Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,685
- 119,325
Wanabodi,
Niko hapa hoteli ya Serena kwenye garden yao huku nyuma karibu na pool, niko na jamaa zangu na mgeni wangu kafikia hapa. Meza ya jirani yangu kuna wazungu nao wamekaa wanapata vinywaji.
Wenzangu wazungu wako na kamera zao wanapiga picha kwenye mandhari ya Serena, kiukweli huku kwa nyuma wana garden nzuri, yenye mandhari nzuri sana!.
Kuona hivyo na mgeni wangu si na yeye akataka picha, nikatoa kamera na mimi nimtwange picha, mara ghafla akaja mlinzi wa KK Security na Meneja fulani sio ndio meneja ulinzi, akatuzuia kupiga picha!, eti watu hawaruhusiwi kupiga picha bila kibali!.
Nikamuonyesha wale wazungu nikasema mbona wale wamepiga picha bila kuulizwa chochote au kuzuiwa, kwa nini sisi tuzuiwe?!.
Jamaa akajibu, hao wazungu ni wageni wetu!, Mwenyeji wangu mswahili akasema hata mimi ni mgeni hapa!. Jamaa kauliza number ya chumba, kaonyeshwa, akasema basi lazima mgeni huyo atoe taarifa kwa uongozi kuwa anataka kupiga picha kwenye mandhari ya Serena!, Ati watu wanaruhusiwa kupiga picha mandhari ya Serena ni wageni wao wazungu tuu!, na waswahili labda wakiwa ni maharusi tuu!.
Wajameni huu sio ubaguzi wa rangi mbaya kabisa wa racial discrimination ndani ya nchi yetu!, kibaya zaidi ubaguzi huu unafanywa na waswahili wenzetu, ile kuajiriwa Serena, wamegeuka vibaraka kuwaona wazungu ndio bora wanaostahili kuchukua picha lakini sisi Waswahili inakuwa nongwa!.
Kama ubaguzi wenyewe ndio huu kwa sisi wageni tuu, hao wafanyakazi Waswahili watakuwa na hali gani humo ndani?.
Jee tuwashitaki hawa jamaa kwa Magufuli awatimulie mbali, huwezi kuja nchi ya watu, hata kama ndio kwa kisingizio cha uwekezaji, uwekezaji gani huu wa kuwabagua wageni kwa rangi zao?!.
NB. Kunatokeaga mbwa wa mzungu kuwa mkali hata kuliko mwenye mbwa!, isije ikawa hawa wafanyakazi Waswahili ni vijibwa tuu vya mzungu, na huo ubaguzi sio sera ya uongozi wa Serena bali wao katika kujiona bora zaidi na kujikombakomba, ndio walioinitiate huo ubaguzi ili kujionyesha tuu wao ni watu muhimu, mzungu ndio apige picha freely, Mswahili lazima uombe kibali!, na wote ni wageni wenye hadhi sawa!.
Nashauri hii Serena imulikwe, ikithibitika ni kweli kuna ubaguzi, hili nalo ni jipu, linahitaji kutumbuliwa!.
Kiukweli nilikasirika, na mgeni wangu amekasirika atauona uongozi kupeleka malalamiko yake ya kubaguliwa!.
Say no to any form of discrimination!.
Pasco
Pasco
======
UPDATE:
======
Nimepokea ufafanuzi rasmi kutoka Uongozi wa Serena, kumbe kuna mwana jf pale Serena, amenishukia in box na kunifafanulia, kuwa kupiga picha madhari ya Serena kwa kutumia kamera ndogo au simu, inaruhusiwa ila mradi usiingilie uhuru wa wegeni wengine kutokea kwenye picha yako.
Lakini professional photographs zozote, lazima mtu upate kibali rasmi kutoka uongozi wa Serena.
Watu wenye functions zao pale, huwa wanapewa vibali vya kupiga picha pale.
Hivyo huyu mgeni wangu alipaswa kumuarifu duty manager kuwa kuna mgeni wangu atakuja na professional team to take profession shots.
Naomba radhi sana kwa uongozi wa Serena kukwerwa na tuhuma za ubaguzi!, ila kiukweli hao wazungu pia walikuwa na professional camera with a stand ila inawezekana wenzangu walikuwa na vibali!.
Ujio wa kamera za 4K zitapunguza haya mauza uza kama haya, maana kikamera ni kidogo tuu kama cha picha za facebook na insta lakini ni very professional. hatutasumbuana sumbuana hivi.
Mode unaweza sio tuu kuufunga huu uzi, bali kuupotezea jumla tusije tukaathiri biashara yetu ya utalii pale Serena kwa kuchafua jina la Hoteli yetu ya Serena iliyojengwa kwenye kiwanja cha wazi cha Gymkana!.
Mimi mwenyewe nilipooa, harusi yangu nimeifanyia hapo Serena enzi hizo ikiitwa Sheraton, kazi yao kubadili tuu majina kila baada ya kipindi cha tax holiday kumalizika!.
Asanteni na poleni kwa usumbufu uliojotokeza.

Mkuu Asprin, asante kumtag huyu Mkuu Mtambuzi, jamaa aliotuzuia kupiga picha ni hadi name tag yake nimeisoma, ukilihitaji jina nitakupatia kwa uchunguzi wa ndani!.