Uchaguzi 2020 Sera za CHADEMA kwenye kunyimwa Uhuru wa Kuandamana na Uhuru wa Tume ya Uchaguzi zinakinzana

Jul 8, 2015
31
39
Kauli za CHADEMA kuhusu Kunyimwa Uhuru wa Kuandamana na Uhuru wa Tume ya Uchaguzi Zinakinzana na Uhalisia.

Katika baadhi ya nguzo wanazojiandaa nazo kwa kusimama kidete kuelekea kampeini za Uchaguzi Mkuu, 2020, CHADEMA wanadai, huku wakiipotosha jamii ndani na nje ya nchi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.

Dk. John Pombe Magufuli, amekuwa akiminya Demokrasia ya upinzani kwa kuzuia maandamano kwa upande mmoja na huku wakidai kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi haiko huru, kwa upande mwingine!

Ikumbukwe kwamba Rais wetu hakuwahi kutamka kuwa wapinzani wasiandamanebali ukweli ni kwamba chanzo cha CHADEMA kutoandamana ni amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza katika *Shauri la Maombi Mchanganyiko (Miscellaneous Civil Application) Na. 87/2016 kati ya Freeman Aikael Mbowe vs Officer Commanding District Geita & Attorney General,* mbele ya *Mhe. Jaji Matupa.*

Katika shauri hilo CHADEMA waliandika barua ya kuomba kibali cha kuandamana kwa OCD Geita ambaye aliwajibu kwa barua kuwa wavumilie kidogo kwa sababu hakuwa na nguvu ya kutosha kuwapa waandamanaji ulinzi kwani jeshi la polisi (askari polisi) walikuwa kenye operesheni ya kulinda amani kwenye matukio yaliyokuwa yanalisumbua Taifa katika maeneo mbali mbali ya nchi hasa Kibiti, Ikwiriri na Amboni, pamoja na uvamizi wa vituo vya polisi katika maeneo mbali mbali nchini. OCD aliongeza pia kuwa atawajibu haraka iwezekanayo hali ya amani itakapotulia.

Kwa mujibu wa kifungu cha 11(4) cha Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258 na Kifungu cha 43(1) cha Sheria ya Jeshi la Police na Huduma Saidizi (Police Force and Auxiliary Services Act, Sura ya 322 vinavipa wajibu vyama vya siasa kuomba
kibali kwa kutoa taarifa kwa OCD kuhusu kusudio la kuandamana au kufanya mikutano; wakati kifungu cha 11(6) cha Sheria ya Vyama kikisomwa sambamba na kifungu cha 43(3) na 44 vya Sheria ya Jeshi la Police vinampa mamlaka OCD
kuzuia maandamano au mikutano endapo kwa maoni yake maandamano hayo yanaweza kuwa na athari kwa usalama wa umma, au atakavyoona inafaa.

Hivyo, maandamano yale ya CHADEMA hayakuwa sahihi kwa sababu kwa kipindi kile polisi ambao wangewapa ulinzi waandamanaji walikuwa kwenye operesheni ya kijeshi kulinda amani ya nchi katika maeneotajwa hapo juu kiasi kwamba OCD aliona inafaa awambie wavumilie kwani ingekuwa ni hatari kuwaruhusu kuendelea na maandamano bila ulinzi wa Askari Polisi.

Sasa, Sheria ya Jeshi la Polisi kifungu cha 43(6) kinasema mtu yeyote ambaye hakuridhika na uamuzi wa OCD akate rufaa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani kitu ambacho CHADEMA badala ya kuheshimu sheria na taratibu zilizowekwa walikaidi na kukimbilia mahakamani.

Mahakama iliridhishwa na utetezi wa serikali na kushawishika kwa mujibu wa Sheria ya Mienendo ya Madai, (Order XXIII Rule 3) na hivyo kuamuru kwamba CHADEMA waache Kuandamana na wala kuleta tena mahakamani kesi za namna hiyo
zinazohusu maandamano isipokuwa labda likitokea tukio linguine la namna hiyo litokee, ambalo ni uchaguzi mkuu mwingine.

Sheria ya Mwenendo wa madai ambazo hukumu ya mahakama iliegemea hairuhusu hata kukata rufaa kwenda Mahakama ya Rufani wala kufungua kesi upya, na hapo ndipo badala yake CHADEMA walikimbilia mitaani na katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ndani na nje ya nchi kusambaza uwongo kwa kumsingizia Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania eti anaminya Demokrasia kwa kuzuia uhuru wa vyama vya upinzani kueleza hisia zao kwa njia ya maandamano. Ukweli ni kwamba Rais hakuwahi kutamka kitu kama hicho bali CHADEMA walivunja sheria na taratibu
zilizowekwa na hivyo wakazuiwa na mahakama.

Kwa upande wa pili, katika sera zao, CHADEMA wamejipanga kwa kupotosha umma kwa kisingizio cha uhuru wa
Tume ya Uchaguzi. Maneno haya si kweli bali ndani yake yamebeba kusudio la kuujengea umma wa watanzania dhana ya kuwa Tume haiaminiki.

Kwa Mujibu wa Ibara ya 74 (7) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, toleo la 2008 inasema *“Kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu yake yaliyoainishwa katika ibara hii, *Tume ya Uchaguzi itakuwa ni idara huru inayojitegemea, itafanya maamuzi yake rasmi kuhusu utekelezaji wa majukumu yake kwa vikao, na mtendaji wake mkuu atakuwa ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye atateuliwa na kufanya kazi kwa mujibu wa masharti ya sheria iliyotungwa na Bunge”.*

Sasa CHADEMA hawasemi ni maneno gani matamu zaidi ya haya yaliyomo kwenye Ibara hii ya Katiba kiasi kwamba wanataka Katiba mpya itungwe kuweka Tume huru ya Uchaguzi. CHADEMA wanatakiwa kuuambia umma kuwa labda
kuna mtu au kundi la watu wanaingilia uhuru Tume; au kiongozi fulani wa Tume anapendelea chama fulani cha siasa.

Mambo haya ni ya kawaida katika taasisi zote na endapo mtu yeyote ameingilia Tume; au kiongozi yeyote wa Tume
amependelea chama fulani Cha siasa ni suala la ushahidi na ikidhibitika hivyo kinachotakiwa si kutunga Katiba mpya kwani ni suala la uadilifu kama makosa mengine ya kinidhamu na hivyo wanatakiwa kuleta ushahidi ili kuwajibisha aliyekiuka.

Kwa maana hiyo maneno yote ya chadema kuhusu Tume kukoswa uhuru ni majungu tu kwani hakuna mtu hata mmoja wanayemtaja kuingilia mamlaka ya au uhuru wa Tume wala ushahidi kwamba kuna Afisa yeyote wa Tume anayetajwa kupendelea chama fulani cha siasa hivyo kukiuka maadili ya Tume ya Uchaguzi.
 
Kauli za CHADEMA kuhusu Kunyimwa Uhuru wa Kuandamana na Uhuru wa Tume ya Uchaguzi Zinakinzana na Uhalisia.

Katika baadhi ya nguzo wanazojiandaa nazo kwa kusimama kidete kuelekea kampeini za Uchaguzi Mkuu, 2020, CHADEMA wanadai, huku wakiipotosha jamii ndani na
nje ya nchi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dk. John Pombe Magufuli, amekuwa akiminya Demokrasia ya upinzani kwa
kuzuia maandamano kwa upande mmoja na huku wakidai kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi haiko huru, kwa upande mwingine!

Ikumbukwe kwamba Rais wetu hakuwahi kutamka kuwa wapinzani wasiandamanebali ukweli ni kwamba chanzo cha CHADEMA kutoandamana ni amri ya Mahakama
Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza katika
*Shauri la Maombi Mchanganyiko (Miscellaneous Civil Application) Na. 87/2016 kati ya Freeman Aikael Mbowe vs Officer Commanding District Geita & Attorney General,* mbele ya *Mhe. Jaji Matupa.*

Katika shauri hilo CHADEMA waliandika barua ya kuomba kibali cha kuandamana
kwa OCD Geita ambaye aliwajibu kwa barua kuwa wavumilie kidogo kwa sababu
hakuwa na nguvu ya kutosha kuwapa waandamanaji ulinzi kwani jeshi la polisi
(askari polisi) walikuwa kenye operesheni ya kulinda amani kwenye matukio
yaliyokuwa yanalisumbua Taifa katika maeneo mbali mbali ya nchi hasa Kibiti, Ikwiriri na
Amboni, pamoja na uvamizi wa vituo vya polisi katika maeneo mbali mbali nchini.
OCD aliongeza pia kuwa atawajibu haraka iwezekanayo hali ya amani itakapotulia.

Kwa mujibu wa kifungu cha 11(4) cha Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258 na
Kifungu cha 43(1) cha Sheria ya Jeshi la Police na Huduma Saidizi (Police Force
and Auxiliary Services Act, Sura ya 322 vinavipa wajibu vyama vya siasa kuomba
kibali kwa kutoa taarifa kwa OCD kuhusu kusudio la kuandamana au kufanya
mikutano; wakati kifungu cha 11(6) cha Sheria ya Vyama kikisomwa sambamba na
kifungu cha 43(3) na 44 vya Sheria ya Jeshi la Police vinampa mamlaka OCD
kuzuia maandamano au mikutano endapo kwa maoni yake maandamano hayo
yanaweza kuwa na athari kwa usalama wa umma, au atakavyoona inafaa.

Hivyo, maandamano yale ya CHADEMA hayakuwa sahihi kwa sababu kwa kipindi kile
polisi ambao wangewapa ulinzi waandamanaji walikuwa kwenye operesheni ya
kijeshi kulinda amani ya nchi katika maeneotajwa hapo juu kiasi kwamba OCD aliona inafaa awambie wavumilie kwani ingekuwa ni hatari kuwaruhusu kuendelea na maandamano bila ulinzi wa Askari Polisi.
Sasa, Sheria ya Jeshi la Polisi kifungu cha 43(6) kinasema mtu yeyote ambaye
hakuridhika na uamuzi wa OCD akate rufaa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani kitu
ambacho CHADEMA badala ya kuheshimu sheria na taratibu zilizowekwa walikaidi
na kukimbilia mahakamani.
Mahakama iliridhishwa na utetezi wa serikali na kushawishika kwa mujibu wa Sheria ya Mienendo ya Madai, (Order XXIII Rule 3) na
hivyo kuamuru kwamba CHADEMA waache Kuandamana na wala kuleta tena mahakamani kesi za namna hiyo
zinazohusu maandamano isipokuwa labda likitokea tukio linguine la namna hiyo litokee,
ambalo ni uchaguzi mkuu mwingine.
Sheria ya Mwenendo wa madai ambazo hukumu ya mahakama iliegemea
hairuhusu hata kukata rufaa kwenda Mahakama ya Rufani wala kufungua kesi upya, na hapo ndipo badala
yake CHADEMA walikimbilia mitaani na katika vyombo vya habari na mitandao ya
kijamii ndani na nje ya nchi kusambaza uwongo kwa kumsingizia Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania eti anaminya Demokrasia kwa kuzuia uhuru wa vyama
vya upinzani kueleza hisia zao kwa njia ya maandamano. Ukweli ni kwamba Rais
hakuwahi kutamka kitu kama hicho bali CHADEMA walivunja sheria na taratibu
zilizowekwa na hivyo wakazuiwa na mahakama.

Kwa upande wa pili, katika sera zao, CHADEMA wamejipanga kwa kupotosha umma kwa kisingizio cha uhuru wa
Tume ya Uchaguzi.
Maneno haya si kweli bali ndani yake yamebeba kusudio la kuujengea umma wa watanzania dhana ya kuwa Tume haiaminiki.
Kwa Mujibu wa Ibara ya 74(7) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
1977, toleo la 2008 inasema
*“Kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu yake yaliyoainishwa katika ibara hii, *Tume ya Uchaguzi itakuwa ni idara huru inayojitegemea, itafanya maamuzi yake rasmi kuhusu utekelezaji wa majukumu yake kwa vikao, na mtendaji wake mkuu atakuwa ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye atateuliwa na kufanya kazi kwa mujibu wa masharti ya sheria iliyotungwa na Bunge”.*
Sasa CHADEMA hawasemi ni maneno gani matamu zaidi ya haya yaliyomo
kwenye Ibara hii ya Katiba kiasi kwamba wanataka Katiba mpya itungwe kuweka
Tume huru ya Uchaguzi. CHADEMA wanatakiwa kuuambia umma kuwa labda
kuna mtu au kundi la watu wanaingilia uhuru Tume; au kiongozi fulani wa Tume anapendelea chama fulani cha siasa. Mambo haya ni ya kawaida katika taasisi zote na endapo mtu yeyote ameingilia Tume; au kiongozi yeyote wa Tume
amependelea chama fulani Cha siasa ni suala la ushahidi na ikidhibitika hivyo kinachotakiwa
si kutunga Katiba mpya kwani ni suala la uadilifu kama makosa mengine ya
kinidhamu na hivyo wanatakiwa kuleta ushahidi ili kuwajibisha aliyekiuka.
Kwa maana hiyo maneno yote ya chadema kuhusu Tume kukoswa uhuru ni
majungu tu kwani hakuna mtu hata mmoja wanayemtaja kuingilia mamlaka ya au uhuru wa
Tume wala ushahidi kwamba kuna Afisa yeyote wa Tume anayetajwa kupendelea chama
fulani cha siasa hivyo kukiuka maadili ya Tume ya Uchaguzi.
 
Dzzdd

Back
Top Bottom