Serengeti Boys yatakata, yainyuka India 3-1

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
serengeti.jpg

Timu ya soka ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ leo Mei 17, 2016 imechanua vema baada ya kuilaza India mabao 3-1 katika mchezo wake wa pili wa michuano maalumu ya kimataifa iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka India katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Tilak, Maidan mjini Goa, India.

Mabao ya Serengeti Boys yalifungwa na Maziku Amani katika dakika ya 21 wakati lile la pili India walijifunga baada ya beki wake kuhangaika kuokoa krosi ya Nickson Kibabage katika dakika ya 28 wakati lile la tatu lilifungwa na Asad Juma katika dakika ya 48 huku lile la India likifungwa na Komal Thatal katika dakika ya 38.

Kwa ushindi huo, Serengeti Boys sasa wanasubiri angalau sare au ushindi wa mchezo mmoja kati ya miwili, dhidi ya Korea Kusini utakaopigwa Alhamisi Mei 19, 2016 na Malaysia Mei 21, 2016 ili icheze nusu fainali ya michuano hiyo iliyoanza Mei 12 kabla ya kufikia fainali zake Mei 26, mwaka huu. Katika mchezo wa kwanza, Serengeti Boys ilitoka sare ya Marekani ya bao 1-1.
Katika mchezo huo, Serengeti Boys iliwakilishwa na Ramadhani Kabwili, Ally Nganzi, Ally Msengi, Asad Juma, Dickson Job, Issa Makamba, Maziku Amani, Nickson Kibabage, Shaaban Ada, Syprian Mtesigwa na Mohammed Abdallah.

India: Mohammed Nawaz, Reamsochung Aimol, Boris Singh, Mohammed Khan, Juendra Singh, Suresh Wangjam, Amarjit Kiyam, Khumanthem Meetei, Sandjev Staldi, Aniket Jadhav na Komal Thatal.
 
Nina imani sana na timu hii ya Taifa. Halafu ni vijana wadogo kweli kweli, so uwezekana wa kujifunza ni mkubwa sana

Tatizo je tutawatunza kwa mwendelezo mzuri?
 
Hongera Sana vijana. Kuna tv channel inayoonyesha michuano hii??
 
Hawa vijana wanaanza vyema na mafanikio lakini siasa zikishaanza ni chali...wakirudi bungeni hapo gundu linaanza!!
 
cdc86d1f187cfdb87c80eefd767b1fe2.jpg
Serengeti Boys wameonyesha wanaweza kweli baada ya kuwaonyesha soka wenyeji India kwa kuwachapa mabao 3-1 katika mechi ya michuano ya vijana ya AIFF inayoendelea mjini Goa.

Boys walioonyesha soka safi ndiyo walikuwa wa safi walifanikiwa kupata bao kupitia kwa Maziku Amani katika dakika ya 20.

Maziku tena aliunganisha mpira na kuandika bao la pili katika dakika ya 28 na kuwaduwaza wenyeji.
?
Baadaye India walionekana kuamka na kufanikiwa kupata bao katika dakika ya 36 kupitia Komal Thatal na hadi mapumziko ikawa 2-1.

Kipindi cha pili, vijana hao wa Tanzania ndiyo walionyesha soka bomba zaidi na kufanikiwa kupata bao jingine katika dakika ya 47, mfungaji akiwa Asad Ali.

Baada ya hapo, Boys walionekana kuuchezea zaidi mpira, wakipiga pasi za uhakika na kuwakatisha tamaa kabisa wenyeji hao ambao wana kikosi chao kilichotengenezwa chini ya uangalizi bora kwa zaidi ya miaka mitano.

Chanzo Muungwana Blog
 
tatzo kubwa la tff ni namna ya kuendeleza vipaji, maana hata wale vijana walioshiriki kombe la cocacola la watt wa mitaan kama sikosei, kule brazil wameishia mtaani, lakin sa iv wale vijana wangeendelezwa tusingekuwa na aibu ya kwa tunafungwa 7,

hata hao wakija na ushindi, watashangiliwa tuuu wakibombewa na wamama ili wawatunze mjini mwisho nguvu zinaishia kitandani,

wekeni mopango tff ili muwaendeleze vijana,
 
Kwa Maisha ya Mtanzania na uduni wa afya zetu, nina wasiwasi na kikosi hicho kwenye picha kama kweli ni under 17!! Wengi wao hapo ni above 17.
 
Kiukweli hawa watoto wanatia sana matumaini! Ukosefu wa mipango endelevu ndiyo kikwazo. Utashangaa baada ya miaka michache wamepotelea kusikojulikana na timu ya taifa ikibakia kuwa kichwa cha mwendawazimu.
 
cdc86d1f187cfdb87c80eefd767b1fe2.jpg
Serengeti Boys wameonyesha wanaweza kweli baada ya kuwaonyesha soka wenyeji India kwa kuwachapa mabao 3-1 katika mechi ya michuano ya vijana ya AIFF inayoendelea mjini Goa.

Boys walioonyesha soka safi ndiyo walikuwa wa safi walifanikiwa kupata bao kupitia kwa Maziku Amani katika dakika ya 20.

Maziku tena aliunganisha mpira na kuandika bao la pili katika dakika ya 28 na kuwaduwaza wenyeji.
?
Baadaye India walionekana kuamka na kufanikiwa kupata bao katika dakika ya 36 kupitia Komal Thatal na hadi mapumziko ikawa 2-1.

Kipindi cha pili, vijana hao wa Tanzania ndiyo walionyesha soka bomba zaidi na kufanikiwa kupata bao jingine katika dakika ya 47, mfungaji akiwa Asad Ali.

Baada ya hapo, Boys walionekana kuuchezea zaidi mpira, wakipiga pasi za uhakika na kuwakatisha tamaa kabisa wenyeji hao ambao wana kikosi chao kilichotengenezwa chini ya uangalizi bora kwa zaidi ya miaka mitano.

Chanzo Muungwana Blog

Ni kweli wamecheza vizuri lakini walipoteza nafasi nyingi sana za kufunga hasa kipindi cha pili.
 
Kama una afya duni ni wewe sio watanzania wote.
Acha uongo ww. Hapo karibu 1/2 wako above 17!! Ndio akina Sitti Mtemvu, akina Mrisho Ngassa, nk. Pia historia ya Celebrities wengi wa Tz, Bongo Fleva, Football Players and well educated Profs. comes from families with poor or hard background (improving families). These kids are not exceptional.

Wawaletee mashine ile ya kupima umri kama Wanageria waliokutwa wote wako above. Economically Nigeria is better than Tz, and this reflects the welfare of its citizens. Therefore Health services, health conditions and feeding habits Nigeria>than Tz.
 
Hivi india kisoko ni wangapi vile... Walistahili hata magoli 20 maana kikosi chetu ni bora halafu wahindi na soka wapi na wapi
 
Acha uongo ww. Hapo karibu 1/2 wako above 17!! Ndio akina Sitti Mtemvu, akina Mrisho Ngassa, nk. Pia historia ya Celebrities wengi wa Tz, Bongo Fleva, Football Players and well educated Profs. comes from families with poor or hard background (improving families). These kids are not exceptional.

Wawaletee mashine ile ya kupima umri kama Wanageria waliokutwa wote wako above. Economically Nigeria is better than Tz, and this reflects the welfare of its citizens. Therefore Health services, health conditions and feeding habits Nigeria>than Tz.
Acha kubisha bila kujua ili uonekane mjuaji.

Hawa vijana walipimwa umri kabla ya kwenda India, aliyewapima ni Dr kutoka CAF.

Halafu unavyosema eti wanigeria wanakula vizuri na wana huduma nzuri za afya kuliko watanzania unachekesha.
 
Acha uongo ww. Hapo karibu 1/2 wako above 17!! Ndio akina Sitti Mtemvu, akina Mrisho Ngassa, nk. Pia historia ya Celebrities wengi wa Tz, Bongo Fleva, Football Players and well educated Profs. comes from families with poor or hard background (improving families). These kids are not exceptional.

Wawaletee mashine ile ya kupima umri kama Wanageria waliokutwa wote wako above. Economically Nigeria is better than Tz, and this reflects the welfare of its citizens. Therefore Health services, health conditions and feeding habits Nigeria>than Tz.
Kwa bahati mbaya wewe sio mfatiliaji mpira..kwa taarifa yako hawa madogo wote walienda muhimbili kuchukuliwa vipimo(kipimo cha MRI )kama sijakosea...tatizo bongo ujuaji mwingi.!!
 
Back
Top Bottom