Serekali yakacha taarifa kuhusu mgomo wa madaktari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serekali yakacha taarifa kuhusu mgomo wa madaktari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kurunzi, Jun 28, 2012.

 1. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 326
  Trophy Points: 180
  Kwa mujibu wa spika serkali haitatoa taarifa yake leo kama ilivyotangazwa hapo jana, Akitoa sababu Spika Makinda amesema ni kutokana na Mhimili wa mahakama kulalamika unaingiliwa katka majukumu yake, Kwani suala hilo lipo mahakamani.
   
 2. Y

  Yarrot Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 79
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Kwani walikuwa hawajui hilo? Ama ni ule ujinga wa viongozi wetu? My poor Tanzania!
   
 3. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Is't Mizengo Pinda supposed to be a lawyer? Does't he know the separation of powers between the judiciary , the executive and the legislature? Angalia hawa vilaza wa magamba hamna wanalojua ; aibu tupu!!
   
 4. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Taarifa za uhakika kutoka mjengoni Dodoma ni kwamba Serikali yetu iliyo dhaifu imeshindwa kutoa tamko kama ilivyoahidi jana kupitia PM wake Bwana Mizengo Kayanza Pinda kwa kisingizio kuwa hilo swala kwa sasa liko Mahakamani! Kichekesho ni kwamba huu mgomo unaingia wiki ya pili sasa na hili swala inajulikana liko Mahakamani na PM Pinda wakati anaisemea serikali jana Bungeni kuwa itatoa tamko alikuwa anajua hili! Huu ndio udhaifu tunaozungumzia kila siku kuwa kwa sasa Tanzania hatuna Serikali maana viongozi wote ni wadhaifu na hawana maamuzi. Kila siku wanaishia kuweweseka na kutoa kauli zenye kuzua utata mtupu.

  Hakika kwa hili Serikali ya Chama Cha Magamba-CCM imedhihirisha udhaifu wake kupitia Waziri wake Mkuu Pinda. Hii si yo mara ya kwanza kwa Pinda kutoa kauli zenye kutia shaka. Huu ni UDHAIFU mkubwa sana alio nao Mizengo Kayanza Pinda kiasi cha kumfanya aonekane ni PM asiye na maamuzi hata kidogo.Kuna mifano chungu nzima inayoonyesha weakness za Pinda tangu wakti ule aalipokwenda Kanda ya Ziwa kushughulikia MAUAJI YA MA-ALBINO. Pinda bila ya aibu alilia mbele ya wananchi ati kuonyesha uchungu kwa vifo vya albino! Huu ni udhaifu. Mwanamme mzima utaliaje mbele ya wanaume wenzako achilia mbali wanawake na watoto walokuwa kwenye mkutano ule.UDHAIFU. Kuna swala la Katibu wa Nishati na Madini ambalo Pinda alijifaragua kuwa angelimfukuza siku ileile na haikuwa hivyo. Kuna swala la mgomo wa Madaktari ambalo hakika linamwelemea tangu lilipoanza kwa kudai ati Dr. Ulimboka hakuwa Daktari maana alifukuzwa Chuo,baadaye ilikuja onekana alichosema ilikuwa ni uzushi.

  Sasa hili la jana mzee mzima tena kachemka.Je,wakti anasema atatoa tamko alikuwa kasahau kuwa hilo swala liko Mahakama?UDHAIFU mtupu. Hata hivyo kwa Great Thinkers tunaweza kusoma katika ya mistari kwamba: Kitendo cha KUTEKWA KWA DR.ULIMBOKA STEVEN NA MIKAKAKATI YA KUTAKA KUMNYAMAZISHA KWA KIFO limetikisa nchi nzima kwa kila Mtanzania na hasa Madaktari na wapenda amani wa nchi hii. Kulingana na taarifa za tukio zima hawa WATEKAJI WALIDHAMIRIA KUTOA ROHO YAKE KABISA. Lakini kwa vile Mungu siku zote yuko upande wa HAKI alimnusuru Dr. Ulimboka ili hatimaye aweze kuwataja hao wabaya wake ambao tuna hakika anawajua na kuna maneno waliyokuwa wanayatamka wakati wakimsulubisha. Kwa hiyo kila kitu kitawekwa wazi muda si mrefu. Kwa mtu mwenye akili timamu akiunganisha MANENO YA PINDA KUWA LIWALO NA LIWE ANAPOUNGANISHA NA KUTEKWA KWA DR.ULIMBOKA LAZIMA HAPA KUNA MKONO WA SERIKALI KWA ASILIMIA 99.9999%. Serikali kama kawaida yao watajaribu kupotosha ukweli huu lakini wajue kuwa Watanzania si wajinga kihivyo. Time will tell!

  Kama CCM walikuwa wanajidanganya kuwa kumnyamzisha Dr.Ulimboka kwa kifo itazuia mgomo wa madkatari basi ni UDHAIFU mkubwa na UVUVI wa kufikiri. Ni serikali za MADIKTETA TU NDIYO WANAOWEZA KUFANYA VITUKO KAMA HIVI. KWA HAPA TULIPOFIKIA SASA CCM NI UTAWALA WA KIDIKTETA KWA ASILIMIA 100!Maana kiukweli hili litakuwa limewatia CCM DOA na kwa maana nyingine wamezidi KUJICHIMBIA KABURI LAO HUKU WAKILIPAMBA KWA MARUMARU TAYARI KWA MAZISHI YAO KATI YA SASA NA 2015. We are waiting for that great Day. The DEATH OF CCM.

  Nawasilisha.
   
 5. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  The government has no think tank
   
 6. mkandaboy

  mkandaboy JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 237
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  WEAK President, WEAK prime minister, WEAK govt, WEAK judiciary system...
   
 7. silvemaps

  silvemaps Member

  #7
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 26, 2012
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ukombozi wa kuitoa nchi mikononi wa mafisadi/mafarao unakaribia ,VIA TANZANIA,CCM itakufa kifo cha aibu na haitarudi tena madarakani,HAKUNA CHAMA KILICHOLETEA NCHI UHURU KILICHOFANIKIWA KUIONDOLEA NCHI UMASKINI
   
 8. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,648
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Walivyo kimbilia mahakamani hawakulijua hili,wababaishaji wakubwa.
   
 9. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,489
  Likes Received: 5,579
  Trophy Points: 280
  Wanasubiri upepo upite! Shame!
   
 10. silvemaps

  silvemaps Member

  #10
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 26, 2012
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Viva tanzania,viva forever ,madaktari hakuna kulala mpaka kieleweke.mnatakiwa kurizaini wote ili serekali ijue mbunge na dactari muhimu ni daktari.haki sawa kwa wote.
   
 11. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #11
  Jun 28, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,638
  Likes Received: 1,427
  Trophy Points: 280
  Wabunge wa CCM wana kikao mchana huu.. tusitegemee chochote

  Bussiness as usual.. wacha wananchi wapate tabu ili 2015 wasirudie makosa
   
 12. Captain22

  Captain22 JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  The went to the court knowing that they have a control over the decision of the court. Our judiciary system is weak over the executives. The corrupt executive is being protected by the weak, dependant judiciary.
   
 13. N

  Nambombe Senior Member

  #13
  Jun 28, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 161
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Another silly season!!!
   
 14. S

  Sessy Senior Member

  #14
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  shame on you pinda na serikali yako yote umeonesha udhaifu mkubwa sana hivi ana elimu gani huyu mtu jamani....
   
 15. Wachovu

  Wachovu JF-Expert Member

  #15
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 1,197
  Likes Received: 388
  Trophy Points: 180
  Kwani dR Ulimboka ndiye anatoa maamuzi kwa niaba ya madaktari. Jamani CCM msimuue bure mtoto wa watu. Madaktari ni watu wazima wana akili zao sio kwamba kupinga uonevu ni shawishi la Dr Ulimboka . Nawasifu sana vijana wa Tanzania kwa kuchua hatua na wala msirudi nyuma hata kwa vitisho na mauaji , afadhari kufa ukiwa na msimamo wako kuliko kuishi na kutawaliwa na mfumo hovyo , akili ndogo na ndio maana nchi hii na utajiri wa kupindukia lakini imebaki maskini wa kutupwa , angalia magamba yalivyo ovyo yanalimbikiza mihela kibao nchi za nje . Tafakari na Chukua hatua . Madokta tupo nyuma yenu
   
 16. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #16
  Jun 28, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,198
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Hapa ndipo wanapotuthibitishia kuwa serikali inahusika na jaribio la mauaji juu ya dr. Ulimboka.
  Ni hivi, jana asubuhi wakati pinda anasema leo atatoa tamko la serikali juu ya mgomo NA LIWALO NA LIWE, alikuwa anajua vijana wao wameshamaliza kazi ya kumuua Ulimboka, hivyo leo angedanganya mambo kibao kuwa walikubaliana n ulimboka (wakijua marehemu hasemi) na watanzania tuwaone wamefanya kitu.
  Pinda alijua kuwa kesi ipo mahakamani na kuwa hakutakiwa kuiongelea bungeni, sema ndo vile Mungu kawaumbua.
  Ccm kumbuka siku ya kufa nyani miti yote hutereza, Naichukia hii serikali DHAIFU na wauaji
   
 17. pepe17

  pepe17 JF-Expert Member

  #17
  Jun 28, 2012
  Joined: Oct 17, 2007
  Messages: 276
  Likes Received: 191
  Trophy Points: 60
  Serikali imechemsha,Waziri mkuu kachemka, hivi nchi ya Tanzania haina RAISI, akasimama na kutoa maelezo na ufafanuzi wa suala hili?
  AIBU TUPU!!!
   
 18. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #18
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,997
  Likes Received: 2,653
  Trophy Points: 280
  CCM imenichosha sana na mambo yake ya kipuuzi,natama tuizike hata saa hizi pumbavu sana.
   
 19. K

  KISUKALI Member

  #19
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 28, 2010
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Cha kushangaza wao wapo cc tunapiga soga: So Who's WEAK...............??
   
 20. m

  moma2k JF-Expert Member

  #20
  Jun 28, 2012
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 953
  Likes Received: 984
  Trophy Points: 180
  Nilishasema toka siku nyingi ya kwamba: Mizengo Pinda ni DHAIFU, afadhari ya Lowassa. Pinda ni mzigo kwa J.Kikwete raisi wetu. J.Kikwete sasa anatakiwa kufanya kazi za waziri mkuu, wakati waziri mkuu huyo yupo na analipwa mshahara.
  OMBI: J.Kikkwete anatakiwa kuvunja baraza la waziri ili amuondoe Pinda. Pinda ni mzigo kwa mustakabali wa nchi hii.
  Pili, sielewi ajenda ya akina Zitto ya kutokuwa na imani na waziri mkuu ilifia wapi? Au Zitto naye ni msanii wa kuleta ajenda za kisanii? Au Zitto anataka umaarufu tuu kama mtoto mdogo? Tunaomba utetezi toka kwa Zitto mwenye!
   
Loading...