Sera ya Ujamaa bado ipo Tanzania?

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Nakupenda nchi yangu Tanzania. Kipindi cha nyuma katika kufwata milengo ya miwli ya pande mbili Ujamaa na Ubeberu Sisi kama nchi Tuliamua kwenda upande wa Ujamaa tukiwa na nchi nyingine kama Russia,Cuba,Uchina...nk

Ujamaa ni hali ya kushare kwa usawa rasilimali zote zinazopatikana ndani ya nchi husika yawe madini,mafuta,mbuga za wanyama na hata fursa mbalimbali.

Sisi kama Tanzania kwa kipindi hiki bado tupo kwenye Sera za Kijamaa au tushaondoka huko?.Je kuna usawa katika kushare Keki ya Taifa au ndio tiyari nchi imekua ya kikundi cha watu wachache wenye mamlaka juu ya wengine.

Tunafanya maamuzi wote kama wajamaa au kuna classes za watu?wachache wakiwa matajiri sana na wengi wakiwa maskini wa kutupwa na wale maskini wakizidi kunyonywa mpaka tone la mwisho la damu.

Je katika utoaji wa madaraka tunatoa kijamaa au imebaki ile ya nani anamfahamu nani kama hujulikani inakua imekula kwako.

Sio kwamba tumetoka kwenye Sera za kijamaa na kwenda kwenye sera za kifalme nikimaanisha kwa sasa vyeo vinafwata koo/familia kama mzazi wako alikua flani nawe lazima uje uwe flani.

Tukirudi mtaani huku tunaishi Kijamaa kama zamani jirani akipika hata Viazi ataita watoto wote wa majirani na kugawana hata kama ni kiazi kimoja au ndio kila mtu anajifungia kwenye geti lake na kula vinono mwenyewe na kubaki na ile Kauli 'Watajijua wenyewe'

Bado huko kwenye utoaji wa Huduma za kijamii Afya, Elimu, usafirishaji...nk Huduma huko zinatolewa Kijamaa au ndio kuna VIP/VVIP na lower classes mkiachwa na Huduma mbovu mkibanana kwenye vyombo ya usafiri,misongamano mirefu kwenye kutafuta maji na Huduma za Afya.

Na kama tumehama kutoka kwenye mfumo wa Kijamaa kuna haja ya wananchi kutangaziwa ili kila mtu ajue atakula kutokana na urefu wa kamba yake.


Muwe na Jumamosi Njema.
 
Back
Top Bottom