Sera za ccm na jk zazidi kufa...shule la kata kufeli kwa 80% ni jubu kwa umma. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sera za ccm na jk zazidi kufa...shule la kata kufeli kwa 80% ni jubu kwa umma.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Not_Yet_Uhuru, Jan 28, 2011.

 1. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wana JF;
  Mengi yamekuwa yakisemwa kuhusu uanzishwaji holela wa Sekondari ya Kata '(yeboyebo)' na kwa wachambuzi wa masuala ya maendeleo na sera walionya kuwa mwendo huu wa CCM na Serikali yake kuanzisha shule za mkupuo kwa malengo ya kisiasa ni ishara ya kukosa umakini na kutokuzingatia hali ya baadaye ya taifa kielimu lakini CCM walikanusha na kila siku wanataja uanzishwaji wa Serondari hizi kama ufanisi wao kisera!

  Kulingana na Matokeo halisi ya Kidato cha nne yaliyotoka, mbali na wasichana kuongoza, shule za kata ndizo zilizofeli kupindukia, na kati ya shule zote za kata, zaidi ya 80% wamefeli vibaya, na hawawezi kuendea. Kwa maana nyingine, ni chini ya 20% ndio angalau wamefaulu kuendelea. Hii imetajwa kama 'JANGA KWA KITAIFA' (Source: Nipashe -28/02/2011)

  Janga hili kitaifa linamaanisha nini??

  • Wazazi woote walioshawishiwa na Serikali kupeleka watoto wao Sekondari za kata, wameingia shimoni, kwa miaka yao yote minne (4) imepotea bure, wamerudi vijijini kuanza kuhangaikia maisha mbadala.
  • Wazazi wao wamevurugwa malengo yao yote kuhusu future ya watoto wao na hivyo maendeleo ya jumla ya kufikra na kijamii yameathirika.
  • Mbali na ukweli wa kuanguka huko kwa Sekondari za Kata, ukweli unabaki kuwa, shule hazina vifaa, waalimu, na pia wanafunzi wengi wanapelekwa huko bila hata kujua kusoma au kuandika na hivyo kufeli huku ni continuous, hakutaishia hapa.
  Hii ni ishara nyingine kuwa CCM na Serikali yake vinaangamiza uhai na dira ya taifa kwa kuua nguvu ya vijana hawa na hivyo kurudisha nyuma harakati za kulikomboa taifa ili wao waendelee kubaki kutawala mbali na ukweli kuwa wameshapoteza dira!

  Nomba kuwasilisha Great Thinkers...kwa mjadala....

  KATA4.jpg KATA5.jpg
   

  Attached Files:

 2. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Sera za Fisadi Kikwete na bado sana dawa ni kumuondoa huyu nduli CCM na Kikwete ndio nchi itaendelea :laugh:
   
 3. m

  mosquito Member

  #3
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  labda mlimwambia JK tunauhaba wa housegirls majumbani......yote ni dalili za kufeli kwa JK,ntaandika kitabu ntakiita ''The rise and fall of JK''
   
Loading...