Serekali ya Suk uchumi umekuwa %7.6 jee tukiwa na Z,bar huru uchumi utakuwa % ngapi?. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serekali ya Suk uchumi umekuwa %7.6 jee tukiwa na Z,bar huru uchumi utakuwa % ngapi?.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Oct 9, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [​IMG]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]Uchumi wa Zanzibar kukua kwa asilimia 7.5


  na Nasra Abdallah, Zanzibar


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]KATIKA mwaka huu wa fedha, 2012/2013, uchumi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar unatarajiwa kukua na kufikia asilimia 7.5 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 0.7 kulinganisha na mwaka jana.
  Hayo yalisemwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, wakati wa mkutano wake na wahandishi wa habari, ikiwa ni utaratibu wake wa kukutana nao kila baada ya miezi mitatu kwa ajili ya kuzungumzia utendaji wa serikali, mkutano uliofanyika Hoteli ya Grand Palace, Malindi mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki.
  Maalim Seif alisema jambo hilo wana imani watafanikiwa kutokana na namna walivyojipanga ambapo kwa mwaka 2011uchumi uliweza kukua kwa asilimia 6.8.
  Vilevile alidai kwamba pato la Mzanzibari limekua kutoka sh 782,000 kwa mwaka hadi kufikia sh 960,000 ambazo ni sawa na dola za Marekani 615 kutoka dola 560 kwa mwaka 2010.
  Hata hivyo kiongozi huyo alisema kwamba kwa vyovyote vile bila kuwepo hali ya amani na utulivu na maelewano, serikali isingeweza kujenga imani kwa wawekezaji na vitegauchumi ambavyo hadi sasa wanaendelea kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono kwa kuwekeza miradi yao.
  Pia alikiri kwamba bado wanayo kazi nzito mbele yao ya kuzidisha bidii kwa kila mmoja kuiunga serikali mkono katika kuhakikisha inaendelea kubaki katika hali ya amani na utulivu na kusaidia kukuza kasi ya kuimarika uchumi.
  Kwa upande wa sekta ya kilimo, alisema kwamba biashara na huduma zimeendelea kupewa msukumo mkubwa na kuendelea kuchangia kwa kiasi kikubwa uchumi na mapato ya wananchi.
  “Kwa mfano katika huduma, utalii umeendelea kutoa mchango wa kipekee katika uchumi wa Zanzibar ambapo sekta hiyo imeweza kuchangia asilimia 80 ya fedha za kigeni na asilimia 70 ya wananchi wanafaidika katika sekta hii.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
Loading...