Serekali ya SUK itatuwe utata huu ambao umeukaribisha wenyewe kuwepo Z'bar. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serekali ya SUK itatuwe utata huu ambao umeukaribisha wenyewe kuwepo Z'bar.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Jul 23, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=1]Waliopewa viwaja vya kupima(Plan) na Serekali na wakajenga,haliyakuwa yalikuwa ni mashamba ya watu kabla ya mapinduzi,Jee Serekali ya SUK itashukuwa hatua gani?.[/h]Written by Hassan10 // 23/07/2011 // Habari // No comments

  Kabla ya Serekali ya Umoja wa Kitaifa GNU kuingia madarakani Maalim Seif Shariff aliuzizwa jee suala la mashamba yawatu yalio yanganjwa kabla ya Mapinduzi ya 64 na Serekali ikagawa maeneo ambayo hivi sasa imekuwa miji mashamba hayo vipi watarudishiwa wenyewe au Serekali itachukuwa hatua gani kulitatua tatizo hili?.
  Maalim Seif alisema Serekali ijayo haito myanganya mtu Nyumba alokwisha jenga na kurudisha Shamba lakini itawalipa fidia wenyewe au kuwadengea maeneo yakuwapa.
  Sasa jee Serekali ya Umoja wa Kitaifa ikiongozwa na Ccm na Cuf akiwa Maalim Seif ni Makamo wakwanza wa Rais imefanya hivyo?, maana hivi sasa kuna kesi nyingi zimerundikana bila Serekali kutowa jawabu nihatua gani imeshukuwa kuondosha utata huu ulopo zidi ya jamii.
  Jee Serekali ya Umoja wa Kitaifa GNU inayongozwa na Chama cha Ccm na Cuf kweli imetimiza kauli yao, ambayo alitowa Maalim Seif Shariff kabla ya kunda Serekali hio ya Kitaifa.
  Hivi sasa kuna kesi nyingi tu Zamadai bada ya kuingia Serekali ya umoja wa Kitaifa SUk na kutaka kusibitisha kauli ya Maalim Seif alioitowa kipindi cha nyuma kabla ya kuingia ktk Serekali ya SUK.
  Katika kauli yake hivi sasa kuna wadai wa aina mbili kuna wadai waliokuwa wamiliki wa machamba ambayo yalichukuliwa na Serekali kabla ya mapinduzi na wakayagawa viwanja ambayo takribani nusu na robo ya unguja na Pemba Nyumba zilizo jengwa zimejengwa ktk mashamba ya watu.
  Na walio jenga wamepewa nyaraka za serekali na kupimiwa viwanja vya plan na Serekali na yako majumba ambayo yalibomaka kutokana na uchakavu na badae Serekali kuza eneo hilo au kuza bazi yao kwa raia na yako yalibakia kuweko mpaka leo ktk Mji mkongwe wa Unguja na Pemba haya yamemilikiwa na Serekali na kuitwa msajili wa Majumba.
  Sasa kwa kuondosha utata huu na kuisafisha nchi yetu kutokana na mambo yalio fanyika nyuma yasiendelee kufanyika tena,hivi sasa walokuwa na mashamba mashamba hayapo tena kuna Majumba yamejengwa ktk mashamba yao na umekuwa mji kusema zivunjwe nyuma zote na arudishiwe mwenye shamba itazidi kuleta mfarakano tena mpya ktk jamii? kwa vile miji mingi ya unguja na Pemba iko juu ya mashamba ya watu?.
  Sasa ili Zanzibar ivuke na tupate rehma na baraka za M/mungu ktk nchi yetu isizidi kwenda kwenye zulma, nilazima Serekali ya Umoja wa kitaifa SUk ishukuwe hatua ngumu ya wadai kama alivyo sema Maalim Seif kuwa hatuto wanyanganya watu majumba yao walokwisha kujenga na tukawarudishia viwanja wenyewe kwa vile ni Serekali ilio chukuwa viwanja na kuvigawa na kuwapa hati za serekali.
  lakufanya Serekali tutalipia fidia kwa wale wasil waliokuwa na mashamba yao na hivi sasa yameshajengwa nyuma za raia.
  Sasa chakujiuliza jee Serekali imefanya hivyo? maana hivi sasa kuna tatizo kubwa sana Zanzibar ktk kesi za madai hayo na mlengwa mkubwa ni serekali kwa vile wao ndio walio chukuwa mashamba na wakakata viwanje vya plan na kufanya miji ambayo takribani kila mji wa Zanzibar utaona umejenjwa ktk mashamba ya watu?.
  Sasa vipi Serekali italikwepa jambo hili? ama wavunje miji kurudisha mashamba ya walokuwa wamiliki au walipe fidia ili kujisafisha na zulma ilio fanyika ktk mkono wa serekali au walio jenga wenyewe wakubali kuvunja nyumba zao ili kurudisha shamba la watu.
  Hivi sasa unaweza kukaa na kujishtukizia umeletawa barua kutoka Wakfu na mali ya amana kwa kupitia kwa Sheha au naibu Sheha kuwa unaitwa Wakfu.
  Ukifika Wakfu unakutana na familia ambayo inakuambia pale ulipo jenga lilikuwa ni shamba letu ambalo lilishukuliwa na Serekali na likagawa viwanja, kwa hio sisi tuna pataka wenyewe, sasa kuna mambo mawili hapo kukubaliana kukusamehe kwa vile umesha jenga na hukujuwa na badae ukalipa fidia wewe mwenyewe binafsi, au kukwambia sisi hatutaki chochote tunataka sehemu yetu tu.
  Sasa ili serekali iondowe utata huu uliowaingizia wananchi hivi sasa nilazima ichuhulikie mambo haya haraka kama kweli tunataka kuisafisha nchi yetu na m/mungu angize mkono wake.
  Kuna zulma za mpili hapa kuna mzulumiwa wa mwanzo alokuwa na Shamba na wapili ni alopewa na serekali kiwanja kujenga bila kujuwa.
  Wote hawa ni walengwa na Serekali ndio muhusika mkubwa wa utata huu wa kushukuwa mashamba na kuyageuza miji.Kuna jamaa wengi hivi sasa wenye asili za kiarabu na kihindi wanadai majumba yao ya mji mkongwe,mengine bado yapo lakini mengine yamesha anguka na kuzwa kwa watu wa kawaida na kujengwa nyumba nyingine juu yake.
  nilazima serekali itowe jibu haraka ya utata huu ambao wao ndio wahusika wakubwa.
   
Loading...