Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17, Seerengeti Boys sasa njia yao ni nyeupe kushiriki michuano ya mataifa ya Afrika kwa vijana (U-17) baada ya mchezaji wa timu ya Congo, Langa Bercy aliyetiliwashaka kuwa umri wake ni mkubwa kushindwa kufika kufanyiwa vipimo vya umri, Magnetic Resonance Imaging (MRI).
Kushindwa kwa Congo kumpeleka mchezaji huyo kwa ajili ya vipimo nchini Gabon ni dhahiri kuwa nafasi yao itachukuliwa na timu ya Tanzania waliokuwa wameondolewa na Congo katika hatua ya kufuzu.
Januari 12 mwaka huu Shirikisho la Soka Afrika (CAF) liliagiza kwa mara nyingine mchezaji huyo afanyiwe vipimo kufuati malalamiko yaliyokuwa ymetolewa na Tanzania kuwa mchezaji huyo aliyefunga goli lililoiondoa Tanzania katika dakika 90+2, alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 17.
CAF ilituma taarifa TFF kuwa isitume wawakilishi kwenda kwenye vipimo Gabon baada ya Congo kushindwa kumpeleka mchezaji huyo ikiwa ni kwa mara ya tatu. Kwa mujibu wa sheria na taratibu za michuano hiyo, Congo Brazzaville hawatoshiriki michuani hiyo.
Alipoulizwa kuhusu jambo hili, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mwesigwa Celestine alisema kwa sasa wanasubiri taarifa rasmi kutoka CAF juu ya hatua inayofuata.
Chanzo: Swahili