakimbia ambao niliwafahamu kwa nguo walizokuwa wamevaa na majina, wote wa Kijiji cha Kitembele. Niliposhika mgongoni nikakuta mshale, nikapiga kelele kuomba msaada," alisema.

Alisema wananchi walikusanyika na kumpeleka kituo cha afya cha Natta, lakini walishindwa na kumpa rufaa kwenda hospitali hiyo.

Kuhusu chanzo cha tukio, alisema ni kutokana na masuala ya kisiasa kwa kuwa siku hiyo kwenye mkutano wao kulitokea vurugu zilizosababishwa na wafuasi wa vyama vingine na wakati anarudi nyumbani akashambuliwa.

Kamanda wa polisi wa Wilaya ya Serengeti, Pius Mboko alikanusha madai ya kuhusisha siasa, akisema Mayala alijeruhiwa na watu wanaodhaniwa kuwa wezi wa ng'ombe.

"Si suala la siasa bali alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wanafuatilia wezi wa mifugo, ndipo akapigwa mshale wakati akiwa na watu wengine," alisema.

"Watuhumiwa hawajakamatwa na tunaendelea kufuatilia," alisema bila kubainisha ni ng'ombe wangapi walikuwa wameibwa na walikuwa ni mali ya nani.

Alisema ng'ombe hao waliibwa katika Kijiji cha Monuna.

Chanzo:Mwananchi
 

Attachments

  • sere.jpg
    sere.jpg
    31.1 KB · Views: 2,414
Stop being general! Sema vurugu zilisababishwa na wafuasi chama cha mapinduzi CCM.

Me huwezi kunilisha maneno ya kuongea, kilichoandikwa ndio hicho na ndio maana hii mada ikaletwa ili ijadiliwe ila usimfundishe binadamu mwenzako kuzungumza kitu cha uongo (Sisi sio Polisi we are the human being like any body) kama unataka useme ni CCM visaidie vyombo vya usalama katika hili.

Asante.
 
tutalipiza kisasi maana hao ni mafisadi wa escrow

Ifahamike tu kuwa,baada ya ccm kukosa mwelekeo( rejea kauli ya Marehemu katibu Mkuu bwana Horace korimba)
Ccm imepoteza mwelekeo,baada ya kuwatukana Think Tank yao ya akina Salm Ahmed Salim,Butiku,joseph Sinde warioba, na timu zote za waona mbali.wariobaki ni enterpreneure!
 
Hii nchi vituko huwa haviishi. Aliyepigwa anasema anadhani kupigwa kwake kunatokana na mambo ya siasa lakini huyo kamanda wa polisi yeye anasema mhusika amepigwa na wezi wa mifugo na kwamba watuhumiwa bado hawajakamatwa!!! Aliyejeruhiwa amesema anawafahamu, ni kwa nini sasa hawajakamatwa? aliyejeruhiwa anasema alikuwa anatoka kwenye mkutano lakini kamanda anasema jamaa alikuwa anafuatilia mifugo iliyoibiwa akiwa na wenzake ndipo akapigwa!! Kuna kitu hakiko sawa hapo na huyo kamanda atakuwa anajua kinachoendelea!
 
alienda kenye kampeni na kundi la ngombe wakati anarudi wakaibwa ndo akafuatilia ila akawazi spidi wevi ndo mana wakampiga mgongoni au niiwekeje?
 
alienda kenye kampeni na kundi la ngombe wakati anarudi wakaibwa ndo akafuatilia ila akawazi spidi wevi ndo mana wakampiga mgongoni au niiwekeje?

Uwongo mwingine inabidi ujipange vinginevyo ndio majibu kama hayo.
 
Nchi hii tuna polisi wa hovyo kabisa na hii inasababishwa na kupachika vyeo polisi pale tu anapokuwa ni mwanaCCM bila kujali elimu na uwezo kama huyu Polisi kwa maelezo haya yanaonyesha jinsi gani alivyo na uwezo mdogo wa kiakili
 
alienda kenye kampeni na kundi la ngombe wakati anarudi wakaibwa ndo akafuatilia ila akawazi spidi wevi ndo mana wakampiga mgongoni au niiwekeje?

Mkuu huna haja ya kuibadili ulivyoiweka imesomeka vyema kabisa,,,, asante sana wajama
 
Back
Top Bottom