SERENGETI: Askari akatwa mkono na Jangili baada ya kumkamata

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,399
Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Mkoani Mara Deus Mwakajegera (35) amekatwa mkono wa kushoto na Jangili baada ya kumkamata akichunga ng'ombe ndani ya hifadhi katika kijiji cha Bisarara.

Inaelezwa kuwa Jangili huyo hufanya pia vitendo vya uwindaji haramu kwenye Hifadhi kwa muda mrefu.

Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Masana Moshana amesema Jangili huyo Zakaria Omahe (54) Mkazi wa Kijiji cha Bisarara baada ya kufanya ukatili huo amekimbia kusikojulikana, Uongozi wa Kijiji unamsaka.

"Ni kweli askari Deus Mwakajegere juzi tarehe Oktoba 23, 2019 alijeruhiwa na Jangili akiwa doria. Hadi sasa bado amelazwa Bugando hospital kwa matibabu Zaidi. Jangili aliyehusika na tukio hilo tunaendelea kumtafuta ili afikishwe mbele ya sheria.," amesema


Chanzo: Nipashe
 
hawa si wanapewa mafunzo na JTWZ wànashindwa nini wakati ushamkàmàta mtu na yupo chini ya ulinzi wako
 
usalama uimarishwee...mwana wa seremalaa!
67171541_10156350511480840_8261469829802754048_n.jpg
 
Hapo kuna walakin, hainiingii akilini askari avunjwe mkono then mvunjaji akimbie na ng'ombe zake! Kwahiyo mvunjaji ni giants kiasi kwamba aliwabeba ng'ombe wake na kukimbia kusikojulikana?
Ushambiwa jangili mkuu

Ova
 
Hizi ni slogan za ajabu kabisa , mchungaji ana mg'ombe wake wanakula nyasi anaitwa jangili? hapana! tena hana mafunzo yoyote still akamdhibiti askari wanyama pori na kuondoka na mkono,
1. mafunzo wanaypata basi bado hayakidhi
2. huyo ni mchunga ng'ombe tu wala si jangili - kwani walikuta amaeua wanyama wangapio hapo?
TAFAKARI
 
Ushambiwa jangili mkuu

Ova


Huyo siyo JANGILI ni MFUGAJI (Mchunga ng'ombe hifadhini)

ETI, JANGILI NA ALIKUWA ANATAFUTWA SIKU NYINGI,

ALIUWA WANYAMA GANI, WANGAPI, LINI NA JE, ALIKAMATWA KISHA AKATOROKA?

WEKENI WAZI

Kwa kauli ya Kamwelwe, hakuna sheria ya kumtia hatiani Mfugaji, hivyo kumbambika UJANGILI AMBAO NI UHUJUMU WA UCHUMI akikamatwa na kuswekwa ndani atasumbuliwa mpaka wenzie wamuonee huruma.
 
Labda niwasaidie wachangiaji wenzangu humu, Ukikutwa hifadhini bila kuwa na kibali chochote kinachokuruhusu kuwa hapo na zaidi ni majira ya usiku haijalishi unachimba madini,unachunga ng'ombe au mbuzi au unawinda nyumbu au tembo unachukuliwa kama jangili. Na hili ni kutokana kwamba hawa wakurya pale Bisalala wanatumia mwanya huo wa kuingia hifhadhini kwa kujiiba na wanakua na mifugo yao na wakifika kule wako na mapanga na tochi na waya ambazo wanaacha mifugo ikiendelea kula na wao wanaweka mitego ya waya kila sehemu yenye njia za wanyama kwa maana hiyo huyo mtu atakamatwa akiwa na mifugo anachunga ila ni jangili kwa maana anafanya mawindo hifadhili kinyume na sheria. Nimpe tu pole rafiki yangu Mwaka hope atapona na kurudi kama awali tucheze mpira SBT pale.
 
Natamani kujua mpk askari unakatwa mkono na adui tena unamhisi ni jangili, Ulikuwa umekumbatiana naye??

Ama mlipambana mpk akakuzidi maarifa na inaonekana hata angeweza kukukata shingo kabisa😕😕
 
Back
Top Bottom