Sera ya Vyuo Vikuu kubakiza wahitimu wenye ufaulu wa juu badala ya kuajiri wasomi walio- practice unaathri ubora wa elimu inayotolewa vyuoni

Watu upgrade sisi walimu wa sekondari twende kufundisha vyuo vya kati na vyuo vya kati wawe wanapanda waende kufundisha vyuo vikuu.
Unazifahamu sifa za kufundisha chuo kikuu? Tafuta hizo sifa uone kama unazo. Nijuavyo kufundisha ngazi ya sekondary au chuo cha kati siyo mojawapo ya sifa za msingi za kufundisha chuo kikuu
 
Kama ningewashauri serikali namna ya kuleta mageuzi katika elimu ya vyuo vikuu ningewaambia wafate model inayofanyika huko kwa vyuo vikuu vilivyotangulia. Kwenye hivyo vyuo vikuu waalimu wa vyuo vikuu hawaajiriwi kama njugu. Mwalimu wa Chuo Kikuu anapaswa awe mtu mkubwa sana, ili aitendee haki ile nafasi yake.

Wenzetu wanafanya hivi: kwa mfumo wa Western Universities na hata Easten huko Uchina, Japan, South Korea, Singapore, Indonesia, waalimu wa vyuo vikuu wanaitwa PIs (Principal Investigators). Principal Investigators ndio viini vya taaluma za vyuoni. Wanawajibika katika kuanzisha research agenda, kutengeneza research teams, kuattract research funding, kuhire research assistants kama postdocs na tecnicians, kurecruit PhD na Master students. Na kwa vile hawa watu watahitaji budget kubwa pale vyuo vinapotaka kuwaajiri hawaajiriwi kama njugu. Ni lazima itengwe initial budget ya kutosha kuajiri PI (wao wanaita seed funding) ili baadaye aweze kukiingizia chuo fedha zaidi kupitia grants atakazoattract. Department moja ya kitaaluma inaweza kuwa na PI 12 tu, halafu staff waliobaki ndani ya department wanafanya kazi chini ya hao PIs kwenye supporting roles. Ni ka mfumo ka ubepari vyuoni, lakini kako effective.

Hapa kwetu tunafanya tofauti. Mtu anaajiriwa kuanzia tutorial assistant (degree moja) hadi PhD. Wote hawa wanaajiriwa kupitia mfumo wa kawaida wa ajira serikalini. Akifika pale chuoni kama mwajiriwa mpya atapewa ofisi tu na courses atakazofundisha. Huyu mtu anatofauti gani na mwalimu wa sekondari? Wale tutorial assistants wataambiwa waende shule kwanza wapate masters. Ni utoto yaani, maana katika hiyo model hauwezi kupata excellence. Kama tunataka mabadiliko katika vyuo vyetu vikuu ni lazima mapinduzi yafanyike katika namna chuo kinavyoajiri wanataaluma wake. Lazima waajiriwe wanataaluma wachache wenye sifa na ubora wa juu kulingana na malengo ya chuo, lakini watakaowezeshwa vya kutosha ili wakiletee chuo tija katika malengo ya uwepo wa chuo hicho. Wenye sifa hizo wanaweza kupatikana kupitia uzoefu wao ndani na hata nje ya nchi.
 
Mbona kuna ofisi nyingi watu wanajitolea kufanya kazi ili kujiongezea umahili wa vitendo.Shida kama mnawaza kupiga pesa haraka haraka mtashindwa kupractise.
Unajitolea ukiwa na uwezo wa kujipandisha basi na kujilisha mchana 😂😂😂!!!

Kama ada ilikuwa inachangwa na kikao cha ukoo unadhani kujitolea ni rahisi mzee!?
 
Tatizo hamuelewi

Hao wanajikita sana kwenye research ya kila aina ya fani husika tofauti na huyo anaye practize ofisini.Maofisini kuna specialization kubwa.Mtu anafanya kakitu kamoja tu kadogo na jina anapewa kubwa mno hajui kwa upana field yote

Mfano mdogo unakuta ofisi zimejaa wahasibu lakini kaangalie wanachofanya unamkuta mwingine kazi yake miaka 20 ni income accountant anashughulika na mapato tu ya serikali mwingine ni expenditure accountant miaka nenda rudi na mwingine ni payroll accountant miaka nenda rudi huyo ukipeleka chuo kikuu ataenda kufundisha nini?

Haya unaenda kukutana na afisa biashara kasoma ana digrii mbili za biashara yuko serikalini miaka 20 kazi yake kutoa leseni za biashara chuo kikuu ukimpeleka ataenda kufundisha nini ?

Kuna mwingine unakuta ni Afisa masoko kazi yake kupeleka matangazo kwenye vipindi vya redio na television chuo kikuu ukimpeleka ataenda kufundisha nini?
You have a point brother! Sababu mie pia nimeenda fields mbili tofauti ila hakuna cha ajabu nilichojifunza! Zaidi niliishia kufanya kazi ya data entry tu kipindi natafta diploma ya IT na hapo ni TRA kikubwa tu niliasista kwenye installation ya kompyuta za Tancis zile!

Kwenye marketing ndio dah, hata sikumbuki la maana ni lipi! Ila ukinipa vitini niwamezeshe madogo madesa niko vizuri sana yani!
 
Elimu yetu sehemu kubwa ni theory, na walimu wetu ambao nao ni zao la theory wanafundisha bila hata ku-practice field husika, halafu eti tunatarajia tuweze kuwa na wahitumu wenye viwango! Itawezekana kweli?

✔✔💯%
 
Unajua mtu analeta hoja bila kutafakari. Wale vijana wanabakizwa ili wafundishe Chuo Kikikuu. Sasa huko mtaani kuna Chuo Kikuu kipi cha kufanyia mazoezi ya ku-practice field yake ndipo arudi Chuo Kikuu kufundisha? Yaani huo uzoefu wa Kufundisha Chuo Kikuu ataupata wapi kama siyo hapo hapo Chuo Kikuu. Yeye anafikiri hao maprofessor wazoefu walikuwa waki-practice fields zao mitaani ndipo wakarudi Chuoni Kufundisha. Hii siyo kweli. Kwanza wakibakizwa kwenye fields zao kuna wazoefu wanaowalea kwanza (mentorship) kwenye fields zao kabla ya kuingia darasani kufundisha. Wanaanza kwa kuzoezwa kusimamia seminars kisha wanaendelezwa zaidi kitaaluma ndipo wanaanza kufundisha. na somo moja wanaweza kufundisha wazoefu na wapya. Ni utaratibu mzuri kabisa huu wa kuzoea mazingira ya kazi badala ya kuwaleta eti wa mitaani walio-practice fields zao. Ku-practice field yako mtaani ni tofauti na kufundisha chuo kikuu
Na ndiyo maana mtu anaajairiwa akiwa tutorial Assistant, na hapa hafundishi kabisa Bali anawasaidia tu ma lecture huku akijifunza. Then ataenda masters ambapo atajifunza zaidi kuhusu fani yake na kufanya utafiti, lakini pia ili awe lecture ataongeza PhD. So mpaka kufika huku kashaiva
 
Kama ningewashauri serikali namna ya kuleta mageuzi katika elimu ya vyuo vikuu ningewaambia wafate model inayofanyika huko kwa vyuo vikuu vilivyotangulia. Kwenye hivyo vyuo vikuu waalimu wa vyuo vikuu hawaajiriwi kama njugu. Mwalimu wa Chuo Kikuu anapaswa awe mtu mkubwa sana, ili aitendee haki ile nafasi yake.

Wenzetu wanafanya hivi: kwa mfumo wa Western Universities na hata Easten huko Uchina, Japan, South Korea, Singapore, Indonesia, waalimu wa vyuo vikuu wanaitwa PIs (Principal Investigators). Principal Investigators ndio viini vya taaluma za vyuoni. Wanawajibika katika kuanzisha research agenda, kutengeneza research teams, kuattract research funding, kuhire research assistants kama postdocs na tecnicians, kurecruit PhD na Master students. Na kwa vile hawa watu watahitaji budget kubwa pale vyuo vinapotaka kuwaajiri hawaajiriwi kama njugu. Ni lazima itengwe initial budget ya kutosha kuajiri PI (wao wanaita seed funding) ili baadaye aweze kukiingizia chuo fedha zaidi kupitia grants atakazoattract. Department moja ya kitaaluma inaweza kuwa na PI 12 tu, halafu staff waliobaki ndani ya department wanafanya kazi chini ya hao PIs kwenye supporting roles. Ni ka mfumo ka ubepari vyuoni, lakini kako effective.

Hapa kwetu tunafanya tofauti. Mtu anaajiriwa kuanzia tutorial assistant (degree moja) hadi PhD. Wote hawa wanaajiriwa kupitia mfumo wa kawaida wa ajira serikalini. Akifika pale chuoni kama mwajiriwa mpya atapewa ofisi tu na courses atakazofundisha. Huyu mtu anatofauti gani na mwalimu wa sekondari? Wale tutorial assistants wataambiwa waende shule kwanza wapate masters. Ni utoto yaani, maana katika hiyo model hauwezi kupata excellence. Kama tunataka mabadiliko katika vyuo vyetu vikuu ni lazima mapinduzi yafanyike katika namna chuo kinavyoajiri wanataaluma wake. Lazima waajiriwe wanataaluma wachache wenye sifa na ubora wa juu kulingana na malengo ya chuo, lakini watakaowezeshwa vya kutosha ili wakiletee chuo tija katika malengo ya uwepo wa chuo hicho. Wenye sifa hizo wanaweza kupatikana kupitia uzoefu wao ndani na hata nje ya nchi.
Una wazo zuri ila kutekelezeka ndio ngumu hasa katika nchi za Africa.
Tangaza leo kazi ya chemical engineer mwenye PhD kama utapata.
Labda useme serikali ianzishe center of excellence moja halafu ichukue watafiti kokote kule duniani iwajaze hapo kitu ambacho pia haiwezi sababu haitaweza hata kuwalipa vizuri.
Ni bora tuendelee na mfumo huu huu wa kuajiri juniors halafu wakasome. Pia huo mfumo wa kubakiza kwa sasa haupo ajira huwa zinatangazwa na huyo mwenye GPA kubwa ashindane na wenzake.
 
Utaratibu huu ambao ndio kama sera ya vyuo vikuu vingi nchini kiliwemo Chuo Kikuu cha Dar -es-Salaam, sio tu umepitwa na wakati, bali pia haufai kwani unachangia vyuo kuwa na walimu ambao hawaja-practice katika field wanazofundisha na hivyo kuzalisha wasomi wenye kukosa maarifa na uzoefu kutoka kwa watu waliofanya kazi kwenye field husika.

Utaratibu huu ulifaa miaka ya nyuma ambapo wasomi walikuwa ni wachache lakini sio leo hii ambapo wasomi ni wengi wakiwemo waliofanya kazi katika field husika.

Mtu ambae amemaliza chuo na kupata first class kisha akaunganisha masters na baadae PhD ila hajafanya kazi katika field husika, sidhani kama anaweza kuwa mwalimu mzuri zaidi ya kubobea kwenye theory tu.

Pamoja na uwepo wa mafunzo kwa vitendo baada ya theory za darasani wakati wa likizo, bado kuna umuhimu mkubwa wa taaluma katika vyuo vyetu kutolewa na watu wenye sifa na moja ya sifa ya ziada ila muhimu ni walimu wawe walau wamefanya kazi katika field wanayofundisha.

Najua kwa baadhi ya field inaweza kuwa ni changamoto kupata na kuajiri wataalamu /wasomi wa kufundishia walioko katika field, ila vyuo bado vinaweza kutenga muda wa wataalamu hawa kuja kutoa mihadhara kwa utaratibu wa part- time vyuoni.

Tukikubali kutazama upya utaratibu huu na kuufanyia marekebisho kadri inavyowezekana, bila shaka tutakuwa na nafasi ya kuzalisha wasomi wazuri wanaoweza kushindana na wasomi kutoka katika mataifa mengine katika soko la ajira na hata katika kujiajiri.

Elimu yetu sehemu kubwa ni theory, na walimu wetu ambao nao ni zao la theory wanafundisha bila hata ku-practice field husika, halafu eti tunatarajia tuweze kuwa na wahitumu wenye viwango! Itawezekana kweli?

Tujitafakari.
Hoja ina mashiko tatizo ktk hizo field kunakuwa na shida ya ajira.
Wangeweza kuchukua waTZ wanaofanya ktk makpuni, taasisi au mashirika makubwa na kuwaomba kuja kufundisha kwa semester kama wanavyofanya vyuo duniani
 
Watu upgrade sisi walimu wa sekondari twende kufundisha vyuo vya kati na vyuo vya kati wawe wanapanda waende kufundisha vyuo vikuu.
Inawezekana kabisa ndugu regardless una gpa ya 3.8 undergraduate na 4.0 masters degree.
Kama mtu anavigezo na experience ya kutosha hakuna anaemzuia nikusubiri tangazo na kutuma maombi nashangaa mtoa mada anakuja kulia lia humu utadhani kuna mtu kamzuia kutuma maombi .
 
Una wazo zuri ila kutekelezeka ndio ngumu hasa katika nchi za Africa.
Tangaza leo kazi ya chemical engineer mwenye PhD kama utapata.
Labda useme serikali ianzishe center of excellence moja halafu ichukue watafiti kokote kule duniani iwajaze hapo kitu ambacho pia haiwezi sababu haitaweza hata kuwalipa vizuri.
Ni bora tuendelee na mfumo huu huu wa kuajiri juniors halafu wakasome. Pia huo mfumo wa kubakiza kwa sasa haupo ajira huwa zinatangazwa na huyo mwenye GPA kubwa ashindane na wenzake.
Ni vile tu watanzania hatupendi kubadilisha mifumo tuliyoizoea, na tunapenda kuishi kwenye comfort zones zetu. Tukipata kiongozi hata wa ngazi ya wizara mwenye maono na elimu ya juu na mwenye uthubutu kuubadlisha mfumo wa kitaaluma vyuo vikuu si ngumu kivile. Ni suala la kibajeti, pamoja na ushirikishwaji wa diaspora pamoja na watanzania wenye sifa waliomo nchini. Kuna watu hapa Tanzania ni maPI tayari na wanaendesha tafiti zao kwa mfumo wenye tija. Kuna mtu mmoja Dr. Joseph Ndunguru, huyu ni mtaalamu wa molecular biology na biotechnology zamani alikuwa MARI (Mikocheni Agricultural Research Institute) na ni PI wa ukweli. Ila eti undergraduate hakuwa na GPA ya 3.8 hivyo hakidhi sifa za kuajiriwa chuo kikuu! Utoto tu. Na bado kuna watanzania wa kutosha walio maPI huko nje ya nchi.

Unapobadilisha mfumo wa elimu ya juu ili kutengeneza maPI si lazima maPI wote wawe wazawa. Ujuzi na maarifa haviangalii uzawa, kabila au rangi. Weka fursa, weka dau, tangaza fursa duniani kote na kama mwenye sifa amepatikana kutoka Brazil mwache aje awe PI UDSM. South Africa wanarecruit ma PIs all over the world, US wanarecruit PIs all over the world, China (wacommunist wale) wanarecruit PIs all over the world, Botswana hivyo hivyo na sababu ni kwamba PIs ni watu highly skilled tena kwenye rare skills zinazohamasisha uchumi wa nchi kwa haraka, na watu wenye hizo skills wanaziuza kama biashara. Nchi ambazo zimebaki kuendesha vyuo vyao kama sekondari ndizo zimebaki kuwa nchi maskini na kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya kiwango cha ubora wa ujuzi na maarifa ngazi ya vyuo vikuu na kiwango cha uchumi wa nchi.
 
Prof Kabudi ni wakili ambaye hajawahi kufanya shughuli za uwakili, lakini Dr Mwakyembe amefanya sana shughuli za uwakili miaka ya 90's hadi 2000's mwanzoni: Hawa wote wawili ni wanasheria wazuri sana.

Tatizo kubwa ambalo linaikumba nchi yetu ni tabia ya kuchanganya utaalamu na siasa za kujikomba kwa watawala (Intellectual Sycophancy) ambalo limewakumba wanazuoni wetu wengi. Tukifanikiwa kutenganisha siasa na utaalamu naamini tutafika mbali sana...
Kwa hiyo Prof kabudi ni sawa na judge sinde warioba au judge Julie, hutakuta mahali wamehukumu Kesi ila title zao ni kubwa
 
Warioba amekuwa Jaji wa Mahakama ya Afrika mashariki na Mahakama ya Kimataifa ya mipaka ya bahari (Special Tribunal on the law of the sea). Ukisoma kesi za hizi mahakama mbili utaliona sana jina la Jaji Warioba. Lakini Warioba ana jina kubwa kwasababu amewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Tanzania.

Prof Kabudi yeye mbali na kuwa Corporate Counsel wa University of Dar-es-salaam, kufundisha na kuandaa machapisho mbalimbali: Hajawahi kufanya shughuli za uwakili sehemu yoyote ile kama wenzake wakina Rutinwa, Luoga na Fimbo.
 
Title ya ujudge, hata hivyo umetetea vyema learned counsel
 
Kama ningewashauri serikali namna ya kuleta mageuzi katika elimu ya vyuo vikuu ningewaambia wafate model inayofanyika huko kwa vyuo vikuu vilivyotangulia. Kwenye hivyo vyuo vikuu waalimu wa vyuo vikuu hawaajiriwi kama njugu. Mwalimu wa Chuo Kikuu anapaswa awe mtu mkubwa sana, ili aitendee haki ile nafasi yake.

Wenzetu wanafanya hivi: kwa mfumo wa Western Universities na hata Easten huko Uchina, Japan, South Korea, Singapore, Indonesia, waalimu wa vyuo vikuu wanaitwa PIs (Principal Investigators). Principal Investigators ndio viini vya taaluma za vyuoni. Wanawajibika katika kuanzisha research agenda, kutengeneza research teams, kuattract research funding, kuhire research assistants kama postdocs na tecnicians, kurecruit PhD na Master students. Na kwa vile hawa watu watahitaji budget kubwa pale vyuo vinapotaka kuwaajiri hawaajiriwi kama njugu. Ni lazima itengwe initial budget ya kutosha kuajiri PI (wao wanaita seed funding) ili baadaye aweze kukiingizia chuo fedha zaidi kupitia grants atakazoattract. Department moja ya kitaaluma inaweza kuwa na PI 12 tu, halafu staff waliobaki ndani ya department wanafanya kazi chini ya hao PIs kwenye supporting roles. Ni ka mfumo ka ubepari vyuoni, lakini kako effective.

Hapa kwetu tunafanya tofauti. Mtu anaajiriwa kuanzia tutorial assistant (degree moja) hadi PhD. Wote hawa wanaajiriwa kupitia mfumo wa kawaida wa ajira serikalini. Akifika pale chuoni kama mwajiriwa mpya atapewa ofisi tu na courses atakazofundisha. Huyu mtu anatofauti gani na mwalimu wa sekondari? Wale tutorial assistants wataambiwa waende shule kwanza wapate masters. Ni utoto yaani, maana katika hiyo model hauwezi kupata excellence. Kama tunataka mabadiliko katika vyuo vyetu vikuu ni lazima mapinduzi yafanyike katika namna chuo kinavyoajiri wanataaluma wake. Lazima waajiriwe wanataaluma wachache wenye sifa na ubora wa juu kulingana na malengo ya chuo, lakini watakaowezeshwa vya kutosha ili wakiletee chuo tija katika malengo ya uwepo wa chuo hicho. Wenye sifa hizo wanaweza kupatikana kupitia uzoefu wao ndani na hata nje ya nchi.
P
Mkuu kwa sasa muongozo wa TCU ndiyo unafiatwa na vyuo vyote Tanzania. Nafasi hutangazwa na mwenye sifa huomba. Mambo yakubakizana yalikwisha. Vyuo hutangaza nafasi tofauti kuanzia tutorial assistant hadi full professor. Kila level ina qualification zake na kazi maalum ya kufanya. Waombaji hutoka nje ya chuo. Issue ni upatikanaji wa watu wenye sifa, je tunawatu wa kutosha?
Huko kwa wenzetu wanavitu viwili vikubwa 1. Research institutions nyingi katika nyanja tofauti na 2. Uwezo wa kulipa mishahara shindani kimataifa. Kwa hali hii wakitangaza kazi hupata watu wenye uzoefu au walomaliza degree za juu wakiwemo hao ma PI. Hapa kwetu hatuna phds wa kutosha (kumbuka phd ni research na academic degrees ). Hivyo vyuo lazima vijenge toka chini, yaani t.a. na hawa hupandishwa vyeo kwa vigezo maalumu na hopefully kila wanapopanda ujuzi huongezeka.
Kuhusu model yako ya PI ina tatizo ya kuwa huwezi kuitumia kwa kila nafasi na kila chuo. PIs basically ni waongoza utafiti fulani na siyo position kama ya uprofessor na ndio maana hata hapa kwetu kila research project huongozwa na PI. Ma PI huwa wameonyesha uwezo wa kuandika mradi na kuvuta hela za utafiti tofauti na kufundisha. Kama unahitaji mtu wa aina hiyo na wako wachache nchini kwako na huna pesa ya kulipa wa nje basi utakwama tu.
Lingine ni kuwa Tanzania iko nyuma sana tena saana kwenye kusomesha wataalamu tu wategemezi wa misaada na miradi. Wengi wa Masters na PhDs either ni private students au miradi kutoka nje hii inapunguza uwezo wetu wa kuzalisha wataalamu kama nchi. Hivyo hata hii model ya t.a hadi profesa inaface changa moto.
Mwisho naamini political will na commitment ndio dawa ya kutusogeza. All the best.
 
Back
Top Bottom