Serekali ya zanzibar kuanzisha mamlaka kusimamia mafuta yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serekali ya zanzibar kuanzisha mamlaka kusimamia mafuta yake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kakke, Aug 26, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1][​IMG][/h]Written by Ashakh (Kiongozi) // 14/07/2012 // Habari // 4 Comments


  13 July 2012
  Rushyd Ahmed
  SERIKALI ya Zanzibar inakusudia kuanzisha Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji. Waziri wa Maji, Ardhi, Makazi na Nishati, Ramadhani Abdallah Shaaban, ameliambia Baraza la Wawakilishi.
  Waziri alitoa kauli hiyo wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2012/13 katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kin…achoendelea Chukwani, Zanzibar.
  Alisema tayari mataarisho ya Sheria ya kuanzisha Chombo hicho yameanza, sambamba na Sheria za kusimamia na kusambaza nishati ya mafuta na Petrol ya Zanzibar.
  “Mheshimiwa Spika kwa ajili ya kutekeleza sera ya Nishati Zanzibar, Wizara inaendelea kujiandaa pamoja na kuwapatia mafunzo wafanyakazi katika sekta ya nishati na mafuta,” alisema Waziri Shabaan.
  Alisema juhudi za kuwapatia mafunzo wafanyakazi wa Wizara hiyo zinalenga kukabiliana na upungufu wa wataalumu wa fani ya nishati ikiwemo kutafuta na kuchimba mafuta katika Visiwa vya Zanzibar.
  Aidha, alisema Wizara yake kwa kushirikiana na Serikali ya Norway inafanya mpango wa kufanya semina na kongamano kwa lengo la kutoa taaluma kuhusu athari za kimazingira zinazotokana na kutafuta na kuchimba mafuta Zanzibar.
  Kuhusu tathmini ya kimazingira inayotokana na mwelekeo wa kutafuta na kuchimba Mafuta na Gesi asilia, Waziri alisema Wananchi katika Visiwa hivyo wamekuwa na matumaini makubwa ya kuwepo kwa nishati hizo.
  Waziri Shabaan, alisema katika mwaka wa fedha unaoanza, Wizara yake pia imepanga malengo ya kuendelea na juhudi za kuwapatia wananchi wa Zanzibar elimu juu ya matumizi ya nishati..
   
 2. F

  FUSO JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  washagundua wabara ni kikwazo, na sasa mtaenda zenji kwa vitambulisho maalum.
   
 3. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  napita tu, maana hili si la muungano. kila la heri
   
 4. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,582
  Likes Received: 1,675
  Trophy Points: 280
  Jambo la heri
   
 5. steveachi

  steveachi JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 4,128
  Likes Received: 1,726
  Trophy Points: 280
  kheri tu
   
Loading...