Serengeti: Adaiwa kumuua mumewe siku 14 baada ya kufunga ndoa, kisa si chaguo lake

Hapo alipomaliza kuua akaenda kucheki msosi kwa mama mkwe na kuendelea kula kama vile nothing happened ndio amenishangaza ukizingatia kuwa ni wa kike.

Ila bora mshikaji amekufa baada ya kupiga show.

Anyway, marehemu apumzike kwa amani na binti akapumzike jela.
mkuu, huyo tayari zilishamruka. awahishwe hospital tu
 
Happy Nyasumo (18) mkazi wa Wilaya ya Serengeti amemuua mumewe, Bebe Mbogo (26) kwa madai kuwa hampendi na hakuwa chaguo lake zikiwa zimepita siku 14 tangu walipofunga ndoa.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Alhamisi Aprili 14, 2021 mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu amesema tukio hilo limetokea jana Aprili 14, 2021 saa 4 usiku katika kitongoji cha Pengo kijiji cha Iseresere.

Amesema chanzo ni mgogoro wa ndoa na mtuhumiwa anashikiliwa na polisi kwa hatua zaidi.

Diwani wa Majimoto, Johannes Masirori ambaye ni mjomba wa marehemu amesema Mbogo na Happy walifunga ndoa Machi 31, 2021 na kudai kuwa mwanamke huyo amekiri kufanya mauaji hayo.

"Kabla ya mauaji anadai kuwa mumewe alimlazimisha kufanya tendo la ndoa na baada ya kumaliza mwanaume alilala na yeye alipobaini amesinzia akachukua panga na kumkata mara tatu shingoni,” amesema.

Amesema baada ya kufanya kitendo hicho Happy alikwenda kwenye nyumba ya mkwewe na kuchukua chakula na kuanza kula.
She is lunatic masikini!
 
Bado ni mdogo Sana kumlazimisha ndoa!
Angekuwa kapevuka akili angelikimbia ...lakini akili mdogo haikuwaza Hilo ..Na ndio maana hajali maana...bado ni mdogo!
Wakimtendea Haki ..hatanyongwa Wala kufungwa maisha!

Wazazi wa pande zote wamekula hasara!

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
 
Toto jinga sana hilo, ila wilaya za Tarime na Serengeti hayo matukio ni kawaida kabisa kama biashara ya nyeti za kiume China.
Oooh...!? Nyeti za kiume zinatakiwa china eeeh?. Kama ninazo mboro mbili si nikawauzie moja
 
Serengeti. Happy Nyasumo (18) mkazi wa Wilaya ya Serengeti amemuua mumewe, Bebe Mbogo (26) kwa madai kuwa hampendi na hakuwa chaguo lake zikiwa zimepita siku 14 tangu walipofunga ndoa.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Alhamisi Aprili 14, 2021 mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu amesema tukio hilo limetokea jana Aprili 14, 2021 saa 4 usiku katika kitongoji cha Pengo kijiji cha Iseresere.

Amesema chanzo ni mgogoro wa ndoa na mtuhumiwa anashikiliwa na polisi kwa hatua zaidi.

Diwani wa Majimoto, Johannes Masirori ambaye ni mjomba wa marehemu amesema Mbogo na Happy walifunga ndoa Machi 31, 2021 na kudai kuwa mwanamke huyo amekiri kufanya mauaji hayo.

"Kabla ya mauaji anadai kuwa mumewe alimlazimisha kufanya tendo la ndoa na baada ya kumaliza mwanaume alilala na yeye alipobaini amesinzia akachukua panga na kumkata mara tatu shingoni,” amesema.

Amesema baada ya kufanya kitendo hicho Happy alikwenda kwenye nyumba ya mkwewe na kuchukua chakula na kuanza kula.

"Ameulizwa na kusema bila hofu na kuwaonyesha panga alilokuwa ameficha..., tangu wamefunga ndoa wamekuwa katika mgogoro mkubwa. Happy alirudi kwao kwa madai kuwa hamtaki mumewe lakini huko kwao wakamlazimisha arudi kwa mumewe kwa maelezo kuwa hawawezi kurudisha ng'ombe waliochukua wakati wakimuozesha," amesema.

Masirori amesema wakati watu wakilia na kusikitika kutokana na tukio hilo, mtuhumiwa hakuwa na wasiwasi na aliwataka wasiojua wamtazame vizuri.

MWANANCHI
Ndio ndoa hizo. Mtu anawaambia kabisa hampendi huyo mtu au anawaambia kabisa napigwa sana na kuteswa,bado wazazi mnang'ang'aniza tu nenda tu kwa mumeo ndio ndoa zilivyo,na sisi tuliishi hivyo. Binti ameamua kukatisha sasa,alikuwa hana namna nyingine
 
Back
Top Bottom