Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,460
- 39,928
Tuliwahi kuwa na viwanda vingi na vya namna mbalimbali ambavyo lengo lake kubwa lilikuwa ni kutengeneza uwezo wa ndani wa taifa kuzalisha bidhaa mbalimbali ili kutosheleza kwa kiasi kikubwa mahitaji ya ndani ya nchi..
Lakini, kubwa zaidi katika mawazo ya Mwalimu na waasisi wa taifa letu lengo lilikuwa ni kutengeneza kile ambacho tunakiita "nguvukazi" (manpower) ya ndani ili kuchukua nafasi mbalimbali zilizokuwa zinashikiliwa na wageni. Katika kufanya hili miaka ya mwanzo tukajitahidi sana kuwapa nafasi watanzania kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika makampuni na mashirika mbalimbali yale ambayo tuliyajua kuwa ni "mashirika ya umma".
Baada ya kutarajia kuwa lawama kubwa zaweza kuletwa kwa ujamaa na nyerere naomba niwakubalie watakaoleta hoja hizo na tutoke kwenye hayo ya ujamaa na Nyerere na twende mbele zaidi.
Naomba nichochee mjadala kwa misingi ifuatayo:
a. Viwanda hivi vilikuwa na mafanikio ya kiasi gani katika majukumu yake hayo mawili (kuzalidha kwa ulaji wa ndani na kujenga uwezo wa nguvu kazi)?
b. Kwanini hata baada ya yale yaliyoitwa mabadiliko ya uchumi bado viwanda vingi vilikufa au kudumazwa wakati kinadharia na kihalisia tumekuwa na ongezeko kubwa la watanzania wenye ujuzi na uzoefu kuliko wale walioanza baada ya Uhuru?
c. Ni kwa namna gani katika uchumi huu mpya bado tunaweza kufufua baadhi ya viwanda hivyo na kutafuta namna mpya ya umiliki wa viwanda vya umma kama kwa kutumia mtindo wa hisa za mojwa kwa moja kwa wananchi na taasisi binafsi za wananchi?
d. Serikali inaweza vipi kutengeneza mazingira yanayoweza kuboresha uendeshaji wa viwanda hivi aidha kwa mtindo wa private-public patnership au mtindo wowote ambao utahakikisha wamiliki wanapata faida, kizalishwacho ni cha ubora wa kisasa na vile vile ni endelevu?
e. Ni viwanda vipi ungependa unaona vinafufuliwa kwa misingi hiyo hapo juu na kwanini?