Serekali ya CCM yajenga makaburi feki Mpwapwa

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Messages
11,290
Points
2,000

Kibo10

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2013
11,290 2,000
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Chipogolo wilayani Mpwapwa mkoa Dodoma, wameulalamikia uongozi wa serikali yao kujenga makaburi feki pasipo kuwashirikisha wahusika wa makaburi hayo.

Wakizungumza wananchi hao wamemtupia lawama mtendaji wa kijiji YONA MGANGA, na kusema kuwa serikali imeamua kuhamisha makaburi bila kufuata utaratibu.

Akizungumza EMANUELL MKIGA mmoja wa vijana walio pata tenda ya uhamishaji wa makaburi hayo ameelezea jinsi zoezi hilo la ujenzi wa makaburi feki lilivyofanyika katika kijiji hicho kwa kusema kuwa walilipwa shilingi elfu tisa kwa ajili ya ujenzi.

ARFEDI NDEGEULAYA Mwenyekiti wa kijiji cha mpwapwa amethibitisha kuwepo kwa tatizo hilo na kusema kuwa yeye anafanya jitihada mbalimbali ili kumaliza tatizo hilo katika kijiji chake.
 

Forum statistics

Threads 1,392,167
Members 528,552
Posts 34,100,407
Top