OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 419
- 669
Kwenye kiswahili tuna neno moja kwa maneno hayo mawili ya kiingereza, Mkulima. Lakini watu wanaoweza kuilisha nchi ni ‘Farmers’ sio ‘peasants’. Kwa tafsiri sahihi, ‘Peasant’ ni mtu anayelima ili kujazia padogo palipopungua. Hawa huwa wanalima kwa kile kitu tunaita ‘subsistance economy’ just for consumption. Ila pia hata kwa namna hiyo, mazao yao huwa hayawatoshi na hulazimika kununua miezi kadhaa baada ya msimu wa mavuno kuisha
Tumesikia kuwa, Tanzania ina wakulima zaidi ya 50% hizi ni takwimu zisizozingatia tofauti ya maneno tajwa hapo juu. Kama wakulima ni asilimia hizo, ama kwa hakika tusingekuwa tuna-import chakula zaidi tungekuwa ni exporters wakubwa wa bidhaa za kilimo
Hii inaonyesha kuwa tumeshindwa kuona mkulima haswa wa kumpa mazingira bora ni yupi, tumebaki kuwaambia vijana wakalime huku tukijua fika hawana mitaji. Wengine wanasema mitaji ipo, anza kidogo kidogo, yote haya yanasisitiza kilimo cha small scale ambacho ni u-peasant na sio ukulima
Taja wakulima kama kina Summry ambao wanalima mashamba ya kutosha na wamejiwekeza kwa mabilioni ya pesa. Leo unampa kijana laki 6 akalime, ili umuite mkulima, ukuze uchumi. Wakati chakula atakachozalisha hakitoshi kumlisha hata yeyey mwenyewe kwa mwaka mmoja. Kuna mkulima hapo?
Mahusiano ya kiuchumi hubadilika muda na muda, kilimo kilianza kwa ile wanaita labor intensive technique, ambayo ilionekana kuwa ni muhimu kipindi kile cha Nyerere, though tulikuwa nyuma ya muda.
Kipindi kile wakawa na kauli ya KILIMO CHA KUFA NA KUPONA, ilikuwa hivyo ili vijana wasikae kijiweni. Lakini mtu hafui dafu kwenye teknolojia, na hata KILIMO CHA KUFA NA KUPONA hakikuwa na matunda kwa kuwa baadae tukaanza kuagiza chakula kutoka nje, (Japo hapa zipo sababu tofauti tofauti tofauti)
Baadae tukaja na kauli KILIMO UTI WA MGONGO, watu wakaima sana, lakini bado hatukutambua kuwa kilimo hiko kilikuwa hakijalenga kwenye kubadili mfumo wa kutoka kwenye labour intensive kuja kwenye Capital Intensive technique, kilimo uti wa mgongo kikaenda na maji
Tumekuja kwenye KILIMO KWANZA, tunachukua mawazo yasiyo na tija kuyatumia na bado tunapata shida zilezile za awali. Tunasema wakulima zaidi ya 50% Corona imetutisha kidogo tu, tunaona upeo wa njaa, sasa hao wakulima asilimia 85 walikuwa wanlima nini? Walicholima kikowapi kituokoe kwenye kipindi hiki
Wala hatutakiwi kuruka stage, kama hiyo ya kubaki kwenye jembe la mkono kuhamia kwenye hydrospony, huko ni mbali bado ardhi ipo na ina rutuba, inapaswa kutumika. Wala tusikimbilie teknolojia kwa sababu fulani anafanya bali kuangalia tija yake.
Hizo hydrospony ziwe kwa kilimo bustani na mashamba darasa kwa maprofesa wakilimo ili nao wafanye mazoezi nyumbani sio kilimo cha kuokoa nchi.
Tafsiri ya uchumi nnayoikubali ni ya Adam Smith, inquiry into a nature
HOJA: Sera zijikite kwenye kuzalisha wakulima na sio kuwafariji Peasants
Signed:
Oedipus