• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Serekali Ya CCM Hamzioni Dalili Hizi

Chademakwanza

Chademakwanza

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2014
Messages
6,348
Points
1,225
Chademakwanza

Chademakwanza

JF-Expert Member
Joined Jun 11, 2014
6,348 1,225
Nimekaa nikatafakari Sana kwa maslahi yangu binafsi na kwa nchi yangu nikaona angalau niliseme hili. Huko tunakoelekea tunakwenda kulaumiana kwa kushindwa kufungua macho kuliona hili.

Mgomo wa Magari Leo umenifanya nitafakari upya ufanisi wa Serikali hii inayoongozwa na chama cha mapinduzi CCM.

Miezi michache iliyopita tulishuhudia mgomo wa wenye maduka, hapo nyuma kidogo ulikuwepo na mgomo wa waalimu japokuwa hadi sasa wapo kwenye mgomo baridi matokeo ya mtihani yanasadifu kinachoendelea madarasani, kabla ya huo ulikuwepo wa madaktari nk.

Migomo hii imetokea ndani ya miaka 4 na ni migomo iliyoitikisa nchii kweli sisi wenyewe ni mashahidi. Leo wenye magari wameamua Kuwa frustrate wadogo zetu walioanza mitihani yao jana. Kuna wanafunzi leo kwa namna moja au nyingine watakuwa wameharibiwa feature zao kutokana na mgomo huu. Achana na hasara za kiuchumi na usumbufu ambao raia wameupata.

Hizi ni dalili mbaya kwa serikali lazma tuseme ukweli hapa. Mapinduzi mengi duniani ya kisiasa yametokea kutokana na vitu kama hivi. Hadi kufika hapa niseme ni wakati muafaka sasa kwa chama cha mapinduzi ccm kuachia madaraka na wao kuwa wapinzani.

Crane Brinton ni katika nadharia yake ya mapinduzi aliyoiandika kwenye kitabu chake cha " Anatomy of revolution" anafananisha mapinduzi na homa. Katika mazingira hayo Brinton anasema homa si jambo la kufurahia na linapaswa kuepukika au kutibiwa kwa mapema pindi dalili za homa hiyo zinapojitokeza.

Kwenye nadharia hiyo Brinton kutokana na uzoefu alioupata kwenye American revolution, France Revolution na British revolution alihitimisha nadharia hii kwa kusema kuwa kuna hatua kuu tatu za taifa kupitia hatimaye mapinduzi kutokea iwe katika mazingira yoyote yale.

Kwenye hatua ya kwanza hapa kwetu ni sawa na kwamba tumeshaikamilisha (symptoms stage). Kwenye hatua hii kuna mambo mengi ambayo hutokea na kwa hapa kwetu tayari yameshakamilika na ukamilisho wake ni hii migomo ambayo serikali imeshindwa kuizuia.

Matatizo ya kiuchumi tunayoshuhudia sasa kama kushuka kwa thamani ya shilingi, serikali kushindwa kutetekeleza majukumu yake kwa ufanisi, migomo ya watu kukataa kulipa kodi, viongozi kushindwa kutoa kauli za mwisho, rushwa na ufisadi mkubwa , ni vitu vinavyoelezewa kwenye hatua hii. Swali la kujiuliza haya yameshatokea au bado?

Huwezi kumwambia mtu alipe kodi huku fedha nyingi za wananchi wa Taifa hili zikiwa kwenye account za wachache.

Wamekuwa wakijiamini na kuongoza kwa kutumia vyombo vya Dola ila mapinduzi yakifikia hatua ya mwisho vyombo hivi huamua kushirikiana na raia kuwaondoa kabisa mapinduzi mengi hili limefanyika hata juzi juzi tuliliona Misri.

Japokuwa tumeshaanza hatua ya pili ila tunaweza kuitibu homa hii. Homa hii itatibiwa kwa kukubali kuambizana ukweli. Ukimya wa viongozi wa Ccm unatumika vibaya kwa waliopewa madaraka, wananchi wanaumia lazima tuseme au tukubali kuwa wamechoka na wawaachie wengine.

Kwa mwendo huu Hapana hatuwezi kufika niwakati muafaka sasa kufanya maamuzi sahihi wala si maamuzi magum kwa maslahi mapana ya nchi Yangu.

Mungu ibariki Tanzania
 

Forum statistics

Threads 1,402,655
Members 530,951
Posts 34,401,273
Top