Serengeti: Adaiwa kumuua mumewe siku 14 baada ya kufunga ndoa, kisa si chaguo lake

Happy Nyasumo (18) mkazi wa Wilaya ya Serengeti amemuua mumewe, Bebe Mbogo (26) kwa madai kuwa hampendi na hakuwa chaguo lake zikiwa zimepita siku 14 tangu walipofunga ndoa.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Alhamisi Aprili 14, 2021 mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu amesema tukio hilo limetokea jana Aprili 14, 2021 saa 4 usiku katika kitongoji cha Pengo kijiji cha Iseresere.

Amesema chanzo ni mgogoro wa ndoa na mtuhumiwa anashikiliwa na polisi kwa hatua zaidi.

Diwani wa Majimoto, Johannes Masirori ambaye ni mjomba wa marehemu amesema Mbogo na Happy walifunga ndoa Machi 31, 2021 na kudai kuwa mwanamke huyo amekiri kufanya mauaji hayo.

"Kabla ya mauaji anadai kuwa mumewe alimlazimisha kufanya tendo la ndoa na baada ya kumaliza mwanaume alilala na yeye alipobaini amesinzia akachukua panga na kumkata mara tatu shingoni,” amesema.

Amesema baada ya kufanya kitendo hicho Happy alikwenda kwenye nyumba ya mkwewe na kuchukua chakula na kuanza kula.
Mambo ya kuongea na wakwe badala ya kukubaliana kwanza na mtu wako haya. Jamaa kakojoa akauchapa usingizi wa moja kwa moja.
 
Doh...kumbe kule kulala lala baada ya kupiga kimoja sio kuzuli lolote linaweza kukutokea.
 
ndo maana dada hakuona shida kumgecha na panga halafu akatafuta na msosi wa kushushia. Probably she endured so much from her abuser. Men stop abusing women, mwanamke akiamua kufanya ukatili dunia huwa inasimama kwanza kusikilizia.
Unatumia kinywaji gani nikuchek kidg!
 
Sasa chief cha mwisho utakijua ni kipi? Au ukijihisi kuchoka choka?
Haswaaa ukiona umechoka inatakiwa ukeshe macho😂, na pia ni vyema tuwafikishe juu kabisa ya mlima kilimanjaro ili hata akitaka kukuua akakumbuka raha uliyompa anakusamehe
tumeitishq kikao cha dharula kama walichofanya SADC kujadili hali ya amani huko kanda ya ziwa hasa wanaume waishio Tarime, Rorya, Nyamongo na Mugumu wapo hatarini kutoweka
 
Babe tukichomwa mikaa sisi hamsemi .tukiua mnakuja duh😑! Nimekumis nikajiapiza na kujinuiza sitakutafta tena na ole wako nikifa usije nizika😶! Ila waha mna maringo jamani 😡😡😡..mngepata ziwa victoria kubwa kama kwetu si tungekufa jamani😆
Nimeelewa maumivu mnayopitia darling. Mfumo dume ni shida. Huyo binti hata asingeua angebaki anakufa yeye ndani kwa ndani. Asingefurahi ndoa wala tendo. Maisha kwa ujumla.

Nimekumiss zaidi mtoto mtam. Nilijua tu umenikasirikia nikaona nikuache kidogo coz hata ningejieleza usingenielewa. Usijiapize nkoi.

Hahaaa nimecheka sana...eti ziwa Victoria.
 
Nimeelewa maumivu mnayopitia darling. Mfumo dume ni shida. Huyo binti hata asingeua angebaki anakufa yeye ndani kwa ndani. Asingefurahi ndoa wala tendo. Maisha kwa ujumla.

Nimekumiss zaidi mtoto mtam. Nilijua tu umenikasirikia nikaona nikuache kidogo coz hata ningejieleza usingenielewa. Usijiapize nkoi.

Hahaaa nimecheka sana...eti ziwa Victoria.
Acha tu aue mambo mengine yasonge ...nimecheka na comment yako🤣
 
Back
Top Bottom