Serekali ya kihuni: DAWASCO kutoza fees kwa watu waliochimba visima vya maji kwao

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
Binafsi huwa sipendi mambo ya kuitukana serikali na wanasiasa lakini katika hali ya uchumi ilivyosasa kuna mpango kambambe ushapitishwa na HARUNA MASEBU na wenzake kuwa kila aliyechimba kisima cha maji nyumbani kwake atatozwa fees

This is unfair na nadhani its about time tukaanzisha petition online, facebook na kufanya kampeni za kimataifa kulipinga hili kwa nguvu zote.

Hwa watu juzi wamespend zaidi ya bilioni 90 kwenye sherehe za uhuru leo wanataka kuwanyanyasa wananchi wa kipato cha chini kunywa maji

Pia ninategemea waziri kivuli na viongozi wa upinzani kulibebea bango hili to the end.
 
...nasubiri aje mtu hapa kwangu ...Hata TV yangu ikitumika kuniletea habari hiyo ntaichukulia hatua stahiki. Ebo!!
Yaani ushindwe kuniletea maji, nihangaike kivyangu, halafu eti nini?
 
Mh! Kama ni kweli basi hii kali. Labda kwa waliochimba visima kwa madhumuni ya kufanya biashara hao wanatakiwa kulipa kodi kama wafanyabiashara wengine. Lakini kama ni kwa ajili ya matumizi binafsi baada ya DAWASCO hao hao kushindwa kutoa huduma walizotakiwa kuzitoa then hii haiingii akilini asilani. Je, kuna sheria inayohalalisha hayo?
 
Hawa Dawasco mbona hawana akili,maji yenyewe hakuna kama wanataka wasambaze maji nchi nzima na yawe yanatoka 24hrs kama hawawezi acha tuchimbe wenyewe bwana!!
 
hawawezi kuleta upuuz kama huo, mwisho wa siku utaambiwa ulipe kodi choo chako cha shimo.
 
Mh! Kama ni kweli basi hii kali. Labda kwa waliochimba visima kwa madhumuni ya kufanya biashara hao wanatakiwa kulipa kodi kama wafanyabiashara wengine. Lakini kama ni kwa ajili ya matumizi binafsi baada ya DAWASCO hao hao kushindwa kutoa huduma walizotakiwa kuzitoa then hii haiingii akilini asilani. Je, kuna sheria inayohalalisha hayo?

...kulipa kodi dawasco!?
 
Afanalek!! Kuweni na staha, huyu Masebo ndio serikali? Sidhani kama lengo lake litakubalika, kwa sababu wabunge, watu maarufu, taasisi za kidini na nyinginezo zinachimba visima, kama kuna kutozwa kodi nani atachimba visima hivyo wakati serikali peke yake haiwezi? Tufe kwa kiu? asituongezee kutupa maumivu kama kodi zilizopo.
 
Ati nini? Yani mie sipati maji na niamue nichimbe kisima kwangu halafu hawa Dawasco waje kunitoza kwa kujitafutia maji yangu mwenyewe? Hii ni halali kweli? Wana akili hawa? Na serikali inawasapoti? Watakuja na kodi ya choo cha shimo hawa! Hapana aisee kunaile kitu inaitwa haki za binadamu naona ntatumia wakinifata!! Na hii manake ni kwamba Taneshko nao watatoza watu wenye Solar power majumbani mwao wakati umeme wenyewe hakuna? Yani mpaka najisikia kutapika tapika kwa kweli... Ngoja waje ntawatapikia!!!
 
huo utakua ni upuuzi kabisa, badala ya kusambaza huduma ya maji wamekalia kutafuta hela za wanyonge ili wazitafune.... Nipo dar toka mwa 1990 siyajui maji ya Nuwa wala Dawasco......bora ninyamaze maana nita-lusinde bure hapa
 
Kama ni kweli mpango huo upo utakuwa ni uonevu kwa wananchi. Wangetuambia kwamba watawatoza kodi kwa waliochimba kwa madhuni ya kibiashara hapo ningekubaliana nao.
 
Mkuu nakuunga mkono. Na vita kuu ya nne italetwa na ARDHI, na ile ya tano na ya mwisho italetwa na DINI na ndio utakuwa mwisho wa dunia.

Umekosa! vita ya mwisho itasababishwa na chakula na maji.
 
Jamani hiyo kitu sio mpya.
Ipo kwenye makaratasi tangu enzi za nuwa ila ilikuwa ni swala la ufuatiliaji tuu.
Naona sasa wameamua kufuatilia baada ya Serikali kuwa hoi kifedha.
 
Binafsi huwa sipendi mambo ya kuitukana serikali na wanasiasa lakini katika hali ya uchumi ilivyosasa kuna mpango kambambe ushapitishwa na HARUNA MASEBU na wenzake kuwa kila aliyechimba kisima cha maji nyumbani kwake atatozwa fees

This is unfair na nadhani its about time tukaanzisha petition online, facebook na kufanya kampeni za kimataifa kulipinga hili kwa nguvu zote.

Hwa watu juzi wamespend zaidi ya bilioni 90 kwenye sherehe za uhuru leo wanataka kuwanyanyasa wananchi wa kipato cha chini kunywa maji

Pia ninategemea waziri kivuli na viongozi wa upinzani kulibebea bango hili to the end.

Waambie waanzie kwangu tuone kama kuna atakaepona brain concussion. Yaani nichimbe kwa gharama zangu then unitoze fees? Kwa hili, niko tayari kwenda Segerea. Alaaaa!
 
Mie kwangu kuna kisima na alogwe mtu aje eti kodi ya DAWASCO? Nitamtoa mtu kamasi!
 
Hii imekaa vizuri sana na ninaombea waweke kodi kubwa tu ili watu wa Dar akili zao zipate SHOCK kidogo.

Nitawashukuru sana wakianza hivyo mapema mno ili wakumbatia CCM wa Dar waanze kujua nini maana ya CCM.

Kwa majimbo yasiyo na CCM nina imani wabunge wake watakomaa nao ili kuwatolea mbali kama vile wamemuona Santa Claus aliyekuja nyumbani na fimbo tu bila zawadi. Unamnyang'anya hiyo fimbo yake na kumcharaza hadi arudi kwao Finland.

Somo litaeleweka tu maana sasa hivi serikali imeishiwa na mtu lazima aruke majuu ili ndege isipate kutu, hata ikibidi kuuza watoto wetu wa Kike ili hela ipatikane basi watoto watauzwa.

Kufa hatutakufa ila cha moto tutakiona.
 
Back
Top Bottom