Serengeti: Afa akizungumza na simu iliyokuwa kwenye chaji

Johnny Sins

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
2,538
3,826
Vumilia Kitang'enyi (19), mkazi wa Serengeti amekufa wakati akizungumza na simu aliyokuwa ameichomeka kwenye chaji.

Taarifa zilizolifikia gazeti la Mwananchi zinaeleza kuwa tukio hilo limetokea leo Jumatano Februari 5, 2020, kwamba Vumilia alikutwa amekufa akiwa amepiga magoti huku ameshika simu mkono wa kushoto. Amekutwa na majeraha ya kuungua katika shavu la kushoto.

Mganga mkuu wa hospitali ya Nyerere, Tanu Warioba amethibitisha kifo cha Vumilia lakini hakuwa tayari kueleza suala hilo kwa kina.

Akizungumza na Mwananchi mwenyekiti wa mtaa wa Sedeko eneo la Mugumu Mjini, Charles Chacha amesema Samwel Joseph maarufu Wazo alimkuta Vumilia ambaye ni mkewe akiwa amepiga magoti huku mkononi akiwa ameshika simu.

Amesema simu hiyo ilikuwa katika chaji na alipomchunguza alibaini amebabuka katika shavu lake la kushoto.

"Soketi aliyochomeka chaji inaonekana ilikuwa mbovu, naye kwa kuwa alikuwa anafua alikuwa na majimaji na katika sakafu kulikuwa na unyevunyevu kutokana na mvua zinazonyesha, inawezekana ni chanzo cha kifo chake," amesema Chacha.

Mwenyekiti huyo wa Serikali ya mtaa amesema mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) walifika katika nyumba hiyo na kufanya ukaguzi ambapo walibaini mfumo wa umeme katika nyumba hiyo una shida.

Byabato Wenchislaus, shuhuda wa tukio hilo amesema ,” mumewe aliporudi alimkuta Vumilia ameanguka huku mkononi akiwa na simu ameing’ang’ania. Awali alidhani amepiga magoti na alipomtazama alibaini amekufa, alianza kupiga kelele ndio tukajitokeza kumsaidia.”

Amesema watu ambao Vumilia aliwaacha nje wakati akiingia ndani, walishangaa walipopata taarifa za kifo chake kwa kuwa hawakusikia hata akipiga kelele kuomba msaada.

Chanzo: Mwananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiko kifo inaonekana kina utata,
Hio shoti na yenyewe pia ni utata,
Hao tanesco nao majibu pia yana utata,
Daktari ameshindwa kuelezea sababu ya kifo kutokana na utata,

Maendeleo hayana chama
 
mmmh aisee, yaani na mimi ni jana usiku nilikuwa naongea na mtu simu iko kwenye umeme....simu ilikuwa 1% ila nilichukua tahadhari kidogo, niliweka earphone na nikaiziba simu kidogo na nguo... nikawa naigusa chaja au simu kuangalia kama zimepata moto zisije zikanilipukia bureee..(mfumo wa umeme kwangu upo salama)

wataalamu hii imekaaje?
 
Nikuulize ,wewe Ni mfuasi wa mwaipopo?
 
simu ni hatari sana ikiwa kwenye chaji.
Sasa unapotaka kuongea na mtu wakati ipo kwenye chaji ni kuyakaribia mauti.
nakumbuka siku moja nilikuwa na simu ya jm. huawei sasa betri likafa. Nikalitoa betri nikaanza kulifungua na msumali. Bwana weee ule msumali ukakutana na carbon.
Nikasikia paaa.nilikuwa nimekaa kwenye kiti.
Lakini nilijikuta nipo chini . betri limewaka motoo.
Na ilibaki kidogo niungue mikono.ila nikaungua vinyweleo tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mmmh aisee, yaani na mimi ni jana usiku nilikuwa naongea na mtu simu iko kwenye umeme....simu ilikuwa 1% ila nilichukua tahadhari kidogo, niliweka earphone na nikaiziba simu kidogo na nguo... nikawa naigusa chaja au simu kuangalia kama zimepata moto zisije zikanilipukia bureee..(mfumo wa umeme kwangu upo salama)

wataalamu hii imekaaje?
Usirudie kufanya huo ujinga tena. Usizungumze na simu chaji ikiwa asilimia 20 kwenda chini..unless weka loudspeaker.
 
mmmh aisee, yaani na mimi ni jana usiku nilikuwa naongea na mtu simu iko kwenye umeme....simu ilikuwa 1% ila nilichukua tahadhari kidogo, niliweka earphone na nikaiziba simu kidogo na nguo... nikawa naigusa chaja au simu kuangalia kama zimepata moto zisije zikanilipukia bureee..(mfumo wa umeme kwangu upo salama)

wataalamu hii imekaaje?
Mbaya sana hii, kidgo ungeweka loud speaker alafu unakaa mita kadhaa kutoka ilipo simu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom