Sera ya Vyuo Vikuu kubakiza wahitimu wenye ufaulu wa juu badala ya kuajiri wasomi walio- practice unaathri ubora wa elimu inayotolewa vyuoni

Kuna baadhi ya lecturers njuka ni wakomoaji bwana

Nilikuwepo napiga bachelor UDSM pale

Hahahahah ndio maana wanajitaftia experience pale pale ya kuwa makatili na kuanza kunyanyasa wenzao kupitia courseworks!

Hilo ndilo nalofahamu atleast for now!
 
Utaratibu huu ambao ndio kama sera ya vyuo vikuu vingi nchini kiliwemo Chuo Kikuu cha Dar -es-Salaam, sio tu umepitwa na wakati, bali pia haufai kwani unachangia vyuo kuwa na walimu ambao hawaja-practice katika field wanazofundisha na hivyo kuzalisha wasomi wenye kukosa maarifa na uzoefu kutoka kwa watu waliofanya kazi kwenye field husika.

Utaratibu huu ulifaa miaka ya nyuma ambapo wasomi walikuwa ni wachache lakini sio leo hii ambapo wasomi ni wengi wakiwemo waliofanya kazi katika field husika.

Mtu ambae amemaliza chuo na kupata first class kisha akaunganisha masters na baadae PhD ila hajafanya kazi katika field husika, sidhani kama anaweza kuwa mwalimu mzuri zaidi ya kubobea kwenye theory tu.

Pamoja na uwepo wa mafunzo kwa vitendo baada ya theory za darasani wakati wa likizo, bado kuna umuhimu mkubwa wa taaluma katika vyuo vyetu kutolewa na watu wenye sifa na moja ya sifa ya ziada ila muhimu ni walimu wawe walau wamefanya kazi katika field wanayofundisha.

Najua kwa baadhi ya field inaweza kuwa ni changamoto kupata na kuajiri wataalamu /wasomi wa kufundishia walioko katika field, ila vyuo bado vinaweza kutenga muda wa wataalamu hawa kuja kutoa mihadhara kwa utaratibu wa part- time vyuoni.

Tukikubali kutazama upya utaratibu huu na kuufanyia marekebisho kadri inavyowezekana, bila shaka tutakuwa na nafasi ya kuzalisha wasomi wazuri wanaoweza kushindana na wasomi kutoka katika mataifa mengine katika soko la ajira na hata katika kujiajiri.

Elimu yetu sehemu kubwa ni theory, na walimu wetu ambao nao ni zao la theory wanafundisha bila hata ku-practice field husika, halafu eti tunatarajia tuweze kuwa na wahitumu wenye viwango! Itawezekana kweli?

Tujitafakari.
Hivi hao walio-practice hizo field wangepataje huo uzoefu kama wasingeajiriwa? Sasa lazima tuzalishe wazoefu wengi. Tukisema ajira ni kwa walio-practice tu sasa hawa watoto wetu wanaomaliza shule na vyuo wataajiriwa wapi? Uzoefu hatuzaliwi nao, tunamwajiri asiye na uzoefu ili akate huo uzoefu. Tunampa ajira mtu ambaye hajapractice field husika ili a-practice field husika. Vinginevyo tutaendelea kubakia na wazoefu wachache na wanaendelea kuzeeka na kutwaliwa.

Wahurumie vijana wasio na ajira ndugu yangu. Haya masharti ya kazi ya eti awe ana uzoefu wa miaka kadhaa si rafiki kwa ulimwengu wa sasa wa vijana wengi kumaliza masomo na kukosa kazi kwa kubanwa na kigezo cha uzoefu. Labda kama una agenda nyingine dhidi ya young generation. Kwanza hawa wanaobakizwa na kuajiriwa vyuoni hukutana na wazoefu kwenye fields zao na kuelekezwa cha kufanya (Mentorship), wanapewa uzoefu na wazoefu kwenye fields zao. Hivi kama utasema hospitalini waajiriwe tu madaktari wazoefu itatusaidia nini mbeleni? Lakini madaktari wachanga wanafanya kazi na madaktari wazoefu na hatimaye nao wanakuwa wazoefu.
 
Jamaa ana point! Hao wanafunzi wenye first class hio practical wanaifanyia wapi ambapo kuna kazi za proffessional zao? Au wataifanyia mtaani kwa kuanza kufanya biashara za ubuyu na kupost nguo mtandaoni?
Tatizo hamuelewi

Hao wanajikita sana kwenye research ya kila aina ya fani husika tofauti na huyo anaye practize ofisini.Maofisini kuna specialization kubwa.Mtu anafanya kakitu kamoja tu kadogo na jina anapewa kubwa mno hajui kwa upana field yote

Mfano mdogo unakuta ofisi zimejaa wahasibu lakini kaangalie wanachofanya unamkuta mwingine kazi yake miaka 20 ni income accountant anashughulika na mapato tu ya serikali mwingine ni expenditure accountant miaka nenda rudi na mwingine ni payroll accountant miaka nenda rudi huyo ukipeleka chuo kikuu ataenda kufundisha nini?

Haya unaenda kukutana na afisa biashara kasoma ana digrii mbili za biashara yuko serikalini miaka 20 kazi yake kutoa leseni za biashara chuo kikuu ukimpeleka ataenda kufundisha nini ?

Kuna mwingine unakuta ni Afisa masoko kazi yake kupeleka matangazo kwenye vipindi vya redio na television chuo kikuu ukimpeleka ataenda kufundisha nini?
 
Jamaa ana point! Hao wanafunzi wenye first class hio practical wanaifanyia wapi ambapo kuna kazi za proffessional zao? Au wataifanyia mtaani kwa kuanza kufanya biashara za ubuyu na kupost nguo mtandaoni?
Unajua mtu analeta hoja bila kutafakari. Wale vijana wanabakizwa ili wafundishe Chuo Kikikuu. Sasa huko mtaani kuna Chuo Kikuu kipi cha kufanyia mazoezi ya ku-practice field yake ndipo arudi Chuo Kikuu kufundisha? Yaani huo uzoefu wa Kufundisha Chuo Kikuu ataupata wapi kama siyo hapo hapo Chuo Kikuu. Yeye anafikiri hao maprofessor wazoefu walikuwa waki-practice fields zao mitaani ndipo wakarudi Chuoni Kufundisha. Hii siyo kweli. Kwanza wakibakizwa kwenye fields zao kuna wazoefu wanaowalea kwanza (mentorship) kwenye fields zao kabla ya kuingia darasani kufundisha. Wanaanza kwa kuzoezwa kusimamia seminars kisha wanaendelezwa zaidi kitaaluma ndipo wanaanza kufundisha. na somo moja wanaweza kufundisha wazoefu na wapya. Ni utaratibu mzuri kabisa huu wa kuzoea mazingira ya kazi badala ya kuwaleta eti wa mitaani walio-practice fields zao. Ku-practice field yako mtaani ni tofauti na kufundisha chuo kikuu
 
Mkuu rejea kwenye msingi wa vyuo vikuu. Kazi ya vyuo vikuu sio kuandaa practioners bali critical thinkers! Haya ya practical yako vyuo vya kati.
Wewe ndiye umenena. Ni makosa makubwa kufikiri kuwa Vyuo vikuu ni ku-practice au kutatua matatizo. Wao ni kukupa maarifa wewe ya kutafakari na kufikiri kimantiki kulingana na unachokutana nacho na kukitafutia ufumbuzi, na siyo eti unaenda kwa professor akutatulie. hiyo siyo kazi ya vyuo vikuu. Hiyo ni kazi ya vyuo vya kati. Universities ni kutengeneza Theories za kutumia kutoa utatuzi wa jambo au za kukuongoza kufikiri na kuamua kulingana na mazingira, na siyo kukupa majibu ya matatizo yako. Vyuo vikuu ni think tanks za kuzalisha critical thinkers
 
Na ndio maana kwa sasa serikali inapeleka wahitimu wengi wa kidato cha nne wenye ufaulu wa kati mf. DIV 2 dhaifu na DIV 3 vyuo vya kati kusoma Diploma.

Huko ndio kwa kuzalisha fundi mchundo/ wasaidizi wa madaktari, mainjinia, wahasibu etc. Tatizo hapo kati tulidhani degree ni kwaajili ya kila mtu, sera ikawa kuongeza vyuo ili watu wapate degree. Hata wasio na uwezo wakaenda degree ya kwanza na ya pili ... wakasoma kwa shida kiasi lecturers wakaonekana wanawaonea.

WaTZ tumesahau kuwa mwanafunzi unatakiwa ku fit kwenye mfumo wa chuo lakini siyu chuo kijishushe ili kuendana na sifa za wanafunzi vilaza. Hao vilaza wetu wakaajiriwa maofisini wakashindwa ku perform, wengine hata kujenga hoja kwenye vikao hawawezi.

Angalia bungeni, wasomi waliotakiwa kuwa critical thinkers hawawezi hata kujenga hoja, hata huo ujasiri hawana. Hao ndio watu tuliowalazimisha wapate degree wakati hawakustahili
Well said. Kwanza vyuo vikuu siyo kwa ajili ya wote bali ni kwa ajili ya wachache wenye manufaa kwa wengi, na siyo wengi wenye manufaa kwa wachache.
 
Athari nyingine ni ku-recycle knowledge zile zile. Mtu kasomea UD undergraduate anarudi hapo kufundisha mwanafunzi, naye mwanafunzi wake anarudi tena kufundisha hapo hapo. Kama mwalimu wa kwanza kuna kitu kilikuwa kinamsumbua, unageuka ugonjwa wa kizazi, ni bora wangekuwa hata wana-exchange kati ya chuo na chuo
Usiangalie upande mmoja tu, labda kama una mashaka na taaluma ya chuo husika. Kuna upande wa faida kwa maana kwamba kama Chuo Chenu ni bora basi huo ubora unakuwa endelevu. Ukifanya hiyo exchange na Chuo ambacho ni dhaifu kitaaluma maana yake unaleta ubovu na udhaifu kwenye chuo Chako. na kama chuo chako ni dhaifu na ukawabakiza wahitimu wako hapo unaendeleza udhaifu. Cha msingi ni kuangalia ubora wa Chuo Chako.
 
WaTZ tumesahau kuwa mwanafunzi unatakiwa ku fit kwenye mfumo wa chuo lakini siyu chuo kijishushe ili kuendana na sifa za wanafunzi vilaza.
Uko sahihio kipindi cha NYerere ilikuwa ukipata division one na two kidato cha sita marufuku kuajiriwa serikalini ilikuwa lazima uende chuo kikuu

Direct employment zilikuwa zikitolewa kwa waliopata division three na four

Alifanya hivyo ili apate viongozi baadaye baada ya kuona ana upungufu mkubwa wa viongozi hasa baada ya kutaifisha biashara kwenye azimio la Arusha wahindi na wazungu wakaondoka ghafla

Tatizo likawa hao ma failure walioajiriwa wakawa mbummbumbu hawajui lolote zaidi ya kufanya routine jobs za ukimwambia kaa hapo anakaa anafanya hicho hicho hajiongezi wala nini kwa kuwa upeo wao ulikuwa mdogo

Kila sekta utendaji ukawa mbovu na mishirika kupata hasara kibao na kufa sababu hiyo mi failure ilikuwa ikipanda ngazi hadi kuwa mibosi kila idara wakati vichwani haina kitu!!!

Baadaye serikali ilipoona kuna wasomi sasa wengi ikaleta zoezi la kupunguza wafanyakazi miaka ya 90 wasiosoma wengi wakabwagwa chini nafasi zikaanza kupewa wasomi ndio tukaanza kuona mabadiliko ya kidigitali nk maofisini utendaji ukaanza kubadilika kuwa mzuri zaidi na more proffessional.

Japo wengi walipunguzwa miaka hiyo lakini bado mingine ikajipenyeza ilipojua inatakiwa uwe na elimu jumla ilikuwa elfu 35 ikaamua kutengeneza vyeti feki hii ndio aliiotumbua kwa wingi Magufuli ili kuwasafishia njia vipanga waingie kwenye ajira


Vyuo vikuu wanaijua field kwa upana kuliko anayepractice kwenye area specialized moja sababu ya research maofisini mtu hafanyi research yeye kazi yake ni routine kwa hiyo uelewa wake wa field alipo haupanuki sana

Vyuo vikuu uzoefu wanao ndio maana hata makampuni makubwa huwafuata kwa ajili ya consultancy .
 
Mleta hoja nadhani wala haelewi system ya vyuo vikuu ilivyo, na vigezo vya kuajiliwa, kupanda vyeo nk.
Haelewi chochote kuhusu uendeshaji wa vyuo vikuu. yeye anafikiri kila mtu anaye-practice field mtaani basi ana vigezo vya kufundisha chuo kikuu. Pia anafikiri kila mwenye PhD ana sifa za kufundisha chuo kikuu. Siyo kweli hata kidogo.
 
Wewe ndiye umenena. Ni makosa makubwa kufikiri kuwa Vyuo vikuu ni ku-practice au kutatua matatizo. Wao ni kukupa maarifa wewe ya kutafakari na kufikiri kimantiki kulingana na unachokutana nacho na kukitafutia ufumbuzi, na siyo eti unaenda kwa professor akutatulie. hiyo siyo kazi ya vyuo vikuu. Hiyo ni kazi ya vyuo vya kati. Universities ni kutengeneza Theories za kutumia kutoa utatuzi wa jambo au za kukuongoza kufikiri na kuamua kulingana na mazingira, na siyo kukupa majibu ya matatizo yako. Vyuo vikuu ni think tanks za kuzalisha critical thinkers
Mtu ambaye hana practicle experience hawezi kukupa maarifa utakayokutananayo kwenye field zaidi ya theory za vitabuni tu.

Darasani na kuwa katika field ni vitu viwili tofauti.
 
Ukutane nao darasani sasa walivyo na mbwembwe kumbe wazee wa kumeza, kuna walimu wangu pale Mlimani nna hasira nao mpaka kesho, japo nnapanga kurudi hapo kuongeza elimu sijui nikikutana nao itakuaje maana wengi wana Phd sasahivi
Kwani kumeza ni tatizo? Unajua watu wanasoma lakini hawaelimiki. Kumeza ni sehemu ya maarifa. Tunaiita "recalling". Sasa wewe unaulizwa hata jina la Rais wa nchi yako huwezi kutaja jina lake halafu unasema eti "mimi siyo ya kumeza bali kuelewa". Sasa tutaelewaje kuwa umeelewa kama huwezi hata kutaja viungo vya mwili wako, ila unasema naulelewa mwili wangu. Jina la baba yako limeze, meza ili mtu akikuuliza utaje jina la baba yako uweze kutaja. Sasa hapo unataka uelewe, uelewe nini? Kuna vitu vya ku-recall vingi sana katika mchakato wa ujifunzaji. Usidharau kumeza utatia aibu siku moja na usomi wako wa kusema eti mimi ni msomi wa kuelewa tu siyo kumeza.
 
Mtu ambaye hana practicle experience hawezi kukupa maarifa utakayokutananayo kwenye field zaidi ya theory za vitabuni tu.

Darasani na kuwa katika field ni vitu viwili tofauti.
Wewe huelewi maana ya elimu. Hivi kwa mfano mimi najifunza mfumo wa Jua chuoni. Na wewe unasema sharti nifundishwe na mtu mwenye practical experience, nitampata wapi huyo aliyeishi kwenye jua? kwani wewe una chuki na maarifa ya kitabuni? Sasa unataka tupate wapi maarifa nje ya kitabu? Kwani hujui kuwa Vitabu ni mojawapo ya hifadhi ya maarifa? Hata wewe nakushauri ukiweza hamisha maarifa uliyonayo kichwani kwenye kwenye vitabu ili yawafaidie watu wengi zaidi kizazi na kizazi. Usife na maarifa kichwani, binadamu tunapita tu duniani, tunatoleka. Huoni kwa sasa hatuna mwendazake? Tulimshauri maono yake ayaweke kwenye mifumo akakataa, sasa kaenda zake na maono yake hata kama yalikuwa ni mazuri.
 
Tatizo hamuelewi

Hao wanajikita sana kwenye research ya kila aina ya fani husika tofauti na huyo anaye practize ofisini.Maofisini kuna specialization kubwa.Mtu anafanya kakitu kamoja tu kadogo na jina anapewa kubwa mno hajui kwa upana field yote

Mfano mdogo unakuta ofisi zimejaa wahasibu lakini kaangalie wanachofanya unamkuta mwingine kazi yake miaka 20 ni income accountant anashughulika na mapato tu ya serikali mwingine ni expenditure accountant miaka nenda rudi na mwingine ni payroll accountant miaka nenda rudi huyo ukipeleka chuo kikuu ataenda kufundisha nini?

Haya unaenda kukutana na afisa biashara kasoma ana digrii mbili za biashara yuko serikalini miaka 20 kazi yake kutoa leseni za biashara chuo kikuu ukimpeleka ataenda kufundisha nini ?

Kuna mwingine unakuta ni Afisa masoko kazi yake kupeleka matangazo kwenye vipindi vya redio na television chuo kikuu ukimpeleka ataenda kufundisha nini?
Tatizo wewe huelewi mfumo wa Chuo Kikuu. Chu Kikuu mtu mmoja hafundishi kila kitu, anafundisha eneo dogo la ubobezi.
 
Back
Top Bottom