Serekali ya kihuni: DAWASCO kutoza fees kwa watu waliochimba visima vya maji kwao

Binafsi huwa sipendi mambo ya kuitukana serikali na wanasiasa lakini katika hali ya uchumi ilivyosasa kuna mpango kambambe ushapitishwa na HARUNA MASEBU na wenzake kuwa kila aliyechimba kisima cha maji nyumbani kwake atatozwa fees

This is unfair na nadhani its about time tukaanzisha petition online, facebook na kufanya kampeni za kimataifa kulipinga hili kwa nguvu zote.

Hwa watu juzi wamespend zaidi ya bilioni 90 kwenye sherehe za uhuru leo wanataka kuwanyanyasa wananchi wa kipato cha chini kunywa maji

Pia ninategemea waziri kivuli na viongozi wa upinzani kulibebea bango hili to the end.
Hebu tupe Source ya habari zako ili tujue tuanzie wapi kuweka mikakati ya ku challenge hiyo idea. Au una wasiwasi mizengwe inawekwa kwa vile Arumeru mashariki visima vya maji viemeanza kuchimbwa na Nasari pamoja na Sabodo?
 
Nlisikia kuwa sheria ya kulipia visima ipo siku nyingi ila tatizo ni utekelezaji. Hata kuchimba kisima bila ruhusa ya Idara ya maji ni kosa kisheria maana inatakiwa visima vyote visajiliwe. Tatizo hapa, ukiandika barua kuomba ruhusa ya kuchimba maji, kujibiwa tu hiyo barua ni miaka!
Suala la kodi ya visima ni lile lile. Hamjasikia kuwa idadi ya walipa kodi nchini haizidi milioni 2? hapo wanajaribu kuongeza idadi na wigo wa kodi.
EWURA, ni mzigo mwingine kwetu, tunawalipa 1% kwenye bills za maji na umem
 
Binafsi huwa sipendi mambo ya kuitukana serikali na wanasiasa lakini katika hali ya uchumi ilivyosasa kuna mpango kambambe ushapitishwa na HARUNA MASEBU na wenzake kuwa kila aliyechimba kisima cha maji nyumbani kwake atatozwa fees

This is unfair na nadhani its about time tukaanzisha petition online, facebook na kufanya kampeni za kimataifa kulipinga hili kwa nguvu zote.

Hwa watu juzi wamespend zaidi ya bilioni 90 kwenye sherehe za uhuru leo wanataka kuwanyanyasa wananchi wa kipato cha chini kunywa maji

Pia ninategemea waziri kivuli na viongozi wa upinzani kulibebea bango hili to the end.

Acheni UPUUZI wenu, Mnaelekea kwenye malipo ya TV zenu hamsemi, hili la maji mnapiga kelele: kumbuka kulipia maji ni lazima. Soma sheria ya matumizi ya maji ya Mwaaka 2002. Na sio hao hata wale wanaomwagia MCHICHA kule msimbazi nao wanatakiwa kulipa ila tu kwa sababu ya ubutu wa sheria zetu ndio maana tumewaacha free.
 
Wambieni waishie huko huko DAWASCO wasifike AUWASA.
Jamaa yangu wa AUWASA aliniambia kodi ya kisima ni elfu 30 kwa mwaka.
Hao AUWASA walidhani wakinikatia maji ntaogopa, sijapata maji miezi 6 halafu nilipie capacity charge kila mwezi, siku walipokuja kukata niliwasimamia ili wakate haraka na nikawambia nitaunganisha tena siku wakishachimba visima Njiro. Yaani hata mgawo wa maji uliwashinda kusimamia.
 
Walimwaga tochi kibao kwa traffic wakaona ela haitoshi bse nyingi huenda kwa watu
Sasa wanalileta ili la visima hawa ndo watu ambao wanalipwa mishahara ya maana but output yao ndo iyoo!
Ivi mfano ukishawatoza iyo kodi sijui fine utapata tshs ngapi kwa mwezi then kwa mwaka.
Badala ya kufikilia sources za maana za gvt revenue mnaanza waza utumbo/mashudu!
No wonder baada ya ili mtakuja ata kwenye vyakula!
 
Wameshindwa kusambaza maji sasa wameona wawalipize hata waliojichimbia bisima,watoe nafasi iliwasaidiwe ktk usambazi wa maji
 
Acheni UPUUZI wenu, Mnaelekea kwenye malipo ya TV zenu hamsemi, hili la maji mnapiga kelele: kumbuka kulipia maji ni lazima. Soma sheria ya matumizi ya maji ya Mwaaka 2002. Na sio hao hata wale wanaomwagia MCHICHA kule msimbazi nao wanatakiwa kulipa ila tu kwa sababu ya ubutu wa sheria zetu ndio maana tumewaacha free.
Yeah, nilisikia kuna kitu kinaitwa water right. Wadau inabidi wajielimishe kuhusu hili kabla ya kulipuka tu.
Hifadhi ya maji ardhini inashabihiana na madini, huezi tu ukavuna bila utaratibu..kisayansi ilitakiwa mikondo yote ya hifadhi ya maji ardhini itathminiwe na ijulikane visima au maji kiasi gani yanaruhusiwa kuvutwa ktk eneo fulani kukizingatiwa na ile inayoitwa groundwater recharge. Hili halikwepeki,.. naeza sema safe way ya sasa ni kuvuna maji ya mvua, watu wakivuna haya maji hata street runoff zitapungua (or at least peak runoff) na kusave pesa ya ukarabati wa miundombinu ikiwemo barabara.
 
Na mbaya zaidi ata hao waliochimba kwa ajili ya huduma/kuuza wanaweza kugoma kutoa iyo huduma apo sasa wananchi Lazima waandamane ndo watatia akili!
Yaani badala ya kuwaza mambo ya maana ndo mnawaza fees.
Waambieni waliowatuma kuna fees nyingi za kucollect migodini
 
Tanzania mi naona wote tuiname kwa pamoja haraf tusimame kwa pamoja jib litapatkana kwa dola kandamiz mfumuko wa bei hawauon ndo kwanza wanaongeza gharama za maisha
 
Yeah, nilisikia kuna kitu kinaitwa water right. Wadau inabidi wajielimishe kuhusu hili kabla ya kulipuka tu.
Hifadhi ya maji ardhini inashabihiana na madini, huezi tu ukavuna bila utaratibu..kisayansi ilitakiwa mikondo yote ya hifadhi ya maji ardhini itathminiwe na ijulikane visima au maji kiasi gani yanaruhusiwa kuvutwa ktk eneo fulani kukizingatiwa na ile inayoitwa groundwater recharge. Hili halikwepeki,.. naeza sema safe way ya sasa ni kuvuna maji ya mvua, watu wakivuna haya maji hata street runoff zitapungua (or at least peak runoff) na kusave pesa ya ukarabati wa miundombinu ikiwemo barabara.

Point yako nini hapo???? Huwezi kuipa hoja uzito kwa kuleta sheria na vocabulary za tasnia husika banaaa
So ukiwalipisha watu hiyo ground water recharge ndo inakuwa ballanced kwa pesa itayokusanywa au????
Au ndo yatanunuliwa kutoka Kenya na kuja kumwagwa Tanzania for re-saturation kwa kutumia hayo makusanyo????

Kama hoja inalenga kwenye "tragedy of the commons" then solution yake haiwezi kuwa any sort of charging system mkuu
 
Hapo pazuri ni wajaribu mie na kisima changu kivule nimechimba kwa 3milion nawakaribisha kama ni mtendaji wa mtaa,wajinga majembe au yono action mart kwangu hata leo lazima niwapeleke makaburi ya kinondoni.Masebu naye anatoa ushauri mfu kwa taifa ili mafuta ya pamoja bado bei inazidi kuongezeka na uchakachuaji unazidi sasa naye ni mzigo na EWURA yake. 3% ya mauzo ya maji na huduma ya umeme kwa EWURA ambacho ni chanzo cha mapato kwa EWURA kinamptosha macho.SHAME ON THEM
 
hamjawahi ona vita ya jeshi la mtu mmoja na serikali yake basi inakaribia?Ole wake mtu aje kwangu eti lete kodi ya maji atajuta nini kimemleta.
:smash:
 
Point yako nini hapo???? Huwezi kuipa hoja uzito kwa kuleta sheria na vocabulary za tasnia husika banaaa
So ukiwalipisha watu hiyo ground water recharge ndo inakuwa ballanced kwa pesa itayokusanywa au????
Au ndo yatanunuliwa kutoka Kenya na kuja kumwagwa Tanzania for re-saturation kwa kutumia hayo makusanyo????

Kama hoja inalenga kwenye "tragedy of the commons" then solution yake haiwezi kuwa any sort of charging system mkuu
Soma tena nilichoandika halafu unambie hujaelewa wapi.
 
Hii nchi sasa inakoelekea ni hatari sasa. imekuwa kama haina mwenyewe ni shamba la bibi... basi itafika kipindi watasema hata makaburi yatozwe fee..kisima nichimbe mwenyewe kwa gharama zangu tena kwenye kiwanja changu ambacho bado nalikipia ada kila mwaka.....naomba mungu hizi habari zibaki kuwa tetesi...tukilemaa hili likapitishwa basi nao tanesco wanatesema wote wanaotumia jenereta zao walipie ada kwa kutumia....god forbid

...nasubiri aje mtu hapa kwangu ...Hata TV yangu ikitumika kuniletea habari hiyo ntaichukulia hatua stahiki. Ebo!!
Yaani ushindwe kuniletea maji, nihangaike kivyangu, halafu eti nini?
 
Hii ndiyo Serikali yetu ya KIFISADI! Kwa sheria gani na vigezo gani vya sheria wawatoze watu wanaochimba visima vyao na kupata maji chini ya ardhi, tena maji yenyewe yasiyo na hata chembe na ubora sembuse kuwa maji ya chumvi hapa Dar? Labda huko mikoani! Mwe! Lazima tuanzishe kampeni kuupinga mkakati huu. Tupeni habari kamili.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom