Sera za Kibepari za CCM ndiyo chanzo cha Mgomo wa TUCTA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sera za Kibepari za CCM ndiyo chanzo cha Mgomo wa TUCTA

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 9, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ubepari ule wa asili kabisa una matokeo mengi mazuri na mabaya; nitawaacha wengine wayazungumzie mazuri lakini lakini itoshe miye kusema tu kuwa mojawapo ya matokeo mabaya ya ubepari ni mgongano kati ya waajiri na wafanyakazi. Wafanyakazi chini ya mfumo wa kibepari hujikuta mara zote katika mgongano na mazungumzo na waajiri kwa sababu mfumo wa ubepari hauwezi kamwe kuwatuliza wafanyakazi na kuwahakikishia maisha bora na usalama wa kazi zao.


  Ni lazima tuelewe kwanini mgogoro unanukia kati ya wafanyakazi na serikali pamoja na waajiri wengine; mgogoro ambao matokeo yake yatakuwa ni mgomo wa kitaifa. Hatuwezi kuuelewa mgogoro huu au mingine itakayotokea huko mbeleni bila kuelewa japo kwa kiasi tu mfumo wa ubepari ulivyo na kwanini mfumo ndio unatengeneza hali zinazosababisha migongano hii ya waajiri na wafanyakazi.


  Mojawapo ya makosa makubwa ambayo kama taifa tumeyafanya baada ya kuamua kuacha kujenga nchi kwa mfumo wa ujamaa tuliotaka kuujenga ni kujaribu kujenga nchi bila kuanisha mfumo tunaotaka kujenga nchi hiyo. Wanasiasa wetu waliopokea jukumu la kutuongoza kuelekea kwenye mabadiliko ya kiuchumi waliamua kufanya hivyo kwa kubunia na kukisia bila kuanisha itikadi na nadharia za kutuongoza huko tunakotaka kwenda. Matokeo yake waliupokea ubepari bila kuuhoji, kuukosoa, kuuchambua wala kuufafanua kwa wananchi.
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,547
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji, nimekusoma japo utangulizi tuu, I'd like to differ kwa hoja ,moja tuu ni kuhusu vyama vya wafanyakazi enzi za mfumo wa Ujamaa, enzi za NUTA then JUWATA.

  Enzi hizo hakukuwepo migomo simply kwasababu hakukuwa na vyama huru vya wafanyakazi. NUTA na JUWATA zilikuwa ni jumuiya ya Chama, enzi hizo chama ndicho kilichokuwa kimeshika hatamu za uongozi. Hicho chama ambacho ni jumuiya ya chama tawala kilichoshika hatamu za uongozi wa nchi, kitaanzia wapi kuitiasha mgomo?.

  Chama imara cha wafanyakazi kwa nchi za kisoshalisti, kilikuwa ni cha Poland tuu enzi zile kikiwa chini ya Lech Walesa, kuna uwezekano pia vyama imara viko na nchi nyingine za kijamaa ila havikusikika.

  Baada ya kupanua demokrasia, chama kikaachia hatamu za uongozi kwa serikali, ndivyo vikaundwa vyama huru vya wafanyakazi ambayo ndivyo hivi vinavyokohoa sasa.

  My opinion kuhusu mgomo, uhalali wake bado haujatimia mpaka mazungumzo yanapovunjikia mezani.

  Nitarejea baada ya kumaliza kukusoma.
   
Loading...