Sera ya Vyuo Vikuu kubakiza wahitimu wenye ufaulu wa juu badala ya kuajiri wasomi walio- practice unaathri ubora wa elimu inayotolewa vyuoni

Jamaa ana point! Hao wanafunzi wenye first class hio practical wanaifanyia wapi ambapo kuna kazi za proffessional zao? Au wataifanyia mtaani kwa kuanza kufanya biashara za ubuyu na kupost nguo mtandaoni?
na wewe ujaelewa kitu,umekurupuka kucoment bila kusoma uzi kama inavyotakiwa: hili ndo tatizo la Wadanganyika wengi🤣 Mtoa mada anashauri Walimu wa Vyuo wawe wale ambao wanatokea mtaani baada ya kufanya kazi kwa miaka kadhaa,Wasichukukiwe wale direct from School ili waweze fundisha kwa umakini na kutumia uzoefu wao na changamoto walizokutana nazo wakiwa kazini kwa new generation,sasa hivi ni kama vile Kipofu kuongoza Kipofu mwenzake.....mtu ajawai mathalani kufunga ata mnara mmoja wa simu,au kufungua/kuasembo engine ata moja ati kwa kuwa amefaulu vyema anakuja kuwa mwalimu wa Automotive engineering au wa Telecom... Mfano Prof Assad kwa sasa yupo pale Muslim Unv Morogoro...Tuna amini wanafunzi walio chini yake watamaliza chuo wakiwa na uelewa mpana sana kwenye taharuma ya Uhasibu kuliko wale wanaofundishwa na Maprofessor ambao awajawai kuajiriwa au kijiajiri kwenye fani walizosomea
 
Na ndio maana kwa sasa serikali inapeleka wahitimu wengi wa kidato cha nne wenye ufaulu wa kati mf. DIV 2 dhaifu na DIV 3 vyuo vya kati kusoma Diploma.
Wakati nakua au tunakuwa tulikuwa tunaaminishwa ya kuwa au kuambiwa ys kuwa vyuo vya ufundi vinawafundisha vijana kazi na wanajua kazi kweli,nikakua mzee mzima nikapita katika baadhi ya vyuo hivyo,nilichokiona ni tofauti na nilichokisikia ni theory tu na ukikuta practical ni zile za zamani na zimeshapitwa na wakati katika ile hali ya vifaa.

Ukitaka kujua kazi kwanza ni kwa juhudi yako na kupenda unachokifanya na kuingia field husika. Hapa nawazungumzia mafundi wenzangu. Mfumo wetu wa elimu hado mbovu sana kuanzia ngazi za chini mpaka huko juu.
Huko ndio kwa kuzalisha fundi mchundo/ wasaidizi wa madaktari, mainjinia, wahasibu etc. Tatizo hapo kati tulidhani degree ni kwaajili ya kila mtu, sera ikawa kuongeza vyuo ili watu wapate degree. Hata wasio na uwezo wakaenda degree ya kwanza na ya pili ... wakasoma kwa shida kiasi lecturers wakaonekana wanawaonea.
Kwa fani za ufundi hasa sisi mafundi,walimu wetu pia wanatakiwa wawe mafundi hasa.

Lakini hata hao wenye uwezo walipofika vyuoni walifeli na wasio na uwezo wengine walifaulu. Haya mambo huwa yanataka kujitambua na mifumo kubadilishwa.

Mimi huwa nawaambia wadau kama ningepata wasaa wa kutoa maoni au kupewa mchongo wa kubadilisha mtaala katika shahada ya uhandisi wa umeme vijana wangepata ladha ya ufundi tangu wapo mwaka wa kwanza. Mfumo wetu unatupotezea muda sana sasa sijui wasomi wetu hawajiamini au shida ni ipi.
 
na wewe ujaelewa kitu,umekurupuka kucoment bila kusoma uzi kama inavyotakiwa: hili ndo tatizo la Wadanganyika wengi🤣 Mtoa mada anashauri Walimu wa Vyuo wawe wale ambao wanatokea mtaani baada ya kufanya kazi kwa miaka kadhaa,Wasichukukiwe wale direct from School ili waweze fundisha kwa umakini na kutumia uzoefu wao na changamoto walizokutana nazo wakiwa kazini kwa new generation,sasa hivi ni kama vile Kipofu kuongoza Kipofu mwenzake.....mtu ajawai mathalani kufunga ata mnara mmoja wa simu,au kufungua/kuasembo engine ata moja ati kwa kuwa amefaulu vyema anakuja kuwa mwalimu wa Automotive engineering au wa Telecom... Mfano Prof Assad kwa sasa yupo pale Muslim Unv Morogoro...Tuna amini wanafunzi walio chini yake watamaliza chuo wakiwa na uelewa mpana sana kwenye taharuma ya Uhasibu kuliko wale wanaofundishwa na Maprofessor ambao awajawai kuajiriwa au kijiajiri kwenye fani walizosomea
Uko sahihi kabisa. Ulimwengu huu wa sasa umekuwa na changamoto nyingi sana kuliko zamani,hautati story nyingi zaidi ya kutatua matatizo na kusonga mbele.
 
Mkuu Eyce, mleta mada anaamini kwamba kuwabakiza wanafunzi wenye ufaulu wa juu ni makosa. Sasa nashindwa kumuelewa kwasababu huu utaratibu uko dunia nzima, pia mtu huwezi kutoka kuwa Tutorial Assistant/Tutor na kupanda juu kuwa Assistant Lecturer hadi Lecturer bila kufanya tafiti na kuwa na uzoefu.

Pili, huwezi kufundisha wanafunzi wa shahada kama wewe bado una shahada. Utasaidia tu kazi chache-chache na ukipata shahada ya pili ndipo utaingia darasani. Lakini kubwa TCU imetoa utaratibu kwamba kila muhadhiri ni lazima aandike machapisho kadhaa ndani ya muda fulani.

Ukienda UDSM shule ya sheria waalimu karibia wote ni mawakili wazoefu na wameandika machapisho mengi na kufanya tafiti kubwa sana pengine kuliko vyuo vingine nchini Tanzania, sasa sifahamu alikuwa anazungumzia uzoefu upi labda.....
Maprofesor/ lecturer wanaoongoza Kwa kutoa machapisho mengi Tanzania nafikiri ni SUA . Most prereviewed journal
 
Utaratibu huu ambao ndio kama sera ya vyuo vikuu vingi nchini kiliwemo Chuo Kikuu cha Dar -es-Salaam, sio tu umepitwa na wakati, bali pia haufai kwani unachangia vyuo kuwa na walimu ambao hawaja-practice katika field wanazofundisha na hivyo kuzalisha wasomi wenye kukosa maarifa na uzoefu kutoka kwa watu waliofanya kazi kwenye field husika.

Utaratibu huu ulifaa miaka ya nyuma ambapo wasomi walikuwa ni wachache lakini sio leo hii ambapo wasomi ni wengi wakiwemo waliofanya kazi katika field husika.

Mtu ambae amemaliza chuo na kupata first class kisha akaunganisha masters na baadae PhD ila hajafanya kazi katika field husika, sidhani kama anaweza kuwa mwalimu mzuri zaidi ya kubobea kwenye theory tu.

Pamoja na uwepo wa mafunzo kwa vitendo baada ya theory za darasani wakati wa likizo, bado kuna umuhimu mkubwa wa taaluma katika vyuo vyetu kutolewa na watu wenye sifa na moja ya sifa ya ziada ila muhimu ni walimu wawe walau wamefanya kazi katika field wanayofundisha.

Najua kwa baadhi ya field inaweza kuwa ni changamoto kupata na kuajiri wataalamu /wasomi wa kufundishia walioko katika field, ila vyuo bado vinaweza kutenga muda wa wataalamu hawa kuja kutoa mihadhara kwa utaratibu wa part- time vyuoni.

Tukikubali kutazama upya utaratibu huu na kuufanyia marekebisho kadri inavyowezekana, bila shaka tutakuwa na nafasi ya kuzalisha wasomi wazuri wanaoweza kushindana na wasomi kutoka katika mataifa mengine katika soko la ajira na hata katika kujiajiri.

Elimu yetu sehemu kubwa ni theory, na walimu wetu ambao nao ni zao la theory wanafundisha bila hata ku-practice field husika, halafu eti tunatarajia tuweze kuwa na wahitumu wenye viwango! Itawezekana kweli?

Tujitafakari.
Ujerumani hauwezi kufundisha vyuoni kama hauja pactice ulichosomea kwa angalau miaka 5. Na hii ni hasa upande wa emgineering
 
Mkuu kwa sasa muongozo wa TCU ndiyo unafiatwa na vyuo vyote Tanzania. Nafasi hutangazwa na mwenye sifa huomba. Mambo yakubakizana yalikwisha. Vyuo hutangaza nafasi tofauti kuanzia tutorial assistant hadi full professor. Kila level ina qualification zake na kazi maalum ya kufanya. Waombaji hutoka nje ya chuo. Issue ni upatikanaji wa watu wenye sifa, je tunawatu wa kutosha?
Huko kwa wenzetu wanavitu viwili vikubwa 1. Research institutions nyingi katika nyanja tofauti na 2. Uwezo wa kulipa mishahara shindani kimataifa. Kwa hali hii wakitangaza kazi hupata watu wenye uzoefu au walomaliza degree za juu wakiwemo hao ma PI. Hapa kwetu hatuna phds wa kutosha (kumbuka phd ni research na academic degrees ). Hivyo vyuo lazima vijenge toka chini, yaani t.a. na hawa hupandishwa vyeo kwa vigezo maalumu na hopefully kila wanapopanda ujuzi huongezeka.
Kuhusu model yako ya PI ina tatizo ya kuwa huwezi kuitumia kwa kila nafasi na kila chuo. PIs basically ni waongoza utafiti fulani na siyo position kama ya uprofessor na ndio maana hata hapa kwetu kila research project huongozwa na PI. Ma PI huwa wameonyesha uwezo wa kuandika mradi na kuvuta hela za utafiti tofauti na kufundisha. Kama unahitaji mtu wa aina hiyo na wako wachache nchini kwako na huna pesa ya kulipa wa nje basi utakwama tu.
Lingine ni kuwa Tanzania iko nyuma sana tena saana kwenye kusomesha wataalamu tu wategemezi wa misaada na miradi. Wengi wa Masters na PhDs either ni private students au miradi kutoka nje hii inapunguza uwezo wetu wa kuzalisha wataalamu kama nchi. Hivyo hata hii model ya t.a hadi profesa inaface changa moto.
Mwisho naamini political will na commitment ndio dawa ya kutusogeza. All the best.
Upo sahihi sana katika maelezo yako kwamba vyuo vyetu viliona ni nafuu kujenga kuanzia chini (T.A) hadi kutengeneza professor.

Ila kuna tofauti kati ya kufanya kile kilicho nafuu (kilicho ndani ya uwezo wako) na kufanya jambo sahihi lakini linalohitaji maamuzi magumu. Ninachopendekeza ni mabadiliko makubwa katika mfumo wa elimu ya vyuo vikuu utakaohitaji maamuzi magumu yafanyike.

Elimu yetu ya chuo kikuu haiwezi tena kuhimili vishindo vya karne ya 21, yenye changamoto za ajira, mabadiliko tabia ya nchi, uchumi wa kidigital, magonjwa ya milipuko, n.k. Vyuo vyetu havipaswi tena kuwa teaching universities, lazima viwe strategic think tanks, research and solution oriented universities. Hii dhana inaaply kwenye field zote (kuanzia Kiswahili hadi Atomic Physics). Kwa sasa unaweza kushangaa watoto ngazi ya chuo kikuu wanaingia darasani kufundishwa irabu za Kiswahili na namna ya kuunda sentensi za Kiswahili. Kwa karne ya 21 tunapaswa kuwafundisha watoto namna gani Kiswahili kinaweza kutumika kupenyeza ajenda ya East Africa across the continent kiuchumi, kisiasa na kitamaduni. Kuna maana yake maana katika context ya utandawazi na itahitaji integration ya lugha, uchumi, siasa na usalama wa nchi. Ndio maana watoto wetu wakienda kufanya interviews na waajiri hawawezi kufikiri nje ya box na kulink mambo. Ni kazi ya PIs kuwa strategic thinkers, na kutengeneza wanafunzi strategic thinkers wengine kupitia ufundishaji na usimamizi.

Huu ni mfano tu, lakini unaapply hata kwenye disciplines zingine ikiwemo Sayansi, Kilimo, Biashara, Teknolojia, Uchumi, Ualimu, n.k, na nakwambia haya mambo yanahitaji yapewe kipaumbele na serikali kuangalia namna gania ya kuondoka kwenye traditional educational systems kwenda kwenye innovative educational systems. Kwa muktadha wa namna ambavyo Kikwete alimleta Maximo Maxime kiutoka Brazili akawa anamlipa milion 11 ili aiboost timu ya taifa, ndivyo Serikali inavyopaswa kulipa umuhimu suala la elimu ya chuo kikuu. Ni kosa la kimkakati kuwa na vyuo vikuu lukuki ambavyo huwezi kuvihudumia inavyostahili. Bora kuwa na vyuo vikuu vichache, vya kimkakati, utakavyoweza kupata PIs wenye sifa -- waendeshe vyuo vikuu kwa tija. Vyuo vikuu vinamsemo wa tangu zama za kale eti kazi yao ni Teaching, Research and Consultancy -- ukiwauliza nionyeshe mfano wa hizo consultancy zenu mnazofanya, utashangaa ni upuuzi mtupu maana wengine ndio kama hao akina REDET na siasa zao za huyu sijui anakubalika kwa asilimia ngapi. Hii nchi tayari inapoteza hela nyingi sana kwenye mifumo ya elimu isiyo na tija, na kila mwaka nchi inatenga takribani bilioni 400 kugharamia wanafunzi wanaosoma vitu vitu visivyo na maana na matokeo yake hawaajiriki. Hizi ni hela nyingi sana ukizistrategize zinaweza kubadilisha sana namna elimu yetu inavyoendeshwa. Kuna mambo mengi ya kushauri kuhusu hili lakini niishie hapa kwa sasa.
 
Nilimalizia kwa kusema tutahitaji political will and commitment. Tuna mfumo wa sauti moja nchi hii na maamuzi magumu labda yatoke juu vinginevyo funding inakuwa shida. Sasa hivi tuna mass production ya graduates karibu vyuo vyote. Na kama haitoshi hao ma phd ndio kila siku wanachaguliwa serikalini kwa kazi ambazo wenye degfee moja au masters wanazimudu. Hii inashusha quality ya elimu yetu na wahadhiri kutopata muda wa utafiti.
Hadi hapo tutakapo pata mtu wa kuchampion elimu kama mkombozi wetu na kuwa tayari kj invest strategically sioni mwanga. Mfumo wetu wote wa maamuzi unahitaji mabadiliko.
 
Wenye GPA za lower second tunadharaulika sana ila trust me. Nilishindana interview na vipanga wenye firts class nikawachakaza vibaya katika post ya meneja katika idara moja nyeti sana ya Umma mwaka jana October.

Nipo nafanya kazi na watu wakubwa sana hadi namshangaa Mungu.

Hakika usidharau confidence uliyonayo hiyo ni zaidi GPA Class yoyote.
 
Back
Top Bottom